Profesa Kabudi amtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, wasema uchaguzi umekwisha sasa kazi tu!

Profesa Kabudi amtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, wasema uchaguzi umekwisha sasa kazi tu!

Waziri wa foreign affairs Prof Kabudi na watendaji wakuu wa wizara yake wamekutana na makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar maalim Seif na kukubaliana kuchapa kazi kwa pamoja.

Maalim Seif amesema uchaguzi umekwisha aliyepata kapata na aliyekosa amekosa cha muhimu ni watanzania kuungana pamoja katika kujiletea maendeleo.

Naye Prof Kabudi ameihakikishia serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kuipa kila aina ya ushirikiano itakaohitaji ikiwemo kuutangaza utalii wa Zanzibar kimataifa.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

Nimecheka kwa nguvu, sasa nimeamini ukhanithi sasa basi.
 
Seif bwana! Hivi Jussa amepona? Anaendeleaje? Kwa ujinga wangu nafasi hiyo hukustahili hata kidogo, na maneno unayotoa hayatokani na utashi wako, sasa ona unapata shida yakupasa utoe kauli za kujipendekeza, Mh Mwinyi anahekima sana alikuomba muunde serikali, ungemtafutia kijana ashughulike nae nawe ungekuwa unashauri na kuangalia mwelekeo!
 
Saa hizi hakuna wa kuwapinga hata matembezi ni habari! 5 tena
 
Damu iliyomwagika pale Pemba imeshasaulika na maisha yanaendelea manyumbu sisi
 
Hongera Prof. Kabudi na Makamu wa Kwanza Wa Rais Maalim Seif kwa hatua hiyo ili tuimarishe uchumi wetu.
Yaani muavunje Vijana miguu wakati wa uchaguzi halafu huyo Mzee mliyemrubuni ndiyo ataweza kuujenga na kuimarisha uchumi?? Hilo pia siyo ajabu kwenye awamu hii kwani kuna Kiongozi Mkubwa aliwahi kuomba msaada Zimbabwe.
 
Muislam gani aliyekula nguruwe? Nafikiri hamkujiandaa kujua deals wanasiasa wanazofanya huwa zinafanana
Alisema hataki UKHANITHI, leo yuko kwenye UKHANITHI, si kula nguruwe huko!
 
Waziri wa foreign affairs Prof Kabudi na watendaji wakuu wa wizara yake wamekutana na makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar maalim Seif na kukubaliana kuchapa kazi kwa pamoja.

Maalim Seif amesema uchaguzi umekwisha aliyepata kapata na aliyekosa amekosa cha muhimu ni watanzania kuungana pamoja katika kujiletea maendeleo.

Naye Prof Kabudi ameihakikishia Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kuipa kila aina ya ushirikiano itakaohitaji ikiwemo kuutangaza utalii wa Zanzibar kimataifa.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom