Profesa Mussa Assad: Hasara za Tozo ni kubwa kuliko faida zake, Mawaziri ndio wakatwe kodi

Profesa Mussa Assad: Hasara za Tozo ni kubwa kuliko faida zake, Mawaziri ndio wakatwe kodi

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amezungumzia suala la Tozo wakati akihojiwa katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

Profesa Mussa Assad amesema anaamini suala la Tozo lina hasara kubwa kuliko faida kwa Serikali.

Amesema “Kuna namna nyingine ya kupata fedha, mfano viongozi wanaotumia magari ya Serikali yenye gharama kubwa kwa shughuli za kiofisini na binafsi, hao ndio wanatakiwa kulipa kodi kwa kuwa wanapata faida ambazo si za kifedha.”

Ametoa mfano wanaotakiwa kukatwa kodi ni Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, wakuu wa mashirika ya Umma na kuwa kama wananunua magari iwe ya gharama ya chini kidogo ili nafuu iwe kwa Wananchi.
Professa nimeulewa ila kiukweli viongozi wa Tanzania 90% ni wapumbavu sana, hawana akili ya kutengeneza kesho ya wananchi, ukiwatazama ni watu wazima ila wengi hawana akili timamu, Tanzania inaharibiwa na viongozi wapumbavu kama akina Mwigulu na makundi yote ya hovyo yaliyopo madarakani.
 
Alipokuwa mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali angeyasema hayo ya wasteful spending on executive perks and luxury kwenye ripoti zake kwa maandishi!

Anatafuta cheo tu, anakumbusha Ikulu kwamba yupo mtaani hana kazi.
 
Sijawahi kuona hata mara moja wazo la kusema mishahara ya mawaziri na wabunge ikatwe kodi halafu serikali ikasema italifanyia kazi hilo wazo, mara zote huwa linayeyuka kama barafu mchana wa jua kali.

Na ajabu zaidi, huwa hatokei mwanasiasa yeyote, kutoka upande wowote, anayekuwa tayari kuhakikisha analisimamia hilo wazo ili kuona linafanyiwa kazi na serikali, wote huwa kimya..

Hawa jamaa sio wenzetu, huwa tunadanganyika tu, sijui wanatumia madawa gani kutupumbaza.
Kuamini wanasiasa ni kujilisha upepo

Sio wa chama tawala au wapinzani wote wanafanana kwenye kupigania maslahi yao

Kumbuka kwenye lile sakata lao bungeni kuhusu sitting allowance n.k yaani ilikuwa ngumu kumjua mpinzani na mtawala.
 
Serikali inalipa mishahara midogo hao mabosi wakubwa ila POSHO gunia zima, wanasema kodi kwa watumishi wa umma inakatwa kwenye Basic salary tu. Kodi kwa watumishi sekta binafsi ikatwe kwenye kila kitu kuleta maana halisi ya PAYE ambayo haina maana hiyo kwa watumishi wa umma.

Mbunge, basic yake walisema ni 2.5m au 3.5m, iliyosalia kufikia hiyo 11m wanayopokea kila mwezi ni marupurupu.

Kwahiyo, hata mkisema wakatwe kodi hao wote, utaratibu ndo utakuwa huo, wanakatwa kwenye basic tu, kodi itakatwa kwenye 2.5m ilhali ana EARN 11m(Paye)

Na ili kuhalalisha huu wizi, marupurupu yote hayawekwi kwenye Salary slip.

Matumizi makubwa yasiyo na tija ndio tobo la kwanza la kuzibwa.

Kuna kigogo mmoja alikuwa na watoto wanaosoma shule mbili tofauti zilizotenganishwa na ukuta tu, wotr wakiingia asubuhi shuleni. Mara nyingi unakutana nao wakishuka kwenye gari zenye namba ST..., cruiser V8, na wakati mwingine kila mtu na yake. Sasa unafikiri, gari nne za serikali zinahudumia familia moja yenye mtumishi mmoja tu serikalini. Gari moja inampeleka baba kazini, mbili zinapeleka watoto shule, moja inampeleka mama saluni, ukute na nyingine inaenda na house helper shopping.

Ndege ya raisi ilipeleka Mkaa visiwani kwa mke mdogo wa nani sijui waliandika kwenye gazeti.
Duh [emoji849][emoji848]
 
Hili tunapaswa kulisimamia sisi wananchi. Mishahara na marupurupu makubwa bila ya kulipa kodi ndiyo kulamba asali kwenyewe.

Kumbuka hakuna mwanasiasa bungeni aliyelivalia suala la malipo ya kufuru wanayolipwa kuliganisha na mzigo anaotwishwa mlipa kodi.

Kwa hakika tunataka serikali itakayolipa watendaji wake ikizingatia maslahi kamili ya mlipa kodi.

Hii ni kote bila kujali atakayekuwa madarakani.
Wanatunyonya sana, yule anayepata kingi haguswi, lakini anayepata kidogo ndio mzigo wa kodi na tozo upo juu yake, kweli kupigania haya mambo lazima wananchi wenyewe tuamke.
 
Sijawahi kuona hata mara moja wazo la kusema mishahara ya mawaziri na wabunge ikatwe kodi halafu serikali ikasema italifanyia kazi hilo wazo, mara zote huwa linayeyuka kama barafu mchana wa jua kali.

Na ajabu zaidi, huwa hatokei mwanasiasa yeyote, kutoka upande wowote, anayekuwa tayari kuhakikisha analisimamia hilo wazo ili kuona linafanyiwa kazi na serikali, wote huwa kimya..

Hawa jamaa sio wenzetu, huwa tunadanganyika tu, sijui wanatumia madawa gani kutupumbaza.
Madawa? Yaani nguvu ya Dola unaita Dawa?
Kama 'Dola' yaani vyombo wanvyohodhi vikawa vinatetea Wananchi zaidi na kukabiliana na Rushwa na mengineyo mengi basi hizo tozo tungejua zinafnya nini.

Madhara yake yanapatikana mitandaoni na Nyumbani kwa Mwananchi anayejitutumua kila siku kulisha familia yake.

Sijui kwa nini hakumaliza nakusema tu wanaohusika 'Wajiuzulu' kuwatoza tozo haitoshi.
 
we kibwengo unahisi huo ni upuuzi? Ulitaka ashabikir unyonyaji wa kishamba na kitapeli namna hio?
Big nonsense,Mwenye kuwanyoosha wavivu kama nyie tumbili wa Dar Mwendazake aliweza na angekuwepo tozo mungelipa..

Sasa tuna Rais anataka kufurahisha wapuuzi kama nyie at the expense of poor people in Villages..

Nasemaga mara nyingi SSH anawachekea na kuwadekeza,hata pale Waziri wa Fedha akitoa Takwimu huwa mnabisha ndio maana Mwigulu anabakia peke yake japo ni maamuzi ya Baraza la Mawaziri na sheria ya Bunge.
 
DOMOTOZO lazima mdomo umemdondoka.

Mh. Ndugai, tunaanza lini Kampeni?
tunamhitaji professor Mussa Assard 2025 mimi mwenyewe nitamfuta na team yangu kumshauri akachukue form , mzee wetu amesimamia ukweli miaka yote ya utumishi wake , tunahitaji watu kama hawa with unquestionable integrity>>>.
 
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amezungumzia suala la Tozo wakati akihojiwa katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

Profesa Mussa Assad amesema anaamini suala la Tozo lina hasara kubwa kuliko faida kwa Serikali.

Amesema “Kuna namna nyingine ya kupata fedha, mfano viongozi wanaotumia magari ya Serikali yenye gharama kubwa kwa shughuli za kiofisini na binafsi, hao ndio wanatakiwa kulipa kodi kwa kuwa wanapata faida ambazo si za kifedha.”

Ametoa mfano wanaotakiwa kukatwa kodi ni Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, wakuu wa mashirika ya Umma na kuwa kama wananunua magari iwe ya gharama ya chini kidogo ili nafuu iwe kwa Wananchi.
Duh ngoja tusubiri Madelu aanze kulipa tozo
 
Back
Top Bottom