Profesa Mussa Assad: Hasara za Tozo ni kubwa kuliko faida zake, Mawaziri ndio wakatwe kodi

Wadanganyika mutaisoma namba kweli na mtamkumbuka Rais Magufuli alisema akiondoka yeye kila kitu kitarudi kama zamani sasa muisome namba wabongo poleni sana.
 

Hili tunapaswa kulisimamia sisi wananchi. Mishahara na marupurupu makubwa bila ya kulipa kodi ndiyo kulamba asali kwenyewe.

Kumbuka hakuna mwanasiasa bungeni aliyelivalia suala la malipo ya kufuru wanayolipwa kuliganisha na mzigo anaotwishwa mlipa kodi.

Kwa hakika tunataka serikali itakayolipa watendaji wake ikizingatia maslahi kamili ya mlipa kodi.

Hii ni kote bila kujali atakayekuwa madarakani.
 
Wawapige ban na Clouds sasa maana Dar tv wamepigwa faini kisa Afande Sele kupinga tozo.
 
Unaijua viete wewe [emoji1]

Ac unapigwa mpk unyayoni

Ova
 
Maisha ya watanzania ni kama kitendawili, ukishindwa kupata jibu unampa mji mtoa Kitendawili bila ya wakazi wa huo mji kujulishwa kama kuna mtu kapewa mji wao ili atoe jibu la Kitendawili.
 

Waliondolewa Kodi lini jamani?
 
Watanzania tunasema wajibu wa kuijenga nchi yetu upo mikononi mwetu, Anataka Nani atujengee nchi yetu? Anataka tukope mpaka lini? Sisi tutajifunza lini kujitegemea? Kwani yeye hajaona miradi iliyotekelezwa na kufanyika kutokana na tozo zetu? Nani kakwambia tozo zinanunua magari? Au anabeba kauli za uzushi wa watu wanajifanya upotoshaji
 
Mikopo ilipozidi walitujibu hata kama wakikopa sana hakuna mwananchi atakae gongewa mlango ili atoe hela alipe

Sasa hivi wameweka tozo kila sehem mishahara inakatwa Kodi zaidi ya Mara 3 na unaambiwa Kama hutaki hamia Zimbabwe

Mimi naamini mwisho upo karibu sana hata paka ni mpole ila ukimpiga ukiwa umemfungia chumbani akakosa pakujitetea ndio utajua ukali wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…