Mkuu
Unamfahamu nyoka aina ya 'KOBOKO'? hata nyoka aina ya Kobra, Kifutu au Chatu wanamgwaya ile mbaya maana anauwezo wa kuua viumbe hai zaidi ya ishirini na tano kwa mfululizo bila kukata sumu yake. Wakigundua yupo karibu wanajificha kwenye mashimo ya vichuguu nk.
Majini na majoka yote yaliyokuwa kifungoni ndani ya chupa na kutupwa baharini, leo mvuvi mmoja huyo kavua samaki na takataka zingine zikiwemo chupa zenye vizibo akaja nazo pwani akazitupa kwenye matumbawe ufukweni, mara anashangaa kuona moshi unafuka kutokea humo huku ukitoa sauti za lawama aliyetufungia humu atatukoma, hivyo ndivyo inavyotokea sasa.
Wajuaji wote unaowafahamu waliufyata mkia enzi za hayati, baada ya kupita wanajitokeza hadharani kumlaani, kumlaumu na kumhukumu aisye na uwezo wa kujitetea. Kiongozi mnafiki, mwoga na laghai wa jinsi hii hafai kuaminiwa kwa chochote. Historia za utendaji wao wa kazi zinawasuta