sijaona tanzia ya ajari mkuu kuwa mkweli mambo si mambo alafu inapiga wanazuoni sana sijajua shida nini
Wiki hii haijawa njema kwangu. Nimempoteza mjomba wangu, rafiki yangu akampoteza mama na baba yake kwa kufuatana. Kabla sijakaa sawa nikapata taarifa za msiba wa kaka Muksin Mambo, kisha nikapata taarifa za msiba wa dada Tuli Nasa.Kabla sijahamaki tukampoteza mzee Arcado Ntagazwa (Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Chadema).
Leo najulishwa rafiki yangu Wenseslaus O W Jnr amempoteza baba yake mzazi. Kabla machozi hayajakauka kaka yangu na mwanafamilia mwenzangu wa GIFTED HEART Anthony Mtaka akampoteza mama yake mzazi. Wakati tukijiandaa kwenda kumpumzisha mama yetu huko Musoma, napata taarifa kuwa kaka John W. Jacob amefariki dunia kwa ajali ya gari.
Wakili msomi, John Jacob alikua mwanafamilia active wa GIFTED HEART FAMILY. Hajawahi kuacha kushiriki tukio lolote la kurudisha tabasamu kwa watanzania. Maisha yake yalikua sadaka kwa jamii hasa watu wenye mahitaji. Alijitoa sana kusaidia watu kwa namna mbalimbali. Rafiki yetu mmoja alipopata kesi ya uhujumu uchumi alijitolea kumsaidia bila malipo.
Mwaka jana baadhi ya wanafamilia wa GIFTED HEART tulimtembelea ofisini kwake Manyoni, Singida. Pamoja na mambo mengine tulimpongeza kwa namna alivyokua akijitoa kwa jamii. Kwa muda wote tuliokaa Manyoni alitukirimu kwa viwango vya juu sana.Alikua rafiki mwema sana na asiye na makuu. Mambo makubwa mawili aliyoyapenda sana ni kusoma vitabu na kusaidia wenye mahitaji. Tulishirikiana nae kwa mambo mengi ya kijamii na kuweka mipango mingi ya maendeleo. Bahati mbaya kifo kimekatisha mipango hiyo.
Aliposikia taarifa za msiba wa mama Mtaka aliniuliza kama familia ya GIFTED HEART itatoa uwakilishi wa kwenda msibani Musoma. Nikamwambia Ndio. Akasema yeye hataweza kushiriki lakini akatuma mchango wake wa rambirambi nimsaidie kuwakilisha.Muda mfupi baada ya kutuma rambirambi yake mauti ikammeza kwa ajali. Laiti kama angejua yaliyo mbele yake, pengine angeahirisha safari yake. Eeh Mwenyezi Mungu utusaidie kuzihesabu siku zetu.
Natoa pole za dhati kwa familia yake (mke, watoto, na ndugu) pamoja na familia ya Gifted Heart. Kwaheri kaka yangu John, kwaheri wakili msomi. Tutaonana tena Paradiso. Eeh Mungu tunakushukuru kwa maisha ya ndugu yetu John. Kwa miaka michache ya uhai uliyomjalia aliweka alama kwenye maisha ya wengi.