Profesa Kabudi: Tanzania kupokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje

Huo urafiki wa nchi yetu na china wa miaka 55 sioni Kama uko na tija kwa upande wetu maana wao ndio wenye kufaidika nao.
Sisi tunaendelea kua nyuma yao wao wanaendea tena mwa mgongo wetu.

Kama huo urafiki ungalikua ni urafiki usio wa kupakana mafuta kwa mgongo chupu leo tungekua tunaongea lugha nyingine.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Ni swala la muda tu mkuu usemayo kutimia.
 
..Tangu mwaka 1991 mawaziri wa mambo ya nje wa China wamekuwa na utamaduni / utaratibu wa kutembelea nchi za Kiafrika kila mwanzoni mwa mwaka.

..kwa mwaka 2021 waziri wa mambo ya nje wa China atatembelea Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Botswana, Tanzania, na visiwa vya Shelisheli.
 

Tujue tu kwamba vitu vyote ambavyo Nyerere aliiga kutoka China havikifanikiwa na azimio la Arusha lilikufa. Hata huko Chima ilibidi waingie kwenye ubepari kinamna. Mkisema miaka 55 sio sawa maana China ile sio China hii wakati ule kulikuwa na vita baridi
 
Pia mwaka 2017 ziara kama hii ilifanywa Afrika na Mh. Wang Yi kuzuru Afrika

9 Jan 2017

Waziri wa mambo ya nje wa china Wang Yi amewasilia nchini kwa ziara ya kikazi.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Wang Yi amewasili nchini na kupokewa na mwenyeji wake waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Balozi Agustine Mahiga ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wataendeleza mazungumzo baada ya China kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za Afrika itakayohamishia baadhi ya viwanda / outsourcing.

5 Jan 2017

Chinese Foreign Minister Wang Yi to visit five African countries​

Chinese Foreign Minister Wang Yi is set to make official visits to Madagascar, Zambia, Tanzania, the Republic of Congo and Nigeria this month. Foreign Ministry spokesperson Geng Shuang says for the past two decades, Africa has been the first stop for the top diplomat's official visits abroad. Geng says the practice shows that Beijing regards its relations with developing countries as the foundation of its diplomacy.
Source : CGTN Africa
 
December 30, 2020

Waziri Kabudi akieleza ugeni mzito kutoka China utakaotua Tanzania Jan 7 , 2021

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi amefanya mkutano na vyombo vya Habari leo, jijini Dar es Salaam kuelezea ziara ya siku mbili itakayofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi hapa nchini Jan 7 hadi 8, mwaka 2021
 
Habari ingekua.madikteta wa uchina kukutana na Madikteta wa Tanzania hivi karibuni.
 
Jicho la tatu linaniambia haya:

Ile simu imeanza kufanyiwa kazi.

SGR hiyo kwa wachina

Bandari ya Bagamoyo nayo iko mbioni, na kadhalika.

JK atakuwa anechaka tu huko aliko na kujisemea kiko wapi sasa!

Baada ya Mungu, ni muda- imani yangu.
IGP atakuwa mchina kama Zambia
 
Hey, hivi wataenda na kwa tundulissu Ubalozini? Alisema sisi ni skunk hata Machina hawatutaki. Kama hayupo tutumie utaratibu ule ule wa majuzijuzi na mabloger wa EU
 
Sielewi unazungumzia kitu gani hapa.

Kwa nini unadhani Mwalimu Nyerere aliiga China hivyo vitu. Wewe unadhani Mwalimu Nyerere hakuwa na akili hata kumshinda Jomo? Bure kabisa wewe.
 
Wewe una lolote? Unafurahia wachina kuja Tanzania?Mugabe waliokuwa wanampa kiburi ni hao hao mwisho wakammalizia tembo nchini kwake,very stupid.
Leo hii nilikuwa nazungumza na Mzimbabwe mmoja mwanauchumi, akasema, 'the day you see many chinese in a poor country, that country is finished. In Zimbabwe, sanctions paralyzed the nation, Chinese killed and buried it'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…