TANZIA Profesa Handley Mafwenga, Mtanzania mwenye shahada 9 afariki dunia

TANZIA Profesa Handley Mafwenga, Mtanzania mwenye shahada 9 afariki dunia

Sawa mkuu,
Macho hayana nguvu hasa jicho la kulia naona kabisa limepunguza uwezo wa kuona....

Napo andika hii comment nipo mbele ya computer 💻

This week ntaenda fanya check up ya macho..
Kama carrots kwenu ni nyingi, kunywa juisi kila siku kama hamna tumia mawese mabichi au mbegu zake kwa eingi japo yanachangamoto zake kwa mtu ambae hajayazoea ila ni tiba.
 
Mafenga.jpg
Alitakiwa awe OSHO wa TANZANIA Osho alikuwa na maktaba yenye vitabu karibu 100000 na anadai alivisoma vyote. Baadae akaacha kuvisoma akawa anajibu maswali magumu na kazi zake zimehifadhiwa
Mwafongo alitakiwa awe na maktaba ya vitabu alivyoandika yeye mwenyewe, na ingekuwa hazina ya TAIFA .
Ningependa kujua je je aliacha vitabu vingapi, maandiko mangapi, alikuwa ana andika makala kwenye magazeti ambapo zinaweza kukusanywa kuwa kitabu ?
Familia yake wangeanzisha platform aither blog au wesite, You tube Channel waweke kazi zake za kitaaluma waziuze nk.
Mtandaoni kuna Youtube channel ya Michael Jackson na Bob marley japo wamekufa nasi tunaweza anzisha vitu kama hivyo kwa watu wetu wakubwa wakubwa kama Nyerere nk.
 
Kama carrots kwenu ni nyingi, kunywa juisi kila siku kama hamna tumia mawese mabichi au mbegu zake kwa eingi japo yanachangamoto zake kwa mtu ambae hajayazoea ila ni tiba.
Option ya carrot 🥕🥕🥕 naona itakua the best naanza Leo hii
 

Aliyekuwa Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu Daraja la Kwanza wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Profesa Handely Mwafwenga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Mwafwenga aliyekuwa na elimu ya digrii saba na shahada tatu za uzamivu (PhD) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo 19, 2023, wakati akipatiwa matibabu ya figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na familia yake kupitia kwa mdogo wake, Innocent Mwafwenga ameeleza kuwa Profesa Handely ambaye ni kaka yake alifariki majira ya saa saba usiku.

“Jana alikuwa amezidiwa ghafla na alipelekwa jengo la wagonjwa mahututi (ICU) na tulipoenda asubuhi ya leo tumemkuta ameshafariki,”amesema Innocent.

Innocent amesema Profesa Mwafwenga kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na tatizo hilo japo haikufahamika lakini baada ya kupima ikabainika kwamba anachangamoto ya figo.

“Mwanzoni alikuwa hajagundulika alikuwa anaumwa lakini tulikuwa hatujui kama ni figo lakini baadaye baada ya kupima ikagundulika na figo na alianza kudhohofika kwa kipindi kama cha mwaka mmoja hivi,”amesema.

Innocent amesema kwa kipindi cha nyuma muda mwingi alikuwa analalamika matatizo ya mgongo lakini baada ya kuona tatizo hilo linazidi ndipo alipenda hospitali na kubainika anatatizo hilo.

Hata hivyo, Wizara ya Fedha kupitia kwa Katibu Mkuu, Dk Natu Mwamba imetoa pole kwa watumishi, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kwa msiba huo.

Innocent amebainisha kuwa Profesa Mwafwenga aliyewai kuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameacha familia ya watu wa tano, mke na watoto wa nne.

“Watoto wake wote ni wakubwa kuna ambao wameshamaliza elimu ngazi ya vyuo na kuna baadhi wapo kazini,”amesema.

Kuhusu msiba, amesema unafanyika nyumbani kwake Mabwepande na keshokutwa wataanza safari kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya kwa maziko.

Jina la ukoo kwa usahihi ni Mafwenga, si Mwafwenga! Poleni sana kwa wafiwa wote.
 
Digrii nyingi Hazinaga urithi kwa watoto labda kama ameacha hazina ya kitaaluma. Ni bora uwekeze kwenye ardhi au viwanda watoto wako watarithi kuliko PhD nyingii za kutishia watu. PhD zote hizo bado ni muajiriwa kashindwa kuanzisha hata kampuni la kuuza utalaam(consultant co).

Mwafwenga ana ombwe ktk modern skill set hasa ktk kuuza ujuzi, ana elimu very traditional ambayo inabidi uajiriwe tu vinginevyo asingekuwa muajiriwa angekuwa ni mmiliki wa makampuni na mwajiri.
We have to learn to adapt modern skill set.
Tuachane na digrii za sifa.
Shaban Robert hakuwa hata na digrii moja lakini ni maarufu kuliko wenye madigrii mengi wa wakati wake.
Ushauri mzuri sana, ila jina la ukoo kwa usahihi ni Mafwenga si Mwafwenga!
 
Back
Top Bottom