Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

USSR,
Serikali inamtumikia nani?
Wananchi au Viongozi dhalimu?
Wanafunzi ni sehemu ya wananchi. Miezi miwili vijana wanaishi kwa dhiki kubwa.

Husikii kila siku anajigamba kuwa pesa zipo? Sasa tatizo liko wapi? Hii so mnasema ni sembe au dona kantri?
 
17 Dec 2019
Waziri Ndalichako amesema kwa kuzingatia uhitaji wa wanafunzi waliojiunga na masomo kwa mwaka 2019/2020 pamoja na kwamba katika bajeti lengo ilikuwa kutoa mkopo kwa wanafunzi elfu 45, lakini hadi kufikia Desemba serikali ilikuwa imetoa mkopo kwa wanafunzi elfu 49, 485 ambao wamepata mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni 172 na milioni 400. - Pia Waziri Profesa Ndalichako, ametoa saa 24 kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam kuhakikisha kuwa kinachukua hatua kwa wanafunzi waliotoa tamko ambalo limekiuka taratibu na kutoa taarifa ni hatua gani zimechukuliwa.


Source: Millard Ayo

Huu utamaduni wa CCM na serikali yake ya awamu ya 5 kushindwa kujibu hoja za msingi ni ugonjwa hatari.

Serikali ya awamu ya 5 ilitakiwa ije na jibu kwa DARUSO, fedha iliyo stahiki kwao ipo wapi na kama haiwezi kupatikana leo lini itapatikana.
 
Siri kali dhaifu inaogopa matamko ya watoto!
Hivi serikali gani duniani itafurahia kupewa masaa kadhaa (kushurutishwa) kutekeleza jambo ambalo bado lipo kwenye majadiliano. Nashauri uongozi wa chuo usitumie jazba ila ichukue hatua ambazo hazitawaumiza hao vijana ila iwape onyo na ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inapaswa kujisahihisha sana.
Kama serikali isipowasikiliza watoto, inategemea waseme kwa jinsi gani kama sio kwa maandamano?

Ikumbukwe kuwa maandamano ni njia ya kudai kusikilizwa kwa mema au mabaya ya karne nyingi tu.

Ubabe unajenga njia ya ziada ya kutaka kusikilizwa.

Kama waziri hataki waandamane basi atumie meza ya mashauriano na viongozi wa wanavyuo.

God bless Tanzania.
 
Kukopa ni harusi,sasa hivi wanalilia kupewa mikopo lakini washaanza kukatwa midomo juu,waziri yuko sahihi,serikali inajua matatizo yao ,huwezi kumuamuru baba yako mzazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali ni mtoto wa wananchi, na siyo mzazi. Wazazi wa serikali ni sisi wananchi tunaoipatia serikali fedha na mamlaka ya kutuongoza. Mwajiri wa serikali ni wananchi.
 
Vijana wameshajibu: Hivi Ndalichako hajui kuwa anapambana na vijana waliopitia JKT, hawa ni jeshi la akiba la nchi, wana nidhamu. Lakini hawana uoga

Img-1576605632277.jpg
 
Vijana wasitumike kisiasa

Wazazi wao wamepambana sana hadi kufikia hatua hiyo

Wakifika vyuoni wasijifanye wanaharakati
Kwahiyo kuikumbusha Serikali kutimiza wajibu wake ni kutumika kisaisa. Ila muda wa Uchaguzi wa Serikali za tunawaimiza kuwachagua wanaccm. Alafu tuna Umoja wa Vijana CCM Vyuo Vikuu, sasa sijui hapo wanatumika kwenye mpira wa miguu au siasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wasitumike kisiasa

Wazazi wao wamepambana sana hadi kufikia hatua hiyo

Wakifika vyuoni wasijifanye wanaharakati
Hawa waliopunguziwa ada, ambao hawajapewa stahiki zao na hawa first year ambao wanavigezo vyote hawajapata mkopo wafanye nn? Haswa baada ya rufaa kubuma?

Mkuu kama vipi nikupatie information za mwanafunzi mmoja umlipie ada kupitia hiyo buku 7

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ivi serikali gani duniani itafurahia kupewa masaa kadhaa (kushurutishwa) kutekeleza jambo ambalo bado lipo kwenye majadiliano. Nashauri uongozi wa chou usitumie jazba ila ichukue hatua ambazo hazita waumiza ao vijana ila iwape onyo na ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali ni wananchi au watawala?
Nipe jibu mkuu ata kwa PM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani wakati tunasoma enzi hizo, tulijua kuwatuliza mawaziri kama huyo. Nakumbuka wakati ule alikuwa ni William Shija. Aliupata fresh. Siku hizi vitoto vyetu vikitikiswa kidg tu badala ya kupambana na serikali wao wanakimbia kupambana na wazazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaogopa hao wakiandamana watafungilia mlango wengine maana wenye madai ni wengi, na propaganda iliyopo ni kuwa awamu hii mambo ni mazuri na nchi ni tajiri. Hivyo hayo maandamano yatatibua hiyo hadaa kwamba sasa hivi mambo ni mazuri.
 
Wakati wanatoa tamko nilisikia wanasema kwamba hii ni wiki ya sita hawajapewa hela zao za mikopo na maafisa mikopo hawatoi majibu yanayoeleweka

Sasa hapo wanakosa gani?

Nakumbuka mwaka fulani kule Dodoma wakati UDOM bado haijakamilika, waliohusika na ujenzi walikuwa wachina!

Mwaka huo wanafunzi waliokuwa wanategemea hela ya bodi walicheleweshewa kama hivi hivi!

Kilichokua kinaendelea huko ni huruma tu!

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokuja na pocket money kama za Sekondari ( elfu 20, 30, 50 +) kila walipokuwa wanaomba kusaidiwa na wazazi ama ndugu zao baada ya kuishiwa hawakueleweka! Na sababu ya kutoeleweka ni rahisi tu! WAZAZI WENGI HAWANA UWEZO!

Baada ya kama mwezi bila kitu kueleweka, wale wachina na baadhi ya vibarua"walijifaidisha" mabinti kwa gharama ya kuwanunulia chakula cha siku kwa mama lishe waliokuwa wanauza chakula kule!

Fikiria unaamka asubuhi hauna hata mia tano mfukoni! Rafiki yako naye hana! Nyumbani ukiomba hawana! Halafu wakati huo huo unatakiwa uwe darasani, ufanye assignment na vitu vingine vingi!

Hivi hapa mambo yataenda? Unadhani watu watatoka na kauli laini?

Ni kweli kabisa kwa hali ya makato ya bodi yanavyoenda kwa waliokwishaanza kurejesha hasa watumishi wanalalamika riba imekuwa kubwa (wanaiita value retention fee) pengine sawa au kuzidi hata mabenki!

Lakini sote tunafahamu hali za watanzania hawakopesheki na mabenki na wengine hawana uwezo kumudu gharama za chuo!

Kwasababu waliingia makubaliano ya kuwahudumia kwa mkopo huo, kwanini wasipewe kwa wakati?

Kwanini wanapodai makubaliano yao kuzingatiwa watishiwe kuchukuliwa hatua?

Hii kweli ni sahihi?

Mbona wao kwenye marejesho hawana subira? Tena hadi figisu zimo! Wengine wamepewa mikopo ya vyuo viwili hadi vitatu wakati kimsingi walisoma chuo kimoja!

Badala ya kushughulika na chuo kilichopokea pesa, wanashughulika na mwanafunzi ambaye kimsingi hakutumia pesa hiyo! Hata pale vidhibitisho vinapotolewa bado muhanga anaendelea kuhangaishwa hadi maika miwili mitatu na makato yanabaki vile vile!

Kwa mtu aliyekulia familia bora, anapata kila atakacho, amesoma bila shida kamwe hawezi kujua shida wazipatazo hawa wanaotegemea HESLB!

Waziri Ndalichako hapo amewatusi wanafunzi, hajawatendea haki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kucheza na serikali ya awamu ya tano na hoja zenu mfu,someni acheni siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Utasoma ukiwa na njaa? Or you mean wakae kimya, wafe kikondoo? Kwa nini mnakuwa na roho mbaya kiasi hiki? Unakosa huruma hata kidogo? Wapeni pesa vijana wasome. Kumekuwa na tabia ya kulaumu graduates wa miaka ya hivi karibuni, kuwa wana graduate wakiwa hawana ujuzi wa kutosha wa kile wanasomea. Mnachoshindwa kujua, serikali ndio sababu.

Imagine mazingira kama haya, mtu atasoma kwa umahiri kweli?
Anyway 2020 haiko mbali, sitayarudia makosa ya 2015.
 
Back
Top Bottom