Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Tulia we dogo muumini wa dhalimu.
Tatizo lako ndio hilo. Msema kweli na mpinga ufisadi unamhusisha na hayati JPM. Ukiulizwa kuweka ushahidi juu ya udhalimu utaweka hapa
 
Tatizo lako ndio hilo. Msema kweli na mpinga ufisadi unamhusisha na hayati JPM. Ukiulizwa kuweka ushahidi juu ya udhalimu utaweka hapa
Wala sio wa kutafuta, ni vile serikali hii ya CCM ina utamaduni wa kulinda uovu wa viongozi wake.
 
Acha uzwazwa mzee. Bora amani ya kijinga kuliko haki yenye fujo.

Watu million 60 huwezi kufanya decision ya kuwafurahisha wote.

Hujifunzi nchi zilizokimbilia kwenye machafuko sasa hvi zinaishije?

Narudia acha uzwazwa aisee.

Yaan mkataba ambao direct impact yake haimfikii hata mtoto wako ndio ufanye nchi iingie kwenye machafuko ambayo yataleta direct impact kwa watoto wako?, tumieni akili basi
Poteleambali kama wewe huwez tuache ss tuandamane Kwa ajir ya vizazi vijavyo sio vya Sasa maana ss tushajichanganya Tyr
 
Inawezekana kabisa timu yetu iliyohusika ikiwa pamoja na kocha mkuu na meneja wake hawakuwa na uelewa wa lugha iliyotumika kwenye terms za mkataba huu. Kifupi ni Magungo wa zama zetu maana Kuna terms ikiwemo hiyo ya kutokuvunja mkataba kwa namna yoyote iwayo ile, hata mtoto wa darasa la 5C angeshituka vinginevyo wanaosema bandari imeuzwa kwa wajomba Wana hoja ya msingi na wasikilizwe.
Watakuwa walipewa chao mapema.
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
CCM Wanambiwa ni jiko la kupikia watu wa kujitoa ufahamu hawaelewi
 
Prof kasema mimi nani nisiunge mkono
Ccm ni majangili wa mchana na usiku wa nchi yetu
Wametoka migodini,mbuga za wanyama sasa wapo kwenye bandari
Ili mradi kipatikane chochote cha kuuza na wao waambulie mgao au kupewa hisa waendelee kuneemeka vizazi na vizazi, ngozi nyeusi ni nyani aliyechangamka anachojali ni ubinafsi tu.
 
Nchi za wenzetu msingi wa elimu yao ya juu sio kukariri na kuelewa theories, bali wanataka uwe na uwezo wa ku evaluate mazingira and applying that knowledge.

Kwa kuwasikiliza hawa wanasheria wa Tanzania na kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa (very average) kuhusu maswala ya magement ya biashara, finance, project management and law of contract. Hitimisho langu ni hili.

1. Nina uhakika wa asilimia zaidi ya 90 Tanzania hakuna chuo kinachofundisha shahada ya business law.

2. (i) Nina uhakika wanafunzi wa masomo ya business management awasomi module ya ‘project management’

(ii) Nina uhakika wanafunzi wa sheria awafundishwi module the law of contract wala business law.

(iii) Similarly module za tort, contract na business law ni mandatory kwenye masomo ya biashara nchi za wenzetu, Tanzania awafundishwi.

Hapo ndio tatizo lilipo hawa watu wanaosoma huo mkataba wanatafsiri literally without the background understanding to envision what those terms mean business.

Mfano uwezi kujua muda wa mkataba kwenye concession/lease agreement bila ya kuelewa thamani ya uwekezaji wa project husika, thamani ya kiwango utakachokuwa unakusanya kurudisha hela yako plus intrest ili upate faida, thamani ya ziada ya muda kwenye FDI kama extra incentive ya kuwekeza hela yako. Mpaka ujue hayo kwanza ndio unaweza panga muda.

Mkataba kuwa governed na sheria za Tanzania, na kutafsiriwa kwa sheria za U.K.
sheria za nchi ni implied terms unless kuwe na clause inayo circumvent sheria husika na kwenye huo mkataba ni dispute resolution tu na utaratibu umeelezwa.

Mengine yote ni subject to Tanzania laws. Whereas sheria za U.K. zitatumika kutafsiri mkataba mahakamani kivipi. U.K. kuna precedents(case laws) za kutosha since 1870 zilizo tafsiri different tests of a contract agreement. Sidhani kama utasoma contract law popote duniani bila ya kutumia hizo precedents kwenye kutafsiri mkataba.

Shida sio mkataba, shida ni uelewa.

Ni busara kuanza kufundisha hizo module vyuoni na kuanzisha hiyo shahada ya business law; nina imani chances are 99.9 hayo mambo hayafundishwi ndio msingi wa tatizo.
 
Back
Top Bottom