Profesa Mussa Assad: Hasara za Tozo ni kubwa kuliko faida zake, Mawaziri ndio wakatwe kodi

Profesa Mussa Assad: Hasara za Tozo ni kubwa kuliko faida zake, Mawaziri ndio wakatwe kodi

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amezungumzia suala la Tozo wakati akihojiwa katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

Profesa Mussa Assad amesema anaamini suala la Tozo lina hasara kubwa kuliko faida kwa Serikali.

Amesema “Kuna namna nyingine ya kupata fedha, mfano viongozi wanaotumia magari ya Serikali yenye gharama kubwa kwa shughuli za kiofisini na binafsi, hao ndio wanatakiwa kulipa kodi kwa kuwa wanapata faida ambazo si za kifedha.”

Ametoa mfano wanaotakiwa kukatwa kodi ni Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, wakuu wa mashirika ya Umma na kuwa kama wananunua magari iwe ya gharama ya chini kidogo ili nafuu iwe kwa Wananchi.
Huwa namwelewa sana huyu Profesa wa ukweli. Siyo yule Dr. wa mchongo wa uchumi
 
Asante baba angu Assad kwa kutupazia sauti
 
Hii maada ni kubwa sana jaribu jukwaa la michezo kuna maada za kutetema kule ukashuke page 3
Mpumbavu huyo jamaa, ungempotezea tu, yeye ndio chawa sasa hivi anakuunga mkono tozo na siku serikali ikisitisha tozo atasifia na kudai serikali sikivu imesikia kilio cha wananchi
 
Hawa Mawaziri wako wangapi mpaka Tozo zao ziweze kubadilisha uchumi wa Nchi.
Hizi sehemu ya ngonjera tu ambazo zinazidi kutuumiza tuliowengi.

Kama wameona mpango wao waunyonyaji hauwezeka sasa wanataka wakatwe wào ili kuonyesha wana huruma kwani ni jambo la kisiasa kwa hali ilivyo watakuja na hii ngonjera ya kukatwa then baada ya miezi minne watajiongezea mishahara ili kuziba hili pengo la Tozo za kisiasa.

Ila mwenyenzi Mungu atatuvusha salama kwa hiki kipindi
 
ASANTE Mzee

We ni kichwa hata WABUNGE walipe Kodi!!

LAKINI
Pia ungemalizia KWA beti hii Hapa;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
Sijawahi kuona hata mara moja wazo la kusema mishahara ya mawaziri na wabunge ikatwe kodi halafu serikali ikasema italifanyia kazi hilo wazo, mara zote huwa linayeyuka kama barafu mchana wa jua kali.

Na ajabu zaidi, huwa hatokei mwanasiasa yeyote, kutoka upande wowote, anayekuwa tayari kuhakikisha analisimamia hilo wazo ili kuona linafanyiwa kazi na serikali, wote huwa kimya..

Hawa jamaa sio wenzetu, huwa tunadanganyika tu, sijui wanatumia madawa gani kutupumbaza.
Mwenge umepumbaza wooooteeeeee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi Jerry Slaa alionesha nini? Maana alikwenda na vitabu viingi.
 
Serikali inalipa mishahara midogo hao mabosi wakubwa ila POSHO gunia zima, wanasema kodi kwa watumishi wa umma inakatwa kwenye Basic salary tu. Kodi kwa watumishi sekta binafsi ikatwe kwenye kila kitu kuleta maana halisi ya PAYE ambayo haina maana hiyo kwa watumishi wa umma.

Mbunge, basic yake walisema ni 2.5m au 3.5m, iliyosalia kufikia hiyo 11m wanayopokea kila mwezi ni marupurupu.

Kwahiyo, hata mkisema wakatwe kodi hao wote, utaratibu ndo utakuwa huo, wanakatwa kwenye basic tu, kodi itakatwa kwenye 2.5m ilhali ana EARN 11m(Paye)

Na ili kuhalalisha huu wizi, marupurupu yote hayawekwi kwenye Salary slip.

Matumizi makubwa yasiyo na tija ndio tobo la kwanza la kuzibwa.

Kuna kigogo mmoja alikuwa na watoto wanaosoma shule mbili tofauti zilizotenganishwa na ukuta tu, wotr wakiingia asubuhi shuleni. Mara nyingi unakutana nao wakishuka kwenye gari zenye namba ST..., cruiser V8, na wakati mwingine kila mtu na yake. Sasa unafikiri, gari nne za serikali zinahudumia familia moja yenye mtumishi mmoja tu serikalini. Gari moja inampeleka baba kazini, mbili zinapeleka watoto shule, moja inampeleka mama saluni, ukute na nyingine inaenda na house helper shopping.

Ndege ya raisi ilipeleka Mkaa visiwani kwa mke mdogo wa nani sijui waliandika kwenye gazeti.
 
Back
Top Bottom