TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

By that time, tulikuwa na pathologist wawili tuu!. Sisi tuliosoma Tambaza tulikuwa tunamuona sana mitaa ya around Muhimbili, alikuwa ni kichwa sana!, ila pia...

RIP Prof. James Shaba.
P
Kweli wahenga walisema, muda unaongea, na wenzetu walisema, Time Heals!
Ni mwaka 1984, ndiyo kwanza kijana mtanashati, msomi na nimepata kazi nzuri shirika la umma!
Ndio kwanza nimehamishiwa Dar toka mkoani, sasa niko makao makuu ya shirika langu.
Kwa sheria za kazi miaka hiyo nilikuwa -entitled" kupatiwa nyumba.
Kwa vile nilikuwa bado sijapatiwa nyumba, mwajiri wangu aliniweka hotel kubwa ya kisasa, New Africa Hotel,
Siku hiyo ilikuwa week end mimi niko Bandari Grill, na girlfriend wangu, ambaye atakuja kuwa mke wangu.

Pembeni yangu kama meza ya tatu ,nikamwona mzee mmoja yuko peke yake, akinywa Konyagi, kavu na huku yuko kimya.

Mara wakaingia vijana, kaka zangu, mmoja namfahamu ni Pilot, Captain wa Air Tanzania, lakini yeye hanifahamu.
Nilimfahamu Kapteni George Mazula kwa vile nilikuwa na safari nyingi Mwanza , Arusha na Musoma miaka hiyo na ndege aina ya Fokker Friendship, F50.

Sasa wale vijana kaka zangu, wakaingia wakaanza kumzonga yule mzee.
Wakaanza kumcheka wanamwambia "Profesa uko njwii, uko njwii....acha Konyagi Profesa Shaba"

Nikageuka kumtazama huyo mzee, na nikajiuliza, kumbe huyu ndiye Profesa Shaba?
Jina lilikuwa linajulikana sana, lakini mtu mwenyewe mfupi na mwembamba na ndevu za kutosha usoni, nilikuwa sijawahi kumwona.

Proffessor akameza fundo la Konyagi akawajibu wale vijana,
"Ninyi vijana, ninyi vijana" na huku akionyesha wazi kuwa kinywaji kimekolea.
"Ninyi vijana mtakuja tu mortuary, mtakuja tu. Nimemwona Sokoine nanyi mtakuja tu"

Mwaka huo ndo kwanza amefariki Waziri Mkuu Edward Sokoine, na bado msiba ule wa kitaifa uko fresh mioyoni mwa watu wengi.

Wale vijana na Capt Mazula, walitoweka pale kama wamefukuzwa au kugusa umeme, wote wakaogopa na kutokomea haraka haraka.

Nami nilipigwa butwaa ,lakini nikamsalimia kwa adabu, "shikamoo Proffessor Shaba"

Tukaanza maongezi, lakini kwa jinsi nilivyo mchukulia kiheshima nikagundua mambo mengi juu ya huyu mtu maarufu. He was a humble man na kuwa amekulia Tukuyu, na alikuwa anaifahamu familia yangu toka babu yangu.

RIP Proffessor James Shaba, Mungu akuweke mahali pema peponi.
 
Kweli wahenga walisema, muda unaongea, na wenzetu walisema, Time Heals!
Ni mwaka 1984, ndiyo kwanza kijana mtanashati, msomi na nimepata kazi nzuri shika la umma.l
Ndo kwanza nimehamishiwa Dar toka mkoani, sasa niko makao makuu ya shirika langu.
Kwa sheria za kazi miaka hiyo nilikuwa -entirled" kupatiwa nyumba.
Kwa vile nilikuwa sijapatiwa nyumba, mwajiri wangu aliniweka hotel kubwa ya kisasa, New Africa Hotel,
Siku hiyo ilikuwa week end mimi niko Bandari Grill, na girlfriend wangu, ambaye atskuja kuwa mke wangu.

Pembeni yangu kama meza ya tatu ,nikamwona mzee mmoja yuko peke yake, akinywa Konyagi, kavu na huku yuko kimya.

Mara wakaingia vijana, kaka zangu, mmoja namfahamu ni Kapteni wa Air Tanzania, lakini yeye hanifahamu.
Nilimfahamu Kapteni George Mazula kwa vile nilikuwa na safari nyingi Mwanza na Musoma miaka hiyo na ndege aina ya Fokker Friendship 50.

Sasa wale vijana kaka zangu wakaingia wakaanza kumzonga yule mzee.
Wakaanza kumcheka wanamwambia "Profesa uko njwii, uko njwii....acha Konyagi Profesa Shaba"

Nikageuka kumtazama huyo mzee, na nikajiuliza, kumbe huyu ndiye Profesa Shaba?
Jina lilikuwa linajulikana sana, lakini mtu mwenyewe mfupi na mwembamba na ndevu za kutosha usoni.

Proffessor akameza fundo la Konyagi akawajibu wale vijana,
"Ninyi vijana, ninyi vijana" na huku akionyesha wazi kuwa kinyaji kimekolea.
"Ninyi vijana mtakuja tu mortuary, mtakuja tu. Nimemwona Sokoine nanyi mtakuja tu"

Wale vijana na Capt Mazula, walitoweka pale kama wamefukuzwa, wote wakaogopa na kutokomea haraka haraka.
Nami nilipigwa butwaa ,lakini nikamsalimia kwa adabu, "shikamoo Proffessor Shaba"

Tukaanza maongeze lakini kwa jinsi nilivyo mchulia kiheshima nikagundua kuwa amekulia Tukuyo na alikuwa anaifahamu familia yangu toka babu yangu.

RIP Proffessor James Shaba, Mungu akuweke mahali pema peponi.
Mkuu Lole, Lole Gwakisa, thanks for this, umenikumbusha mbali, Capt. Mazula tulikuwa tunaishi jirani yetu pale Drive In flats, Mafletini!.
P
 
Waziri mku wa nchi gani? Umekurupuka. Tatizo la pombe ya kudoea unafakamaia tu bila kipimo halafu asubuhi huna hata hela ya supu. Una uzee wa shida sana.
Bure kabisa

Halafu ndio mshindane na UVCCM zamani TYL?!! 😂😂😂

Kwani Kawawa wa wapi?!! Duh..
 
Back
Top Bottom