TANZIA Profesa Gaudence Mpangala afariki dunia baada ya kuugua ghafla

Pole sana wafiwa.

Huyu ni kati ya maprofesa wachache ambao daima wamesimama kutetea weledi wao.

Tunamwomba Mungu mwenye huruma ampokee katika ufalme wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Insha Allah Mungu yupo, madaraka na dola vinadanganya watu kujiona wao Ni wao tu lakin mbele za Mungu mwanadamu Ni kapunje tu. Tunadanganywa Hakuna depotivo la corunaa, Ndugu zetu wameteketea lakin Insha Allah Mungu atatufanyia Njia pasipo na njia.
Ipinde kona kule...
 
Amepoteza uhai akipata matibabu Jijini Dodoma alfajiri ya leo.

Akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mingi kabla ya kuhamia Iringa kwenye Chuo Kikuu cha Ruaha

Profesa wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) mkoani Iringa, Gaudence Mpangala amefariki dunia jijini Dodoma leo asubuhi Alhamisi Februari 4, 2021 baada ya kuugua ghafla.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo mjukuu wa msomi huyo, Andrew Mpangala amesema, “babu alikuwa Dodoma kikazi lakini leo kati ya saa 2 na saa 3 asubuhi akiwa katika safari kuelekea kwenye kikao alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali na ilivyofika saa tano akafariki dunia.”

Amesema mara ya mwisho kuwasiliana na babu yake ilikuwa jana na alimuagiza amtumie taarifa mbalimbali alizotakiwa kuzifuata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kisha azitume Dodoma.

“Leo asubuhi nikapiga simu yake akapokea dereva wake ambaye aliniambia babu hali yake sio nzuri na amekimbizwa hospitalini. Pia dereva akaniambia hakuna mtu wetu wa karibu Dodoma ili aende kumuangalia mzee,” amesema.

Profesa Mpangala alikuwa mchambuzi wa masuala mbalimbali hasa ya siasa.

Andrew amesema mwili utapelekwa chuo cha RUCU kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na baada ya hapo utapelekwa Dar es Salaam.
LONG LIVE COMRADE
 
Kuna vichwa vya kuku na vibalaka wa mabeberu wamejitoa ufahamu,kila ugonwa na mtu akifa wanadhani Corona. Mungu ilaze roho ya Prof wetu mahala pema
 
Rip mwamb kanifungulia DS RUCu
Japo kuwa nilikuw na doji vipind vyake
 
Amepoteza uhai akipata matibabu Jijini Dodoma alfajiri ya leo.

Akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mingi kabla ya kuhamia Iringa kwenye Chuo Kikuu cha Ruaha

Profesa wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) mkoani Iringa, Gaudence Mpangala amefariki dunia jijini Dodoma leo asubuhi Alhamisi Februari 4, 2021 baada ya kuugua ghafla.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo mjukuu wa msomi huyo, Andrew Mpangala amesema, “babu alikuwa Dodoma kikazi lakini leo kati ya saa 2 na saa 3 asubuhi akiwa katika safari kuelekea kwenye kikao alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali na ilivyofika saa tano akafariki dunia.”

Amesema mara ya mwisho kuwasiliana na babu yake ilikuwa jana na alimuagiza amtumie taarifa mbalimbali alizotakiwa kuzifuata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kisha azitume Dodoma.

“Leo asubuhi nikapiga simu yake akapokea dereva wake ambaye aliniambia babu hali yake sio nzuri na amekimbizwa hospitalini. Pia dereva akaniambia hakuna mtu wetu wa karibu Dodoma ili aende kumuangalia mzee,” amesema.

Profesa Mpangala alikuwa mchambuzi wa masuala mbalimbali hasa ya siasa.

Andrew amesema mwili utapelekwa chuo cha RUCU kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na baada ya hapo utapelekwa Dar es Salaam.
Tumepoteza mtu mmoja muhimu sana kwa taifa letu ktk dunia ya sasa aliyebakia aliamua kutumikia elimu yake kikamilifu na si tumbo lake ameondoka na heshima yake tutamkumbuka daima

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Pana haja ya kumwambia mtu fulani na vibaraka wake kuwa kwa hili big NO!

Hadi wafe wangapi? Hadi afe nani?

Itoshe kusema kwamba this is too much.

Sasa basi!

RIP Profesa Mpangala.
Acheni kuwa mahawayani! Kwa akili yenu finyu mnadhani corona inaweza kusababisha kifo cha ghafla namna hiyo? Yaani uwe mzima wa afya ghafla unajisikia vibaya na ndani ya dakika chache au saa moja unaaga dunia. Kwa taarifa yenu hiyo itakuwa ni heart attack (myocardial infarction). Haiwezi kuwa corona by all means.
 
aiseeee....depotivo toka wamsajili suarez wanatisha mno........msimu huu watabaki wachache mno....
 
Acheni kuwa mahawayani! Kwa akili yenu finyu mnadhani corona inaweza kusababisha kifo cha ghafla namna hiyo? Yaani uwe mzima wa afya ghafla unajisikia vibaya na ndani ya dakika chache au saa moja unaaga dunia. Kwa taarifa yenu hiyo itakuwa ni heart attack (myocardial infarction). Haiwezi kuwa corona by all means.
Dr. Akili......ongezeni bidi basi tupate dawa......
 
Back
Top Bottom