Profesa Kabudi: Tanzania inatamani sana Chato ifanane na majiji makubwa ya China ambayo awali yalikuwa ni vijiji vya wavuvi!

Profesa Kabudi: Tanzania inatamani sana Chato ifanane na majiji makubwa ya China ambayo awali yalikuwa ni vijiji vya wavuvi!

Kosa lipi hapo limetendwa!weka data,tutumie data kusema Kuna kosa lipi hapo,je miradi ingejengwa mtambaswala Lindi kungekuwa na kosa?
Au je ingejengwa Kyelwa Kagera je?au ijengwe Manyara Kiteto!?wapi ikijengwa kila mwananchi ataridhika na kusema hapa Hili lina maslahi kwa nchi nzima,
Wapo watu wanasema SGR,Madege ya ATCL hata bwawa la Nyerere la kufua umeme havina tija,ni matumizi mabaya ya pesa,inategemea unaangalia kutokea wapi.
Serikali hii inamatumizi mabaya ya pesa,na upendeleo,ukabila,sikatai.
Swali je,ajenge wapi ambapo wananchi hawatapiga kelele,afanye mradi upi ambao kila mbongo ataridhika?Hapa Ni Nyerere tu aliweza,
Viongozi wote waliotawala nchi hii kwa namna yoyote ile walipendelea maeneo wanayotoka,na hili halitaisha leo,hii ni dalili ya tatizo/Ugonjwa,tusishambulie dalili,tupambane na Ugonjwa,
Hata huko chato kila mtu anaweza kwenda kuwekeza
Hamna rais wa awamu yoyote aliyependelea kwao kama huyu wa leo usitudanganye,nyie baadaye akishatoka kwenye urais mnaanza magu alikuwa mwizi,fisadai,alipendelea kwao kwa sababu uzalendo wenu ni sifuri mnapenda kumpamba mtu sifa za kila aina akiwa kwenye mamlaka akishatoka anakuwa takataka,poor minded system.
 
Wachina waliijenga na wanaendelea kuijenga nchi yao...Na sisi tujenge ya kwetu

Yaani kati ya vitu huwa tunajidanganya ni kudhani Wachina wana moyo mweupe wa kutusaidia...

Sisi "feizhou ren" huwa wanatuona takataka za mwisho
 
Tayari ile pocket money ya mil.358 imeelekezwa huko, tunasubiri hii tuliyoomba kusamehewa madeni tuielekeze nayo kujenga jiji la uvuvi la chato, mbona raha jamaniii.....
 
Profesa Kabudi amemwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwamba anashukuru kwa ziara aliyoifanya Mwaloni leo asubuhi na Tanzania inatamani Chato ije kuwa kama miji mikubwa ya China ambayo awali ilikuwa ni vijiji vya wavuvi kama ilivyo chato.

Profesa Kabudi amesema kwa mahusiano mema ya Tanzania na China hilo linawezekana kabisa.

Profesa Kabudi na waziri Wang Yi walikuwa wanaongea na waandishi wa habari leo hii Chato mkoani Geita.

Chanzo: Upendo tv

Maendeleo hayana vyama!
Njozi kama hizo alikuwa nazo Rais Mobutu Sese Seko. Lakini zilizimika zote mara tu alipotoka madarakani. Washauri wa kariku wa Mkulu epukeni kujipendekeza sana kwa kumpa ushauri uliokuwa fyongo.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Profesa Kabudi amemwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwamba anashukuru kwa ziara aliyoifanya Mwaloni leo asubuhi na Tanzania inatamani Chato ije kuwa kama miji mikubwa ya China ambayo awali ilikuwa ni vijiji vya wavuvi kama ilivyo chato.

Profesa Kabudi amesema kwa mahusiano mema ya Tanzania na China hilo linawezekana kabisa.

Profesa Kabudi na waziri Wang Yi walikuwa wanaongea na waandishi wa habari leo hii Chato mkoani Geita.

Chanzo: Upendo tv

Maendeleo hayana vyama!
Hilo jiji lingepewa jina la Magu,hivi Tanzania anayoisemea kabudi ni ipi?Chato kuwa jiji kutamnufaisha Mtanzania mnyonge?
 
Tanzania ni jiwe.

Anatamani chato iwe kama majiji makubwa ya china ila ndo hivyo hakuna namna anakuna panapokunika.

Anajitutumua kuipendelea chato kadri awezavyo.

Nna uhakika bandari ya Bagamoyo ingekua chato angekubali ijengwe haraka sana.
Kikwete alitaka kujenga jiwe akasimamisha,kama ingekuwa Chato naamini hata kupitisha mizigo Dar kungepigwa marufuku,ingeamuliwa ipitie Chato
 
Ww jamaa una chuki sana na kaskazini,hujaona miji mingine kama Mwanza,Mbeya au hata Dodoma? Unajikomba sana punguza usoro bas
Mbona Arusha na Moshi mnapambana muifikie Carfonia?!

Acheni wivu wa kishamba bhana!
 
Back
Top Bottom