JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Profesa Mussa Assad amesema anaamini suala la Tozo lina hasara kubwa kuliko faida kwa Serikali.
Amesema “Kuna namna nyingine ya kupata fedha, mfano viongozi wanaotumia magari ya Serikali yenye gharama kubwa kwa shughuli za kiofisini na binafsi, hao ndio wanatakiwa kulipa kodi kwa kuwa wanapata faida ambazo si za kifedha.”
Ametoa mfano wanaotakiwa kukatwa kodi ni Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, wakuu wa mashirika ya Umma na kuwa kama wananunua magari iwe ya gharama ya chini kidogo ili nafuu iwe kwa Wananchi.