Profesa Mkenda aapa kutotoa vibali vya kuagiza sukari

Sisi wakulima kwa korosho ni msimu wa 3 mfululizo hatujui pembejeo dukani inauzwa Bei gani? Wakulima wa mounga na mahindi walau Sasa tuna uhakika na Bei ya mazao yetu. Ni muda huu mbaazi na ufuta vimevuta vijana wengi huku kusini mwa Tanzania kuliko wakati wa mkenda. Sasa tunachanganyikiwa tunaposoma hata.
Narudi, Bashe ni binadamu lazima awe na mapungufu, lakini si kwa picha hii munayojenga.
 
Nilimaanisha mpunga na sio kama ikivyoandikwa hapo
 
Mimi sijali sheria,nachosema ikiwa kila baada ya muda Fulani huficha sukari ili iadimike Bei zipande,Wacha viwanda vife
sheria inasema wakificha wapigwe faini ya milioni 500 muulize bashe amewapiga faini mara ngapi walioficha sukari?
 
Bashe mtoto wa mjini.

Mnahangaika bure.

Tuliwambia Katiba Mpya sasa mnalalamika nini.
 
sheria inasema wakificha wapigwe faini ya milioni 500 muulize bashe amewapiga faini mara ngapi walioficha sukari?
Asiwapige,Ila vibali vya kuagiza sukari vizidi kutolewa,anayetafuta ushahidi wa kuficha,akapoteze muda mahakamani
 
Tapeli la kisiasa Hilo.

Bungeni alitoa Kauli Gani?

Alikuwa waziri wa kilimo alifanya Nini?

Hatumtaki na aondoke zakeeee
 
Reincarnation of mpina!!?Ina maana na huyu anapinga maelekezo kutoka juu!!?

Tutarajie kuenguliwa kwake!!?
 
Huyu si minister? Anaifahamu "doctrine of cabinet solidarity"?
Hayo aliyasema akiwa na wadhifa wa wizara hiyo kabla hajahamishwa.
Mrithi wake (Bashe) alipochukuwa wizara, akaona hayo ya mtangulizi wake ni takataka; yeye anafanya yake kama alivyofanya.

Lakini tujikumbushe kidogo: Mkenda aliambiwa "NONSENSE"kwa swala hilo hilo la sukari na kibibi mmmoja ambaye hata shule haijulikani alisoma wapi!
 
Iangalieni vizuri hiyo clip. Hakuna uhusiano kati ya sauti na picha. Hapa wahuni wa mtandao wamewqpiga kanyaboya.

Ni kweli Mkenda alikuwa ni waziri wa kilimo kwenye Serikali ya Magufuli mwaka 2019 na hayo maneno aliyasema. Lakini hakuyasema kwenye mkutano huo.

Hii clip inamharibia tu jina lake Prof Mkenda
 
Kama viwanda vya ndani huficha sukari ili kupaisha Bei,Wacha vife,mashamba yao tulime mpunga
Kila unapo Umefanya vizuri kuitafuta taarifa hii toka huko uliko itoa, lakini unaharibu kujaribu kupindisha habari yenyewe.
Haya uliyoweka hapa si maneno aliyosema Prof. Mkenda baada ya kutokea haya ya Bashe. Haya yalisemwa kabla ya Bashe.
 
Kuna hawa wahindi koo zao zimegawana biashara za kuagiza bidhaa kutoka nje. Kuna wasukari, kuna wa ngano, kuna wa mchele. Watahujumu hatua zozote za uzalishaji wa ndani. Rais aanze kumtema bashe kushindwa kusimamia.
 
Msomali ametoa rushwa haswa
 
Bahati mbaya tuna bunge fake linakubali kuhongwa haliwezi hata kuchunguza mambo ya msingi kama haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…