Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Tujikumbushe, projects kadhaa ambazo Mchungaji Dkt. Kimaro amezifanya akiwa Mchungaji Kiongozi, KKKT Usharika wa Kijitonyama,
1. School of Healing (Morning & Evening Glory) -Youtube Channel (mwanzoni ikiwa Eliona Kimaro TV baadae KKKT Usharika wa Kijtonyama) inayowafikia watu wote Duniani.
2. Jengo jipya la Sunday School (lililogharimu yapata takribani 200m TZS)
3. Ununuzi wa Kiwanja pembezoni mwa kanisa yapata 300m TZS
4. Kusomesha yatima yapata 100
5. World Pray Online (WPO), Call Centre ya maombi masaa 24, siku 7 za wiki.
NB: Ikumbukwe waliokuwa wanasali hizo Morning & Evening Glory wengi hawakuwa waumini wa KKKT bali wa madhehebu mengine na Waislam kuondoka kwake Dkt Kimaro tutarajie mabadiliko kiasi. Hope Mchungaji Kiongozi (Mpya) Anna amejipanga vilivyo kuendeleza alipoishia Dkt Kimaro.
Mimi binafsi napenda Kimaro. Ni Mtumishi anayeipenda kazi yake. Hakuwahi kulala kwenye Huduma ya Kichungaji. Hizi morning na evening Glory ni ubunifu wake Kazini. Wengine hawana kwenye Sharika zao. Seminar za kujifunza Neno na stadi za Maisha ni Ubunifu wake zimewainua Wengi Kiroho, Kimwili na Kiakili.. Amejenga Mahusiano na Watu, Sharika, nje, dini, madhehebu mengineyo Kwa Amani na Furaha kabisa. Leo hii umamsimamisha Kazi Kihuni watakubali Wafuasi watoa Sadaka zinazolipa Mishahara Yao? Wanadahau % wanazopokea huko juu zinakotoka. Ngoja Waumini wasuse ndio Watajua hekima inatakiwa kwenye Maamuzi.
 
KKKT ni taasisi na sio Mali ya mtu binafsi

Anawajibika Kwa taasisi ambayo ndiyo mwajiri wake

Taasisi ndiyo inajua kwanini imempa likizo ya siku 60

Umaarufu wake hauondoi mapungufu yake
Waumini ndiyo waliounda KKKT na kuifanya Taasisi. Usiwachokoze. Moto utalipuka. Mapungufu yapi Mapya ambayo hayafantwa hapa Duniani? Kabaka Mtu? Kaoa Mwanaume mwenzie? Kafungisha Ndoa Mashoga? Kajitangazia Uaskofu? Watieni moyo wanaotunza Roho za Watu siyo kuwadhusha Morali zao.
 
Kweli hayanihusu nmeshindwa kuelewa nmeona meku kimaro anatajwa tajwa hapa
Anyway haki itendeke
 
Daah! Roman Catholic will remain the best Church ever in every thing eg. Leadership structure, Ethics, Faith and all what you know. Hivi kweli hata wewe mleta Uzi na usomi wako( nahisi kidogo umefanikiwa kubukua) unaweza ukaeleza kuwa hayo unayoita mafanikio ya Kimaro ni yeye ndio kayaleta na sio Mungu, kanisa na Waumini? Hao yatima amewasomesha kutoka pesa ya mfukoni mwake, ? Hicho kiwanja Cha mil 300 ni fedha zake binafsi au sadaka. Kanisa sio Mali ya mchungaji,Wala askofu. KKKT wanapaswa kusimama kwelikweli na ikiwezekana wakajifunze Kwa mlezi wao Catholic. La sivyo taasis itavurugwa sana na watu wasio tambua maadili na misingi ya kulinda taasisi Yao ya kidini. Ngoja niishie hapo,anayetaka kubishana NAMI aje saiz
 
Hizi project Ni minor Sana ukilinganisha na anachofanya mastai pale kimara korogwe Kuna shule na hospital na mall na hzo zote za evening na morning Glory

Alichonikera Ni sifa alizo wapa wakatoliki waswasi Tena mbele ya kwaya kwa kuwaita viongozi wetu kuwa Ni matapeli sijapenda hilo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

Unaijua vita anayopigwa Mastai?

Ndiyo vita aliyopigwa Kimaro shida tu huyu kaingia kwenye 18
 
Waumini ndiyo waliounda KKKT na kuifanya Taasisi. Usiwachokoze. Moto utalipuka. Mapungufu yapi Mapya ambayo hayafantwa hapa Duniani? Kabaka Mtu? Kaoa Mwanaume mwenzie? Kafungisha Ndoa Mashoga? Kajitangazia Uaskofu? Watieni moyo wanaotunza Roho za Watu siyo kuwadhusha Morali zao.
Amen
 
Mimi binafsi napenda Kimaro. Ni Mtumishi anayeipenda kazi yake. Hakuwahi kulala kwenye Huduma ya Kichungaji. Hizi morning na evening Glory ni ubunifu wake Kazini. Wengine hawana kwenye Sharika zao. Seminar za kujifunza Neno na stadi za Maisha ni Ubunifu wake zimewainua Wengi Kiroho, Kimwili na Kiakili.. Amejenga Mahusiano na Watu, Sharika, nje, dini, madhehebu mengineyo Kwa Amani na Furaha kabisa. Leo hii umamsimamisha Kazi Kihuni watakubali Wafuasi watoa Sadaka zinazolipa Mishahara Yao? Wanadahau % wanazopokea huko juu zinakotoka. Ngoja Waumini wasuse ndio Watajua hekima inatakiwa kwenye Maamuzi.
Natabiri 22/1/2023 patachimbika
 
Kila usharika KKKT una baraza la wazee, sharika ngapi zimefanya hayo yote? Nenda Usharika wq Sinza bado wanapambana na Deni mpaka kesho, Mwenge hali kadhalika.
NB: Kimaro hata apelekwe GEZAULOLE ataonyesha maajabu, jiulize kabla ya Kimaro-Knyama hapo Kinyama mbona kulikua jiiiii
Usharika wa K-nyama ni mkubwa sanaa chief usiuchukulie poa poa unafahamika tangu enzi kwa makubwa yake
 
Kuna tuhuma haheshimu wakubwa anafanya anavyotaka ...hafuati misingi ya kanisa ...
Makanisa yote yenye mfumo wa taasisi usipokubaliana na wakubwa hata kama wako wrong kisa ukajidai kusema biblia inasema hvi lazima wakule kichwa 😁, Yesu mwenyewe mafarisayo walimla kichwa Kwa sababu hzi hzi , wao waliona ndo wakubwa Ila yeye mara nyingi akawa anatofautiana nao hadharani ....
 
Kwenye kila baraka kuna laana
Kila penye mafanikio pana mapungufu
Kufanya mambo fulani hakukufanyi kuwa mkubwa kuliko taasisi
Kkkt kinyama imekuwa kubwa kabla ya kimaro
Pengine kwaya ya uinjilist knyama miaka ile ikiongozwa na joshua ndio walifanya kanisa kuwa kubwa sana miama 2000

Ujenzi wa jengo la kitega uchumi ghorofa ile ni ya mwaka 2006 hivi kama sikosei

Kituo cha watoto yatima kimekuwepo tangu

Nakumbuka nikiwa kijana wa mafunzo ya kipaimara tulikuwepo na kituo kijichi na tulienda mara kadhaa kutembelea
( kijichi kumbukumbu inaweza kiwa sio sawa jina )

Kujaza waumini

Ile kanisa inajaza mpaka nje ndo chanzo tv zikawa zinafungwa nje kabla ya kimaro

Kuna muda huwa namuona kimaro kama pandikizi kutoka sehemu flani ( hapa mungu anisamehe kama ntakosea)

Kkkt ni taasisi
Ina misingi kama taasisi nyingine
Mf roma wana mpaka amri za kanisa
Kiuka hizo uone cha moto
 
Kila usharika KKKT una baraza la wazee, sharika ngapi zimefanya hayo yote? Nenda Usharika wq Sinza bado wanapambana na Deni mpaka kesho, Mwenge hali kadhalika.
NB: Kimaro hata apelekwe GEZAULOLE ataonyesha maajabu, jiulize kabla ya Kimaro-Knyama hapo Kinyama mbona kulikua jiiiii
Ngoja aende namtumbo akapige injili
 
Nimekufuatilia sana nikagundua wewe mfia kkkt na haukubaliani ma mabadiliko ya kiroho.
Bado unaipenda kkkt iliyodumaa kiroho na hukupendezwa na huduma za uamsho za Kimaro.
Nimekugundua kuwa umhafidhina na sio imani sahihi ya Kikristo.

Kkkt ni dude kubwa ambalo halina msaada katika jamii bado lipo kuwanyonya wa kkkt kimapato ilhali mrejesho katika jamii ni hafifu sio kiriho wala kimwili.

1. Shule za kkkt ziko kipigaji ma ziko taabani
2. Hotel ya corodor spring wakunwa walipiga zaidi ya 3B waumini wamechangishwa karibu wafe na wakakimbia walio wengi.

3. Selian hospital nahitaji kusema zaidi?

Bora Kimaro mara 1000 kuliko hao wachungaji na maaskofu vihiyo.

Note: mimi sio mkkkt lakini naijua jadi gizani
Pilipili ya shamba inakuwashia nini?
 
Mimi binafsi napenda Kimaro. Ni Mtumishi anayeipenda kazi yake. Hakuwahi kulala kwenye Huduma ya Kichungaji. Hizi morning na evening Glory ni ubunifu wake Kazini. Wengine hawana kwenye Sharika zao. Seminar za kujifunza Neno na stadi za Maisha ni Ubunifu wake zimewainua Wengi Kiroho, Kimwili na Kiakili.. Amejenga Mahusiano na Watu, Sharika, nje, dini, madhehebu mengineyo Kwa Amani na Furaha kabisa. Leo hii umamsimamisha Kazi Kihuni watakubali Wafuasi watoa Sadaka zinazolipa Mishahara Yao? Wanadahau % wanazopokea huko juu zinakotoka. Ngoja Waumini wasuse ndio Watajua hekima inatakiwa kwenye Maamuzi.
Hekima haikutumika kwenye hili
 
Kabisa mwaya! [emoji848][emoji848]

Tulishapasahau miaka mingi tangu enzi za ile kwaya ya wakongo ya wimbo hakuna Mungu kama wewe Kijitonyama ilikuwa kama haipo,

Usharika huo umekuja kujulikana baada ya Pastor Kimaro kuja huo ndio ukweli.

Hivi huyo Anna anazani ataweza kutembelea nyota ya Kimaro kweli ?
Kanisani unafuata nyota ya mchungajii au kumuomba Mungu wako?
 
Back
Top Bottom