Profesa Handlay Mwafwenga mwenye digrii Tisa achukua fomu ya Uspika wa Bunge. Anena mazito

Kama CCM haitaki uwe spika hautakuwa spika, kama CCM haitaki uwe Rais, hautakuwa Rais na vile vile kama CCM haitaki uwe Jaji Mkuu hautakuwa Jaji mkuu hivyo basi maamuzi ya CCM yaheshimiwe🍺
 
Asante sana Profesa (9PhD's); tumekupata vizuri sana. Ningekuwa mbunge kura yangu ningekupa wewe. Lakini kwa kuwa CCM imejaa wachumiatumbo wa kutosha, sitegemei kama watakupa kura na kuwatosa wachumiatumo wenzao. Ni ngumu sana.
 
Kwanini wabunge wa JMT waliochukua fomu ni mmoja tu? Tena wa darasa la saba? Au ametumwa kuwakilisha Prof Muhongo? Au ni njia ya kumpitisha Tulia Akson?
 
Tunahitaji Spika na sio Academician.
Sisi wabunge wa CCM hatutaki mtu wa kuja kutusumbua na ma-research yake. Akafanyie kazi huko maofisini, huku kwenye siasa za CCM hakumfai kabisa.

Sisi CCM tunajijua wenyewe. Wasomi wenye madegree mkija huku muwe tayari kuzitupa chooni hizo degree. Mkikomaa nazo hamfiki popote.
 
Ivi Kabudi ana degree ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…