Project kubwa ya kilimo RUVU!

Project kubwa ya kilimo RUVU!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
7,113
Reaction score
933
Wakuu natafuta members ili tuanzishe project kubwa ya kilimo RUVU,nimeplani kilimo cha matikiti maji na natarajia kuwekeza mtaji wa kuanzia 5-10million.

Kwa aliyetayari aniwekee PM ili tuongee fresh.Tutaandika mkataba na mgao wa faida ni kwa hisa kutegemea na mtaji wako.

Natarajia kuanza mchakato Januari.

NOTE:sijapata mashamba ila kwa mujibu wa Wataalam pale Ruvu matikiti yanakubali fresh.

Pia kwa anayejua soko zuri zaidi atuwekee hapa ingawa matikiti yana soko zuri.

Naomba kuwasilisha.
 
Good idea,so unahitaji kama idadi ya watu wangapi hivi kufanikisha hilo..mi napenda kujihusisha na masuala ya kilimo nitakutafuta!!!!
 
Una shamba? Ekari ngapi? Lipo karibu na Mto?
 
Wakuu natafuta members ili tuanzishe project kubwa ya kilimo RUVU,nimeplani kilimo cha matikiti maji na natarajia kuwekeza mtaji wa kuanzia 5-10million.
Kwa aliyetayari aniwekee PM ili tuongee fresh.Tutaandika mkataba na mgao wa faida ni kwa hisa kutegemea na mtaji wako.
Natarajia kuanza mchakato jan,
NOTE:sijapata mashamba ila kwa mujibu wa Wataalam pale Ruvu matikiti yanakubali fresh.
Pia kwa anayejua soko zuri zaidi atuwekee hapa ingawa matikiti yana soko zuri.
Naomba kuwasilisha.

Ekari moja sasa hivi Ruvu chini karibu na mto ni mpaka 3m
 
Good idea,so unahitaji kama idadi ya watu wangapi hivi kufanikisha hilo..mi napenda kujihusisha na masuala ya kilimo nitakutafuta!!!!
Naitaji japo 3-5hds ambao tutaweka mtaji wa 20-30m.
 
andika bussness plan yako then kama watu wata ona iko prctical watakujoin.
Thx kwa ushauri mkuu.Ngoja kwanza nipate complete full expenses then ntafunguka either sat.Kwa sasa niko ars nimefatilia mbegu za matikiti hybrid.Na nimezikuta huku.Kesho ntakua mikese morogoro becouse kuna mtu aliniambia pande hizo pia matikiti yanakubali sana.
 
Kama 2km na unalipa 40,000 kwa eka kwa mwaka...manpower ya pale sio nzuri sana vizuri ulete yako.......nilichukua eka 6 mwaka jana zikiwa 900,000 na nimelima vitunguu na matikiti hela yote imerudi
Kukodi karibu na mto ni bei gani kwa heka?na vipi matikiti yanakubali vizuri?vipi kuhusu vitunguu mkuu?jee pia vinakubali?wastani wa shina 1 la tikiti ulipata matikiti mangapi?na vitunguu ulilima kiasi gani na mavuno yakoje?na uliuza bei gani per pc ya tikiti na gunia la vitunguu?mbegu za matikiti ulinunua bei gani?wapi?naomba msaada wako mkuu juu ya maswali niliyokuuliza.
 
Bado sijapata shamba mkuu.
Ni project ya 10-20acres.

Big up sana mkuu kwa juhudi zako katika kilimo.
Mimi nina shamba huku Ruvu. Ndio sasa naanza kusafisha.
Tupo mbali na mto, ila kuna wanavijiji wana mashamba ya kukodi karibu na mto.
Kama unahitaji naweza kuongea nao nikakuunganisha nao kuafanya kazi nao.
Uzoefu wangu wa huko ni kwamba inabidi uwe na wafanyakazi wako toka Dar.
Watu wa kule si wachapa kazi sana.
 
Thanks kwa taarifa mkuu.
Vipi hapo Ruvu matikiti yanakubali vizuri?
Maana nimeambiwa ata mikese pia kuna ardhi nzuri ya tikiti!
 
Thanks kwa taarifa mkuu.
Vipi hapo Ruvu matikiti yanakubali vizuri?
Maana nimeambiwa ata mikese pia kuna ardhi nzuri ya tikiti!

Ruvu matikiti yanakubali sana. Kule kwenye kijiji ambacho sisi tuna mashamba, kuna jamaa wanalima matikiti na wanapata sana.
Ardhi ya kule in ya udongo mweusi wenye rutuba sana.
Changamoto ni maji tu, ndio maana jamaa wale kule Ruvu wanapendelea kukodi mashamba yaliyo karibu na mto Ruvu.
Ukiwa tayari, unaweza kunishtua nikakuunganisha na wanavijiji wenye mashamba yaliyo karibu na mto.
 
Kuweka Irrigation system ekari 20 inarange kwenye 60M.. so as your planning try to do a thorough research kwenye estimations zako. Kwa haraka sana naona it is good to start small and grow big....!!
 
Back
Top Bottom