Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

Profesa Kabudi: Trilioni 360 za makinikia haikuwa kodi sahihi, Nilikosea kutumia neno “Jalala”

tuwekee video ya maneno haya mimi sina imani na hayo maelezo ya gazeti moja.
Amini ndugu, maana angelikuwa amelishwa maneno hayo angelikuwa amekwisha kanusha au kwenda mahakamani, huyu ni mwanasheria ujue.
 
Kauli hii ya Profesa Kabudi inadhihirisha kuwa Lissu alikuwa sahihi Sana kwa sababu hata kama ni mbinu za kutaka mjadala, kwa wasomi kama maprofesa kutumia mbinu ya uongo "ulio dhahiri" kiasi hiki ulikuwa ni upungufu wa weledi.

Labda tuwasikie Wataalam wa daplomasia ya uchumi waje watufafanulie mbinu hii ya "Uongo mkubwa wa dhahiri" kama Lissu alivyokuwa "Profesorial Rubbish".

======


  • Asema zilikuwa mbinu za majadiliano, ataja tishio la Acacia
  • Afafanua suala hilo limekwisha, atamtafuta mwigulu amweleze
  • Atamba uamzi ule umeleta heshima, faida kubwa kwa nchi
  • Asema alikosea kutumia neno jalala, asisitiza kibiblia ni sahihi.

Nukuu za Prof. Palamagamba Kabudi kwenye gazeti la leo la Jamhuri, Oktoba 4, 2022


=============


Mpatanishi Mkuu wa Scrikali (Chief Government Negotiator) Profesa Palamagamba Kabudi amesema Dola Bilioni 190 za kimarekani sawa na Tsh Trilioni 360 walizotakiwa kulipa kampuni ya Acacia, Julai 2017 kama kodi, malimbikizo na faini ya ukwepaji kodi, hakikuwa kiwango sahihi

Kabudi, aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mpatanishi Mkuu wa Serikali baada ya kutenguliwa uwaziri wa Katiba na Sheria, Januari, 2022 ameliambia Gazeti la JAMHURI mwishoni mwa wiki kuwa serikali ilifahamu tangu mwanzo kuwa kiwango hicho cha Dola bilioni 190 ambazo wakati huo zilikuwa sawa na Sh trilioni 360 kilikuwa hakilipiki.

"Jamani mtu yeyote anayejua, ile haikuwa kodi halali, ilikuwa ni kodi inayobishaniwa. Kwani watu wangapi mmetoa "assessment' (makadirio) ya kodi halafu mnakaa chini? Sasa nikasema siku nyingine nikipata nafasi na nikipata ruhusa, nita-share na wewe, na siyo siri, kwa sababu hata sasa wamekwishalipa ile installment (mkupuo) ya pili ya zile milioni 300.

"Lakini kuna faida nyingine nyingi ambazo tuliingia nazo kwenye mkataba... na ule mkataba sikusaini mimi, ulisainiwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, mimi nilichokuwa nimekisaini kilikuwa kinaitwa Agreement of Undertaking (Makubaliano ya Utekelezaji), lakini yote, ningependa siku moja nikupe details (taarifa) zote kwa sababu ule mkataba sivo siri. Mimi nasoma JAMHURI kila siku," amesema.

Amesema kati ya mambo ambayo nchi katika Kiswahili ni uandishi wa kutumia lugha ya Kiswahili nchini, ila utaalamu huo umesalia katika JAMHURI.

"Unajua bahati mbaya nilikuwa nasema hata leo, umepoteza ladha ya uandishi wa Kiswahili, sasa miongoni mwa watu ninaopenda kusoma ni safu ya SITANII [unayoandika Balile], sasa mtu ambaye hajajua tamathali atasema, 'huyu anaandika nini?”

"Lakini mimi ninachokipenda ni ile aina ya lugha, kwa hiyo nashukuru na nikija Dar es Salaam nitakutafuta ili tukamilishane mawazo katika mambo yatakayotusaidia kujenga.

Lakini mambo mengine mimi hapana, kwa sababu ni vizuri kuona watu wanavyotafsirivitu. "Namtafuta Mwigulu (Waziri wa Fedha) nimwambie kuwa ile ilikuwa ni kodi inayobishaniwa. Na wao pia walitupeleka
kwenye ICSD (Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro) na wenzetu wakawa wanasema mtashitakiwa, mtafilisiwa.

"Unajua hizo trilioni zilipigwa baada ya wao kuwa wamepeleka mashitaka makubwa ICSD ya kudai close to two billion US dollars (karibu dola bilioni 2 za Marekani), sasa vitu vingine huwezi kuvieleza kwa sababu hizo ni mbinu za negotiations (upatanishi).

“Ukivieleza utavuruga, lakini ulichosema ni kweli... wewe hiyo kodi utaitoa wapi? Inazidi GDP za nchi zote, halafu nikasema huyu bwana kweli hatanii," amesema Kabudi.

Amesema tangu mwanzo walijua kuwa kiasi hiki hakilipiki ila walitumia kiwango hicho kama mbinu za majadiliano na upatanishi.

Ameliambia JAMHURI kuwa kwa vyovyote iwavyo, katika mgogoro kati ya Acacia na serikali, Tanzania iliibuka na ushindi na kwa masilahi mapana ya biashara hata Acacia walipata ushindi kwa kufanya biashara inayokubalika kwa pande zote mbili.

"Mimi nasoma JAMHURI kila ikitoka, sasa huko nyuma uliandika kitu nikakaa kimya, lakini cha jana nimekisomaa, nikatafakari, nikasema hebu nirudi kwa Balile niongee naye," amesema Kabudi.

Amesema kabla ya mgogoro huu, Tanzania haikuwahi kupata kitita cha Dola milioni 300 sawa na Sh bilioni 700, ambapo Acacia mwaka 2019 walitoa Dola milioni 100 kwa mpigo na wameendelea kutoa gawio mwaka hadi mwaka bila kuacha.

Huku akisisitiza kuwa hata mwaka huu serikali imepokea fedha nzuri tu kutoka kwenye madini, akaongeza kuwa nchi imepata hisa asilimia 16, inapata mgawo wa asilimia 50 ya faida inayopata Kampuni ya Twiga ambayo ni tanzu, inayomilikiwa kwa ubia kati ya Tanzania (16%) na Barrick (84%), uwazi umeongezeka kila kinachofanywa kinaonekana.

Ameongeza kuwa kuna faida kubwa na Tanzania imekuwa mfano kwa mataifa mengi ya Afrika ambayo sasa yanaiga.

Kabudi amesisitiza kuwa mgogoro wa Acacia/Barrick ulikwisha Oktoba, 2019, hivyo waliruhusiwa kusafirisha makinikia yaliyokuwa yamezuiwa bandarini, wakaanza kulipa kodi kwa mujibu wa makubaliano na deni la Dola bilioni 190 likafutwa katika vitabu vya serikali.

Kati ya fedha hizo, Dola bilioni 40 zilitajwa kuwa ni kodi iliyokwepwa na Dola bilioni 150 zilitajwa kuwa ni faini, malimbikizo na riba ya kukwepa kodi tangu mwaka 2000.

Katika kinachoonekana kuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, ana hoja mahususi aliyoishikilia, Novemba 5, 2021 ikiwa ni miezi sita baada ya kifo cha Rais Dk. John Magufuli, alihoji zilipo Sh trilioni 360 ambazo Serikali ya Awamu ya Tano iliwadai Acacia na kupeleka shauri kwenye Baraza la Kodi....
Akiri pia kwamba alikosea sana sana kumuita jiwe Mungu
 
I'll prof kwanin unakuwa kiazi mbela ya magu ,mbna magu mwepesi tu
IMG_20221006_221309.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tangu gazeti la JAMHURI litoe kinachoitwa Kauli ya Profesa Kabudi kuhusiana na suala la Trilioni 360 kuwa lilishamalizika kuna kila dalili za kuwepo sintofahamu na upotoshaji mkubwa kuhusiana na kauli hiyo.

Watanzania wengi wamepaza sauti kutaka kuletewa uthibitisho wa kauli hiyo ama video au sauti inayomuoyesha Kabudi akisema maneno hayo lakini badala yake tunaona vikundi vya watu mbalimbali vikijadili kinachoitwa kauli ya kaudi.

jambo la kushagaza video za lisu, mpina na mwigulu zinaletwa tunawasikia wamesema nini kuhusiana na suala hilo, kwanini balile ameshindwa kuleta clip inayomuonyesha kabudi akisema hayo?
 
Sitofahamu imeleta simanzi baada ya kukili kwamba matrioni ya Dola yaliyokuwa anadaiwa na Serikali dhidi ya acacia ni batili.

Profesa ulimdanganya marehemu Rais Magufuri na watanzania kuhusu Dili la makinikia inabidi utoae ufafanuzi wa kina au ushitakiwe.
 
Sitofahamu imeleta simanzi baada ya kukili kwamba matrioni ya Dola yaliyokuwa anadaiwa na Serikali dhidi ya acacia ni batili.

Profesa ulimdanganya marehemu Rais Magufuri na watanzania kuhusu Dili la makinikia inabidi utoae ufafanuzi wa kina au ushitakiwe.
JamiiForums-71234489.jpg
 
Anaendelea kuwa mmoja wa mawaziri wakuu bora katika nchi hii.
 
  • CCM...Chama kile kile
  • CCM...Watu wale wale
  • CCM...Ujinga ule ule
  • CCM...Unafiki ule ule
CCM mbele kwa mbelee...kazi iendelee!
 
  • CCM...Chama kile kile
  • CCM...Watu wale wale
  • CCM...Ujinga ule ule
  • CCM...Unafiki ule ule
CCM mbele kwa mbelee...kazi iendelee!
Ccm wanaakili na mipango zaidi ya CHADEMA chama cha kikabila,Kidini, Kiusharati na maa LGBT
 
Back
Top Bottom