Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Unafikiria kizamani sana yaani Kijima!
Nyie si ndo wale wale kelele kibaoooo ila hakuna kitu, na huyu mama mnampigia kelele sababu amewazoesha, angekua magu hata kama angesaini mkataba wa kuuza watoto wako usingekuja kupiga kelele hapa.

Mbona hamkuandamana sasa?

Mimi sishabikii chcht hapa, point ni hayo machafuko mnayowaza mkianzisha tunawazima nyinyi kwanza mkafanye machafuko kwa lucifer huko
 
Inawezekana kabisa timu yetu iliyohusika ikiwa pamoja na kocha mkuu na meneja wake hawakuwa na uelewa wa lugha iliyotumika kwenye terms za mkataba huu. Kifupi ni Magungo wa zama zetu maana Kuna terms ikiwemo hiyo ya kutokuvunja mkataba kwa namna yoyote iwayo ile, hata mtoto wa darasa la 5C angeshituka vinginevyo wanaosema bandari imeuzwa kwa wajomba Wana hoja ya msingi na wasikilizwe.
 
Nguzo yetu imara imeangukaa (inauma),
Shujaa wetu shupavu mbona amelalaa, aaah!!
Amefanya makubwa, yakuigwa ya mfano
Magu tunakulilia, twatamani urudi kidogoo,
Mungu kwanini umeruhusu mwamba wetu aende?
Tumebaki na ukiwa nafsi zimejawa kiiza....

Tutakukumbuka kwa mengi uliyoyafanya baba,
Tumebaki wakiwa ila umetuachia kilaza, Tanzania sio salama tena, Magufuli lala salama, mwendo umeumalizaa

Umetuachia kilaza,
Ngorongoro imeuzwaaa,
Tanzania yako baba bandari zimeuzwaa, baba nendaa.
 
Acha uzwazwa mzee. Bora amani ya kijinga kuliko haki yenye fujo.

Watu million 60 huwezi kufanya decision ya kuwafurahisha wote.

Hujifunzi nchi zilizokimbilia kwenye machafuko sasa hvi zinaishije?

Narudia acha uzwazwa aisee.

Yaan mkataba ambao direct impact yake haimfikii hata mtoto wako ndio ufanye nchi iingie kwenye machafuko ambayo yataleta direct impact kwa watoto wako?, tumieni akili basi
Usipangie watu Cha kufanya
 
Hatuhitaji maamuzi ya kufurahisha watu 60m, tunahitaji maamuzi sahihi. Tulipofikia, machafuko tu ndio yatarejesha nchi hii kwenye mstari.
 
Acha uzwazwa mzee. Bora amani ya kijinga kuliko haki yenye fujo.

Watu million 60 huwezi kufanya decision ya kuwafurahisha wote.

Hujifunzi nchi zilizokimbilia kwenye machafuko sasa hvi zinaishije?

Narudia acha uzwazwa aisee.

Yaan mkataba ambao direct impact yake haimfikii hata mtoto wako ndio ufanye nchi iingie kwenye machafuko ambayo yataleta direct impact kwa watoto wako?, tumieni akili basi
Wewe nae ni tahira,eti hauna direct impact unajua unachokiandika au unaandika ukiwa umelewa?
 
Sawa sasa linganisha kipindi cha Jiwe na kipindi cha Maza wapi taifa linaingia hasara;?
Be honest
Tanzania kiongozi pekee alikuwa na uchungu na hii Nchi ni Nyerere tu,wengine wote Mwinyi,Kikwete,Makapa na Magufuli ni mafisadi na kipindi chao wote kumefanyika ufisadi wa kupindukia mwenye s.actor zote za uchumi.

Ingawa Nyerere alikuwa mroho wa madaraka.
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Halafu kuna Chalamila atakuja kupinga 😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom