Profesa Ibrahim Lipumba: Mawaziri wapewe mkataba wa mwaka mmoja, atakayeshindwa kufanya kazi atumbuliwe

Profesa Ibrahim Lipumba: Mawaziri wapewe mkataba wa mwaka mmoja, atakayeshindwa kufanya kazi atumbuliwe

Utumishi wa umma kwa ujumla wake ulipaswa kwenda kwa mfumo huu wa mikataba.

Kuna watu toka waajiriwe hawajawahi kuwa na tija yoyote.
 
Arudi CCM ,mambo ya CCM vipi atawapangia yeye,ukisikia wanaojitisha ndio hawa,yeye mbona hajakaa hapo kwenye uenyekiti kwa Mkataba ?
 
Mzee huyu kazeeka kwa kasi sana , yaani kasahau kwamba hata yeye kaendelea kukomaa huko CUF miaka yote na hataki kutoka leo hii anamfundisha mama kazi loooooh
 
Na Viongozi wa Vyama vya Siasa nao wapewe mikataba tuone kama yeye atatoboa
 
Mzee ni mpuuzi kabisa huyu na uprofesa wake anaudhalilisha sana, japo alichoongea ni cha muhim na kinafaa kufanyika ili kuboresha utendaji wa hawa waajiriwa kina mwigulu.
 
Mzee ni mpuuzi kabisa hyu na uprofesa wake anaudhalilisha sana, japo alichoongea ni cha muhim na kinafaa kufanyika ili kuboresha utendaji wa hawa waajiriwa kina mwigulu.
Ahaaa.
 
Mwenyekiti wa Cuf na bingwa wa masuala ya uchumi duniani ameshauri kuwa Rais wa JMT samia na makamu wake Dk Mpango wawe wanawapa mkataba wa mwaka mmoja mwaziri ili anayeshindwa kazi atumbuliwe kihalali.View attachment 1743907
Huyo professa aidha hajui utendaji serikalini ulivyo au anatafuta kick. Iko hivi:

Kila wizara ina document inaitwa strategic plan ambapo huonyesha malengo mapana (objectives ) na targets (malengo mahsusi) ambayo hupangwa kukamilika ndani ya miaka mitatu au mitano. Kisha kila mwaka hupangwa activities zitakazotekelezwa kulingana na bajeti ambayio wizara hupewa hii huitwa annual mtf budget.

Bajeti hiyo hupitiwa na kamati ya bunge na hatimaye huidhinishwa na bunge. Wizara huandaa action plan kuonyesha nini kitafanyika mwezi gani.

Kila baada ya miezi mitatu ripoti ya utekelezaji huandikwa na wizara na kuwasilishwa wizara ya fedha na ofisi ya waziri mkuu. Hivyo waziri anakuwa amepinwa tayari kuwa amefanya nini kila miezi mitatu. Mwisho wa mwaka huandikwa ripoti ya mwaka ya utekelezaji .

Hivyo hakuna haja kumsainisha tena mkataba waziri.
 
Mwenyekiti wa Cuf na bingwa wa masuala ya uchumi duniani ameshauri kuwa Rais wa JMT samia na makamu wake Dk Mpango wawe wanawapa mkataba wa mwaka mmoja mwaziri ili anayeshindwa kazi atumbuliwe kihalali.View attachment 1743907
Huu mfumo dume balaa. Makamu wa Rais anahusika vipi hapa? Anayeteua mawaziri ni Rais peke yake. Hivi wakati Mwendazake yuko hai mngethubutu kusema Rais Magufuli na Mh. Samia Hassan wafanye hili na lile? Tumpe Rais heshima yake kwa kutambua kuwa Dr. Mpango ni Makamu wa Rais na sio Rais Mwenza.

Amandla.
 
Huyo professa aidha hajui utendaji serikalini ulivyo au anatafuta kick. Iko hivi:
Kila wizara ina document inaitwa strategic plan ambapo huonyesha malengo mapana (objectives ) na targets (malengo mahsusi) ambayo hupangwa kukamilika ndani ya miaka mitatu au mitano...
Sasa mbona hatuoni wakiwajibishwa kwa utendaji mbovu kama ulivyoainisha? Maana kama ni poor perfomance wengi tu ni wauza chai tu kwenye luninga
 
Wazo zuri ila linatakiwa kuboresha na kuongezewa vipengere liendane na katiba na sheria .
 
Sasa mbona hatuoni wakiwajibishwa kwa utendaji mbovu kama ulivyoainisha? Maana kama ni poor perfomance wengi tu ni wauza chai tu kwenye luninga
Nimeeleza kuwa kila mwaka wizara inapewa pesa hivyo wizara inafanya kazi kulingana na bajeti iliyotolewa. Unaweza kukuta wizara inahitaji biliini 10 kufanya kazi fulani lakini inapewa bilioni moja au milioni mia 500, hivyo inabidi watekeleze sehemu ndogo tu ya kinachitakiwa kufanywa. Yaani inabidi wizara islash baadhi ya activities ambazo zingewezesha target fulani kukumilika.
 
Back
Top Bottom