Profesa Kabudi: Tanzania kupokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje

 
Jicho la tatu linaniambia haya:

Ile simu imeanza kufanyiwa kazi.

SGR hiyo kwa wachina

Bandari ya Bagamoyo nayo iko mbioni, na kadhalika.

JK atakuwa anechaka tu huko aliko na kujisemea kiko wapi sasa!

Baada ya Mungu, ni muda- imani yangu.
We unyamaze tu hakuna lolote la maana, ni sawa na mpiga ramli tu. Waziri wa mambo ya nje mwenyewe anakuja rasmi kumwona mwanaume wa shoka nyumbani kwake Chato, wewe unabwabwaja tu. Tanzania is better now under the leadership of JPM.

FYI Xi Jinping anatembelea Tanzania wakati wowote baada ya ziara hiyo. Ni maandalizi tu kwa sababu China na Tanzania ni dam dam, whether you like it or not. China hata siku moja hawawezi kuwasahau Watanzania hasa walivyowapigania kwenye UN enzi za baba wa taifa JKN.
 
Nchi ambayo ina import cover ya miezi sita na ushee unafananisha na waliokuwa wanauza matango? JPM ameweza kuweka mambo vizuri, kila mnavyofikiri atakwama yeye ndio anapasua anga. Mwacheni Mwanaume moja wa shoka ambaye anatekeleza. Wale malofa wenu walifanya nini zaidi ya kuwatajirisha nyinyi na vibeberu vyenu na kututukana JF?
 
A free advice.
Badala ya kwenda na kurudi na hawa Wachina, Tanzania isipange kupata tumisaada-saada twa dola milioni 50, 100, 300, 5000.... Ipange karata zake iingie kichwa kichwa na Wachina katika 'strategic partnership'. Kila miaka miatano China iipatie TZ bilioni 10 $ kwa muda wa miaka 50 ijayo. Tanzania ianze kulipa baada ya miaka 20 kwa faida ya 2%
Wachina, wakielezewa vizuri, watakubali, maana wanatafuta mahali penye Amani na Rafiki pa kuhifadhi ma trilioni yao ya dola ambayo sasa yanatishiwa 'kutaifishwa' na Marekani inayofilisika. Tanzania imeisaidia sana China, bila ya faida yeyote ya kueleweka. China iko tayari kuingia na Iran mkataba kama huo, sembuse TZ? Halafu tuna Wachina wengi waliopo serikalini wa kututetea. Chukua kwanza mfano wa balozi aliyepita Dr. Lu Youqing.
Huku kukatiwa vijidola hamsini kila mara hakutatufanya tuendelee. Tunahitaji 'a huge infusion of capital' ku revamp kabisa elimu yetu na agriculture, kabla hatujaendelea. Hii maneno ya "Uchumi wa Kati" tulionao ni 'smokescreen' tu. Mwaka huu huu tutarudi kuwa uchumi maskini. Uchumi wa kati haumaanishi tumeshafika basi tutabaki hivyo hivyo. Kwanza uchumi wa kati wenyewe ni "Kati ya chini" siyo "Kati ya juu" kama Kenya. Ila hawawatangazii raia hivyo, wanawaacha waimbe tu!
Alas! Hatuna 'strategic thinkers' katika tabaka la viongozi wetu. Hatuna hata 'long-term mapping' ya maendeleo yetu. Twategemea matamko ya rais tu kuwa mwongozo! Chukua mfano kauli mbiyu ya 'Uchumi wa viwanda' Inasemwa tu. Hakuna aliyeuliza viwanda gani? Wapi watatokea wajenzi Watanzania wa viwanda hivyo? Tuna mainjinia, ma project managers, ma machine operators, ma programme builders........wa kutosha? Tunataka kiasi gani cha hao watoke kila mwaka katika Vyuo vyetu vikuu?
Hii siyo lele mama! Walioendelea walipanga!
 
Hivi kwanini Kabundi ooops sorry Kabudi anapenda sana kumnukuu Nyerere kila mara lakini matendo tofauti? Huyu nae si kaambiwa hafai kugombea urais umri umemtupa mkono. Kuna ndege ana macho km kabudi yule ni Bundi.
 
Kwann mnawachukia Wachina kuwa marafiki wetu,kwani sio watu kwanza Wachina hawana Historia ya kikoloni hawajawahi kumdhalilisha Mwafrika Kama ilivyo Wazungu ama Mabeberu
 
Kasome habari ya money laundering ya benki ya China CCB .......
 
Wale mnaotegemea vikwazo vya Tundu lissu hii si habari njema kwenu!
 
Mbona wachangiaji mko pesmistic sana.

Mbona hamchangii kua wachina sasa wameona concern yetu na wameamua kuja ku renegotiate?!

Mbona hamchangii kua sasa china wanatuheshimu na sasa wamekuja kusign mikataba ya win --win.

Hakianani kazi ipo kwa kizazi hiki kilichokosa uzalendo.
 
Tuombe Mungu kwenye hayo majadiliano ya mikataba, wale waliohusika na majadiliano kuhusu makinikia wasihusishwe ama sivyo tutaiashia kupiga bao tena kama walivyotubadilishia kutojenga SMELTER nchini!!!
Washauri wenyewe ndiyo hao hao maana ndiyo walio tayari kukubali kuandaliwa nini waseme
 
Ujio wa huyu waziri wa mambo ya nje na ile simu ya Raisi wao kwa JPM

Then ukiunganisha kushikiliwa kwa maafisa waandamizi wa Bank yao ya CCB kwa kesi za utakatishaji fedha

Unaweza ona huu ujio sio wa maana yoyote zaidi ya kuombewa waachiwe then tupewe misaada.

Kama hukusikia utapeli wa wachina mpaka BOT ikafunga CCB Soma hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…