#COVID19 Profesa Makubi: Serikali imeunda Kamati ya wataalamu kufuatilia masuala ya Chanjo ya Corona

#COVID19 Profesa Makubi: Serikali imeunda Kamati ya wataalamu kufuatilia masuala ya Chanjo ya Corona

Sayansi bado inaongoza dhidi ya waropokaji na washirikina!

Tutaelewana tu kidogo kidogo japokua wapendwa wetu wanaendelea kuangamia kwa kukosa miongozo sahihi
 
Teh teh teh Mataga hamna tofauti na Kasuku,kila mlio mnaenda nao sambamba. Kazi mnayo awamu hii.
Nchi ya Denmark imesitisha utoaji wa Chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa muda wa wiki mbili ili kuchunguza ripoti za baadhi ya wagonjwa kupata tatizo la damu kuganda siku chache baada ya kupatiwa chanjo hiyo..

Waziri wa Afya nchini humo amesema wamechukua hatua hiyo ikiwa sehemu ya tahadhari ili kuchunguza endapo kuna madhara zaidi yaliyojitokeza tofauti na la damu kuganda.

Mamlaka ya Afya ya Denmark imesema uamuzi wa kusimamisha chanjo umekuja baada ya mwanamke wa miaka 60 nchini humo kupewa dozi ya AstraZeneca na kupoteza maisha.
 
Hapo ndo mtajua JPM aliona mbali...VIVA My President...Mungu akulinde uwe na afya njema
 
Naona baada ya jasusi Kagame kuchanjwa imeleta mwangwi Bongo
 
Mganga mkuu wa Serikali Prof Makubi amesema serikali imeunda tume maalumu ya wataalamu itakayofuatilia masuala ya chanjo ya Corona.

Prof Makubi amesema tume hiyo itafuatilia masuala ya msingi yahusuyo chanjo hizo kwa muda wote hadi pale serikali itakapojiridhisha kama itumie chanjo hizo ama la.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Tunaishukuru Serikali kwa busara hiyo.Maana waswahili wanasema"bila utafiti huna haki ya kuzungumza".
 
Utaalamu maana yake nini, hapo ndipo pa kuanzia. Utachunguzaje kitu ambacho wewe hukijui wala hauna utaalamu wa kukitengeneza.

Hizo ni siasa tu zilizotamalaki katika utawala huu. Hakuna uchunguzi hapo ni watu kwenda kula pesa tu ni kama tu ile tume ya akina Osoro.
 
Basi tutakupeleka wewe.
 
Hakuna siku serikali ilisema hatutaki chanjo, serikali ilisema hatutakuwa sehemu ya majaribio ya chanjo.

Hatua ya majaribio ilishapita na sasa watu wanachanjwa. Hii “hatuwezi kuwa majaribio” ni sababu ya kukataa chanjo! Read between the line, mkuu! Sio lazima sababu ya kukataa kitu iwe na mantiki au uhalali - inapaswa kusemwa tu. Ndio kama hivi. Kwali walipokataa barakoa si walisema zina vijidudu? Ulisikia kuwa wamefanya utafiti na kugundua hilo??
 
Tume imeundwa ikipitisha kuwa chanjo inafaa tutachanjwa boss. Si lazima kubishana na utawala kwenye kila jambo.
 
Naona sasa serikali ya wanyonge imeamua kusalimu amri kwa kuacha sayansi ichukue nafasi yake.
 
mbona ameruhusu kujifukiza hospitali ya Taifa
 
Huna akili.

Hata kabla ya corona kuna watu walikuwa na hawashauriwi kutumia baadhi ya dawa mfano zenye sulpher.
Ila maana yake sio kwamba hazifai
Wewe ndo huna Akili kama nchi wanakataza mpaka wafanyie uchunguzi na nimeweka source mimi na wewe nani hana akili? Sio kila kitu cha kushabikia
 
..inaweza ni maandalizi ya bwana mkubwa kupewa chanjo.

..kwamba kwa hali yake ya kiafya chanjo haiepukiki.
 
Back
Top Bottom