Profesa Tibaijuka: Mikataba yote tunayoambiwa ni ya Siri ni mibovu. Ashangaa kwanini wananchi wapo kimya

Nasisi tunashangaa kwanini wasomi wapo kimya, wasomi nao wanashangaa kwanini wananchi wapo kimya, wananchi nao wanashangaa kwanini wazee wapo kimyaa, wazee nao wanashangaa kwanini vijana wapo kimya kwa ufupi tunashangaana.
Nasisi tunashangaa kwanini wasomi wapo kimya, wasomi nao wanashangaa kwanini wananchi wapo kimya, wananchi nao wanashangaa kwanini wazee wapo kimyaa, wazee nao wanashangaa kwanini vijana wapo kimya kwa ufupi tunashangaana.
Hakuna wa kulaumu hapa.sisi sote ni watanzania tunaopaswa kila mmoja wetu kwa nafasi yake achukue hatua kukemea maovu na kuunga mkono mazuri!
 
Inashangaza sana.

Alipokuwa kwenye system lile sakata la IPTL lilimhusu na hakuona huruma kwa wananchi, sasa ndio anaona.

Inakuwa kama mtu ukipewa madaraka akili unazifungia kwenye sanduku mpaka muda wa cheo uishe.
badala ya kumshambulia ka kejili ni vizuri kumpa pongezi maana yeye leo kapata uthubutu wa kusema hivyo ni heri yeye aliyesema na tufahamu kwamba siye yeye mwenyewe anayefahamu uovu uliopo ndani ya hiyo mikataba bali wapo wengine wengi tu wanaofahamu kwa sababu walishiriki katika kuipitisha lakini kati yao hayupo wa kuusema ukweli kama yeye.

na endapo wangekuwepo wengine wa kuusema ukweli kama yeye basi sauti zao zingetosha kukomesha vitendo hivi vya ushiriki wa viongozi kuandaa mikataba mibovu.

Hongera tibaijuka kwa kutueleza ukweli kuhusiana na mikataba mibovu inayosainiwa na serikali!
 
Hongera Professa Anna Kajumulo Tibaijuka Kwa kutufungua macho na masikio
 
Tiketi za ubaya ubwela zimeisha. Jezi elfu 42 Hilo tunafuatilia kweli. Lakini mambo ya msingi Kwa faida ya watoto wetu na wajukuu wetu tukiulizwa tuna majibu mepesi et tutafanyaje Sasa! Aliyeturoga kafa angekuwapo tungemlazisha atutoe kwenye chupa!
Kama kuna uchawi nchi hiii imerogwa basi ni kuwekeza nguvu nyingi sana kwenye mipira ya simba na yanga badala ya kufikiri sana juu ya maendeleo ya nchi na wananchi
 
Ninyi kina Pasco mnafaa sana kutufungua macho wananchi niwaombee msinunuliwe na vyeo au pesa maana ni kama watawala hutamani sana kuwatawala wasiojua kitu na pia watu wakiwa mamlakani huzimwa vinywa.
 
Alitaka Wananchi wafanye kitu gàni?
 
Wasomi wenye msaada kwa nchi .
 
Tibaijuka wewe kachore ramani za miji tu, Huna ulijuwalo katika mikataba ya kibisahra.


Kifafanuwe kifungu hiki tu, labda utatia akili" non-disclosure agreement".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…