Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Tanzania tuna gesi nyingi mpaka sasa inazalishwa mpaka inakosa matumizi,umeme kukatika ni miundombinu mibovu na ya zamani inachangia matengenezo kila kukicha.Bei ya umeme kwa sasa ipo chini ukifananisha na miaka ya zamani.

Watu wanalipa tsh 9,300 kwa unit 78+,ukiona umeme kwako upo juu basi matumizi yenu ni makubwa pia sawa na viwandani
Mkuu unaongelea miaka ya zamani ipi ya bei ipo chini kuliko hio miaka? Watu majiko ya umeme yamebakia kama mapambo, kabla haujanunua taa unaangalia mara nne ina watts kiasi gani..., hao wa bei ya elfu 9,100/= ni wa matumizi madogo yaani units zisizidi 75 kwa mwezi, sasa hizo units lazima taa ziwake kwa mahesabu na kunyosha nguo iwe mpaka ikibidi, kuchemsha maji ya moto mpaka uambiwe na mganga, microwave utaiona kwenye movies....
 
Kwa CV yake tu huyu Profesa, Uweledi wake, Uzoefu wake na Uwezo wake mkubwa wa Akili nakubaliana nae tena kwa 100% juu ya huu Mtazamo wake.

Ni Rais Mpumbavu tu pekee ndiyo hatotaka kufanya Kazi na Mtu very competent kama Profesa Muhongo ambaye hata Mataifa Makubwa na yaliyotuzidi kila Kitu hadi Akili walifanya nae Kazi na sasa wanamtumia pia kama Independent Consultant katika Masuala ya Madini na Jiolojia pia.

Majungu dhidi yake hayasaidii ni Upuuzi.
Hujajibu swali, je kweli umeme wa maji umepitwa na wkati?
 
Google tu gapo uone umeme wa gas na mafuta mwisho wake ni lini huku duniani siyo Tanzania...Nadhani yeye ndiyo kapitwa na wakati tena anatisha...Watu wanaondoka kwenye magari ya mafita walete ya mvuke na betri yeye anawaza hizo dirty energy sources? Tena bila aibu hadharani mchana kweupe! Kweli nimeamini elimu haitusaidii
Wewe jamaa utakuwa unaota, kama ulaya gari zinazotumia mafuta zitaanza ku phase out mwaka 2050, huku nchi za madongo kuinama hesabu miaka mia mbili mbele kabla hizo sources za energy hazijaanza kutumika angalau na watu wachache...
 
Mkuu unaongelea miaka ya zamani ipi ya bei ipo chini kuliko hio miaka ?, Watu majiko ya umeme yamebakia kama mapambo, kabla haujanunua taa unaangalia mara nne ina watts kiasi gani..., hao wa bei ya elfu 9,100/= ni wa matumizi madogo yaani units zisizidi 75 kwa mwezi, sasa hizo units lazima taa ziwake kwa mahesabu na kunyosha nguo iwe mpaka ikibidi, kuchemsha maji ya moto mpaka uambiwe na mganga, microwave utaiona kwenye movies....
Mwaka 2004 Tanzania iliteseka sana na suala la umeme maana mabwawa yalikauka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Solution ikaonekana ni Gas asilia hapo ndo tukapona, ndio ukaona mpaka sasa umeme upo hadi vijijini. Tanzania Afrika mashariki ndio ina gas asilia tu na inaongoza kwa kusambaza umeme katika maeneo mengi nchini kuliko Kenya hata Uganda
 
SSH ni dhaifu ndio maana majizi yote yapo busy kumshauri, ukiona mtu anakushauri ujinga kwa uhuru kabisa ujue anadharau uwezo wa akili. Tutegemee EPA, ESCROW , RICHMOND, IPTL na mengineyo mengi ndani ya hii miaka ya huyu mama.
Naona tutaanza na kupata mgao wa umeme haya majitu akiyapa nafasi tu.
 
Leo nimeshituka kusikia maneno ya Professor Muongo (Mtaalamu wa Nishati) akisema umeme wa Maji sasa Umepitwa na wakati na Uchumi ni Umeme wa Gesi.

Huenda ni kweli ujenzi wa Hydro Electric Power Plant ukawa na gharama mwanzoni na sio kila nchi / sehemu inaweza ikawa na HEP sababu lazima kuwe na viable infrastructure.

Ila ni ukweli usiopingika kwamba umeme wa maji ni renewable (yaani unaweza ukazalishwa tena na tena na tena) Gesi unless otherwise ni Biogas basi uchimbaji wa gesi sio renewable... Nisiwachoshe kuna hii article hapa chini kuhusu gharama ya renewables na umeme wa maji bado ni cheaper... as of 2017 nadhani hii 2021 hali haijabadilika sana

Huyu jamaa anataka kutufanya tufikirie kwamba palikuwepo/kuna upigaji mahali fulani ulioingiliwa na Magufuli.
Sasa kwa vile Magufuli hayupo, anakimbilia haraka haraka kutaka kurudisha upigaji waliokuwa walishaupanga kwenye mradi ule wa gesi

Nina mashaka sana na hawa watu sasa hivi.

Hii sio kawaida hata kidogo. Wewe fikiria, Bagamoyo imerudi kwa kasi kubwa, ikichagizwa toka huko huko Bungeni; bado hatujatulia, huyu naye anakuja na yake kuhusu mradi uliozimwa ghafla na yeye kupoteza wizara!

Kuna mambo hapa.
Rais asipokuwa mwangalifu, kila kitu atakimalizia hapa hapa katika miezi hii michache ya yeye kushika madaraka.

Sitegemei kamwe kwamba miradi inayoendelea itasimamishwa ianze hiyo mingine upya.
 
Wewe jamaa utakuwa unaota, kama ulaya gari zinazotumia mafuta zitaanza ku phase out mwaka 2050, huku nchi za madongo kuinama hesabu miaka mia mbili mbele kabla hizo sources za energy hazijaanza kutumika angalau na watu wachache...
Sasa unakubali kuwa amedanganya kuwa mafuta ndiyo technology ya sasa?

Oneni aibu basi, mafisadi wakubwa!
 
Nyie mataga mtajibu mambo mangapi mitandaoni? Kumbukeni huu ni mwanzo wa Uhuru WA kujieleza kila mtu atasema analojisikia na nyie mnahangaika kijibu,huyu mama atakuwepo mpaka 2030 madaraka nawasihii Tu acheni kujibu kila hoja mtakufa Bure mwaka huu
 
Mwaka 2004 Tanzania iliteseka sana na suala la umeme,maana mabwawa yalikauka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.Solution ikaonekana ni Gas asilia hapo ndo tukapona ndo ukaona mpaka sasa umeme upo hadi vijijini.Tanzania Afrika mashariki ndo ina gas asilia tu na inaongoza kwa kusambaza umeme katika maeneo mengi nchini kuliko Kenya hata Uganda
Kwa hiyo unatakaje.

Umeme unaotokana na maji tusiuhitaji, kwa vile ilitokea ukavu miaka hiyo? Unajua ukame mwingine utatokea lini; na haiwezekani kufikia wakati huo tukawa tumeendeleza vyanzo vingine vya umeme, ikiwemo na gas?
 
Nimemuelewa sana prof. nyie mnaompinga toeni hoja yeye amesisitiza lazima tuwe na vyanzo vingi vya nishati sio maji tu.
 
Sisi wananchi tumekubali mnaomtukana JPM mtukaneni hadi hasira zenu za kunyimwa upigaji ziishe, mkimaliza uzeni SGR, simamisheni JKNHP, bomoeni sekondary zilizojengwa, bomoeni hospital za Wilaya na mikoa zilizojengwa, futeni elimu bure wazi walipe, vunjeni masoko yaliyojengwa, bomoeni stand zilizojengwa, Vunjeni radar tano zilizojengwa ktk viwanja vya ndege. Mkimaliza futeni mikopo ya wanafunzi vyuoni vikuu. Baada ya hapo vunjeni mshikamano ndani ya ccm.Halafu leteni wawekezaji muwakodishe migodi yote
Una uchungu sana mzee, ila ipo siku watamkumbuka mshua.
 
UNa ajira yoyote nchi hii au unatumaini kuajiliwa?
Unanijua? Hivi unanijua wewe? Nikuwekee hapa Uthibitisho wa attachments wa documents za shares na stocks zangu Amazon na Tesla? Nikuwekee hapa financial data na bank statements zangu za Swiss bank, swiss credit, HSBC na Deutsch Bank, laxembourg na offshores?

Ni kuwekee??
 
Consumer costs depends on many factors all in all TANESCO has to be monitored and regulated with close eyes to lower those costs.
You can.t lower the costs lower than production costs unless otherwise utajikuta kama TTCL kuendesha kampuni kwa Hasara

Government intervention in cost lowering by putting standards openly like in Petrol,diesel will contribute a lot.
Its asking a lot for goverment to try and lower costs on something which we need to import and we don't produce / extract

It is the same as telecommunication company like halotel using fibres and airtel using signal poles they charges same consumer costs also HEP and Gas all should deliver cheap and affordable charges.
Its like comparing mangoes to oranges.., after intial investment the maintanance / running costs of fibre and Posts might be nearly the same; but in the case of HEP and continously gas extration we might have a clear wiinner.., thus HEP beinge cheaper...
 
Hawa wanafikiri kuwa viongozi basi ndio wamewazidi akili watu wote.
 
Tuvunje vitu tulivyojenga kwa kodi zetu ? Wewe jamaa wa wapi JPM alitoa percent ngapi kwenye mshahara wake kujenga hivi vitu ?

Tatizo la kutokushauriana na kuweka vitu wazi huenda ndio vinatufikisha hapa..., Huyu anajenga hiki, huyu akija anasema hakina tija..., huyu anapeleka miradi kibao kwao, sababu tu eti atazikwa huko... (Hakuna Miradi ya Mtu..., Kuna Miradi ya Watanzania)
Hivi Kikwete na Magu nani aliyeacha miradi mingi zaidi.
 
Kwa hiyo unatakaje.

Umeme unaotokana na maji tusiuhitaji, kwa vile ilitokea ukavu miaka hiyo? Unajua ukame mwingine utatokea lini; na haiwezekani kufikia wakati huo tukawa tumeendeleza vyanzo vingine vya umeme, ikiwemo na gas?
Upo sawa pia, inatakiwa tusitegemee chanzo kimoja cha umeme...diversification ndo kila kitu tuwekeze kote ili nchi iendelee sio HEP pekee
 
Back
Top Bottom