Kweli wahenga walisema, muda unaongea, na wenzetu walisema, Time Heals!
Ni mwaka 1984, ndiyo kwanza kijana mtanashati, msomi na nimepata kazi nzuri shika la umma.l
Ndo kwanza nimehamishiwa Dar toka mkoani, sasa niko makao makuu ya shirika langu.
Kwa sheria za kazi miaka hiyo nilikuwa -entirled" kupatiwa nyumba.
Kwa vile nilikuwa sijapatiwa nyumba, mwajiri wangu aliniweka hotel kubwa ya kisasa, New Africa Hotel,
Siku hiyo ilikuwa week end mimi niko Bandari Grill, na girlfriend wangu, ambaye atskuja kuwa mke wangu.
Pembeni yangu kama meza ya tatu ,nikamwona mzee mmoja yuko peke yake, akinywa Konyagi, kavu na huku yuko kimya.
Mara wakaingia vijana, kaka zangu, mmoja namfahamu ni Kapteni wa Air Tanzania, lakini yeye hanifahamu.
Nilimfahamu Kapteni George Mazula kwa vile nilikuwa na safari nyingi Mwanza na Musoma miaka hiyo na ndege aina ya Fokker Friendship 50.
Sasa wale vijana kaka zangu wakaingia wakaanza kumzonga yule mzee.
Wakaanza kumcheka wanamwambia "Profesa uko njwii, uko njwii....acha Konyagi Profesa Shaba"
Nikageuka kumtazama huyo mzee, na nikajiuliza, kumbe huyu ndiye Profesa Shaba?
Jina lilikuwa linajulikana sana, lakini mtu mwenyewe mfupi na mwembamba na ndevu za kutosha usoni.
Proffessor akameza fundo la Konyagi akawajibu wale vijana,
"Ninyi vijana, ninyi vijana" na huku akionyesha wazi kuwa kinyaji kimekolea.
"Ninyi vijana mtakuja tu mortuary, mtakuja tu. Nimemwona Sokoine nanyi mtakuja tu"
Wale vijana na Capt Mazula, walitoweka pale kama wamefukuzwa, wote wakaogopa na kutokomea haraka haraka.
Nami nilipigwa butwaa ,lakini nikamsalimia kwa adabu, "shikamoo Proffessor Shaba"
Tukaanza maongeze lakini kwa jinsi nilivyo mchulia kiheshima nikagundua kuwa amekulia Tukuyo na alikuwa anaifahamu familia yangu toka babu yangu.
RIP Proffessor James Shaba, Mungu akuweke mahali pema peponi.