Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Ila ule sio mkataba, bado hawajaingia mkataba baina ya TPA na DPW
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Halafu yule bibi anadai kuwa eti ameziba masikio
 
Jeshi liko wapi ili litimize wajibu wake wa kikatiba wa kulinda uhuru na mipaka ya nchi?

Ina maana jeshi halijui kuwa bandari ni mpaka?

Ina maana Jeshi halioni kuwa kwa mkataba huu Sovereignity ya nchi iko pabaya?

Majeshi ya nchi yanayojitambua hayawezi kukubaliana na kitu kama hiki!
 
Acha uzwazwa mzee. Bora amani ya kijinga kuliko haki yenye fujo.

Watu million 60 huwezi kufanya decision ya kuwafurahisha wote.

Hujifunzi nchi zilizokimbilia kwenye machafuko sasa hvi zinaishije?

Narudia acha uzwazwa aisee.

Yaan mkataba ambao direct impact yake haimfikii hata mtoto wako ndio ufanye nchi iingie kwenye machafuko ambayo yataleta direct impact kwa watoto wako?, tumieni akili basi
Usihalalishe Wizi wa Rasilimali za Tanganyika kwa logic za kijinga
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Watanzania wanaopewa dhamana ya majadiliano na wageni lazima watuingize mkenge, wait wanavuta Chao,, msala Kwa raia wema
 
Kweli nimeamini huwezi mwelewesha shekh utamu wa nyama choma na bia. Hii serikali haielewi kuwa sisi watanzania ni maskini na sifa ya maskini ni kufatilia mali za urithi. Sasa nyie mnataka kuuza bandari alafu pesa mgawane nyie na vizazi vyenu vyote hapa duniani hata mkifa mna hamu ya kuwa reincarneted kwenye familia zenu ili muendelee kuwa matajiri ndiyo mana akifa mtu anazaliwa mtu kwenye familia zenu?
😬😬😬🤣 Duuh hi sio MCHEZO mkuu umeuliza kwa msisitizo wa hali ya juu taarifa zimfikie HANGAYA THE CHIEF
 
Back
Top Bottom