Wakati wanatoa tamko nilisikia wanasema kwamba hii ni wiki ya sita hawajapewa hela zao za mikopo na maafisa mikopo hawatoi majibu yanayoeleweka
Sasa hapo wanakosa gani?
Nakumbuka mwaka fulani kule Dodoma wakati UDOM bado haijakamilika, waliohusika na ujenzi walikuwa wachina!
Mwaka huo wanafunzi waliokuwa wanategemea hela ya bodi walicheleweshewa kama hivi hivi!
Kilichokua kinaendelea huko ni huruma tu!
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokuja na pocket money kama za Sekondari ( elfu 20, 30, 50 +) kila walipokuwa wanaomba kusaidiwa na wazazi ama ndugu zao baada ya kuishiwa hawakueleweka! Na sababu ya kutoeleweka ni rahisi tu! WAZAZI WENGI HAWANA UWEZO!
Baada ya kama mwezi bila kitu kueleweka, wale wachina na baadhi ya vibarua"walijifaidisha" mabinti kwa gharama ya kuwanunulia chakula cha siku kwa mama lishe waliokuwa wanauza chakula kule!
Fikiria unaamka asubuhi hauna hata mia tano mfukoni! Rafiki yako naye hana! Nyumbani ukiomba hawana! Halafu wakati huo huo unatakiwa uwe darasani, ufanye assignment na vitu vingine vingi!
Hivi hapa mambo yataenda? Unadhani watu watatoka na kauli laini?
Ni kweli kabisa kwa hali ya makato ya bodi yanavyoenda kwa waliokwishaanza kurejesha hasa watumishi wanalalamika riba imekuwa kubwa (wanaiita value retention fee) pengine sawa au kuzidi hata mabenki!
Lakini sote tunafahamu hali za watanzania hawakopesheki na mabenki na wengine hawana uwezo kumudu gharama za chuo!
Kwasababu waliingia makubaliano ya kuwahudumia kwa mkopo huo, kwanini wasipewe kwa wakati?
Kwanini wanapodai makubaliano yao kuzingatiwa watishiwe kuchukuliwa hatua?
Hii kweli ni sahihi?
Mbona wao kwenye marejesho hawana subira? Tena hadi figisu zimo! Wengine wamepewa mikopo ya vyuo viwili hadi vitatu wakati kimsingi walisoma chuo kimoja!
Badala ya kushughulika na chuo kilichopokea pesa, wanashughulika na mwanafunzi ambaye kimsingi hakutumia pesa hiyo! Hata pale vidhibitisho vinapotolewa bado muhanga anaendelea kuhangaishwa hadi maika miwili mitatu na makato yanabaki vile vile!
Kwa mtu aliyekulia familia bora, anapata kila atakacho, amesoma bila shida kamwe hawezi kujua shida wazipatazo hawa wanaotegemea HESLB!
Waziri Ndalichako hapo amewatusi wanafunzi, hajawatendea haki!
Sent using
Jamii Forums mobile app