Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Waziri wa foreign affairs Prof Kabudi na watendaji wakuu wa wizara yake wamekutana na makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar maalim Seif na kukubaliana kuchapa kazi kwa pamoja.
Maalim Seif amesema uchaguzi umekwisha aliyepata kapata na aliyekosa amekosa cha muhimu ni watanzania kuungana pamoja katika kujiletea maendeleo.
Naye Prof Kabudi ameihakikishia serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kuipa kila aina ya ushirikiano itakaohitaji ikiwemo kuutangaza utalii wa Zanzibar kimataifa.
Source ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
Nimecheka kwa nguvu, sasa nimeamini ukhanithi sasa basi.