ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Hata wwe vilevile ...Itaanza na wewe
itakubinua tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata wwe vilevile ...Itaanza na wewe
Siyo kila ugonjwa huwa una dawa au kutibika. Aina ya magonjwa ya binadamu idadi yake ni zaidi ya million mbili. Yanayotibika na yenye dawa za uhakika (80% efficacy) hayazidi elfu moja. Ndiyo maana binadamu na viumbe hai wengine lazima waendelee kufa, tupende tusipende, vinginevyo dunia haitatosha.Dr. Akili......ongezeni bidi basi tupate dawa......
Asante sana, Kuna kitu nilikuwa mbishi Sana, now napata uelewa. Nilikuwa na mgojwa at the Dead point mpaka madaktari walishangaa, Ila matokeo ya vipimo na maelezo ya Dr. Yanashabihiana na ulivyonijibu. Asante sana bro.Siyo kila ugonjwa huwa una dawa au kutibika. Aina ya magonjwa ya binadamu idadi yake ni zaidi ya million mbili. Yanayotibika na yenye dawa za uhakika (80% efficacy) hayazidi elfu moja. Ndiyo maana binadamu na viumbe hai wengine lazima waendelee kufa, tupende tusipende, vinginevyo dunia haitatosha.
Magonjwa mengi hayatibiki (hayana dawa au mbinu za kuyaponyesha) lakini kwa bahati nzuri mengine yanapona menyewe kutegemea na mtu mwenyewe na wakati wenyewe (haitabiliki). Virusi vya aina yote havina dawa ya kuviua kwani virusi havina uhai. Sasa utauaje kitu kisichokuwa na uhai? Bahati nzuri magonjwa ya virusi mengi hupona menyewe yaani uwezo wake wa kuua (case fatality) ni ndogo sana au ni sufuri.
Kwa mfano mafua ya virusi vya influenza virus case fatality yake huko Ulaya ni 0.2% yaani kila wagonjwa 1,000 wawili hufariki. Huku Afrika mafua ya influenza virus case fatality yake ni zero. Case fatality ya mafua ya virusi vya corona (cov-2) huko Ulaya ni 2% yaani kila wagonjwa 1,000 ishirini hufariki. Huku Afrika case fatality ya corona ni 0.1% yaani kila wagonjwa 1,000 wa corona mmoja hufariki. Viko virusi vingine case fatality yake ni kubwa. Kwa mfano virusi vya kichaa cha mbwa (rabies) case fatality yake ni 100% yaani wote wanaougua rabies kufa ni lazima, iwe Ulaya au Afrika ni 100%. Virusi vya surua ni 30%, ebola ni 80%, ukimwi ni 80% etc
Hivyo suala la dawa ya kuponya magonjwaya virusi forget about it. Hata kwa aina nyingi za saratani halipo. Ila mwanadamu hatachoka kufanya majaribio ya madawa au mbinu mbali mbali ya kuepuka au kupunguza vifo vitokanavyo na virusi na saratani.Suala la chanjo kwa virusi vya corona ni gumu kwani virusi hivi kama vilivyo virusi vya ukimwi hubadilika badilika kila wakati genetically na hivyo kuweza kukwepa chanjo zinazogunduliwa. Ni wakwepaji wazuri sana wa immune system. Wamekuwepo miaka million 50 kabla ya uwepo wa binadamu katika dunia hii. Binadamu ataondoka wa kwanza kwenye dunia na virusi vitakuwa vya mwisho kuondoka duniani. Last In First Out (LIFO) ndiyo mpango wa Mwenyezi Mungu. Hofu na taharuki ondoa. Mambo lazima yaendelee kama kawa.
Kwa Kinachoendelea sasa duniani kuna ulazima wa Kusumbuka Kuulizia sababu Kuu ya hivi Vifo vya Mfululizo hasa kwa Watu wazima wenye Umri wa kuanzia miaka 56 hadi 79 kwa hapa Tanzania?Amepoteza uhai akipata matibabu Jijini Dodoma alfajiri ya leo.
Akifundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mingi kabla ya kuhamia Iringa kwenye Chuo Kikuu cha Ruaha
Profesa wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) mkoani Iringa, Gaudence Mpangala amefariki dunia jijini Dodoma leo asubuhi Alhamisi Februari 4, 2021 baada ya kuugua ghafla.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo mjukuu wa msomi huyo, Andrew Mpangala amesema, “babu alikuwa Dodoma kikazi lakini leo kati ya saa 2 na saa 3 asubuhi akiwa katika safari kuelekea kwenye kikao alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali na ilivyofika saa tano akafariki dunia.”
Amesema mara ya mwisho kuwasiliana na babu yake ilikuwa jana na alimuagiza amtumie taarifa mbalimbali alizotakiwa kuzifuata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kisha azitume Dodoma.
“Leo asubuhi nikapiga simu yake akapokea dereva wake ambaye aliniambia babu hali yake sio nzuri na amekimbizwa hospitalini. Pia dereva akaniambia hakuna mtu wetu wa karibu Dodoma ili aende kumuangalia mzee,” amesema.
Profesa Mpangala alikuwa mchambuzi wa masuala mbalimbali hasa ya siasa.
Andrew amesema mwili utapelekwa chuo cha RUCU kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na baada ya hapo utapelekwa Dar es Salaam.