Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Mimi binafsi napenda Kimaro. Ni Mtumishi anayeipenda kazi yake. Hakuwahi kulala kwenye Huduma ya Kichungaji. Hizi morning na evening Glory ni ubunifu wake Kazini. Wengine hawana kwenye Sharika zao. Seminar za kujifunza Neno na stadi za Maisha ni Ubunifu wake zimewainua Wengi Kiroho, Kimwili na Kiakili.. Amejenga Mahusiano na Watu, Sharika, nje, dini, madhehebu mengineyo Kwa Amani na Furaha kabisa. Leo hii umamsimamisha Kazi Kihuni watakubali Wafuasi watoa Sadaka zinazolipa Mishahara Yao? Wanadahau % wanazopokea huko juu zinakotoka. Ngoja Waumini wasuse ndio Watajua hekima inatakiwa kwenye Maamuzi.
 
KKKT ni taasisi na sio Mali ya mtu binafsi

Anawajibika Kwa taasisi ambayo ndiyo mwajiri wake

Taasisi ndiyo inajua kwanini imempa likizo ya siku 60

Umaarufu wake hauondoi mapungufu yake
Waumini ndiyo waliounda KKKT na kuifanya Taasisi. Usiwachokoze. Moto utalipuka. Mapungufu yapi Mapya ambayo hayafantwa hapa Duniani? Kabaka Mtu? Kaoa Mwanaume mwenzie? Kafungisha Ndoa Mashoga? Kajitangazia Uaskofu? Watieni moyo wanaotunza Roho za Watu siyo kuwadhusha Morali zao.
 
Kweli hayanihusu nmeshindwa kuelewa nmeona meku kimaro anatajwa tajwa hapa
Anyway haki itendeke
 
Daah! Roman Catholic will remain the best Church ever in every thing eg. Leadership structure, Ethics, Faith and all what you know. Hivi kweli hata wewe mleta Uzi na usomi wako( nahisi kidogo umefanikiwa kubukua) unaweza ukaeleza kuwa hayo unayoita mafanikio ya Kimaro ni yeye ndio kayaleta na sio Mungu, kanisa na Waumini? Hao yatima amewasomesha kutoka pesa ya mfukoni mwake, ? Hicho kiwanja Cha mil 300 ni fedha zake binafsi au sadaka. Kanisa sio Mali ya mchungaji,Wala askofu. KKKT wanapaswa kusimama kwelikweli na ikiwezekana wakajifunze Kwa mlezi wao Catholic. La sivyo taasis itavurugwa sana na watu wasio tambua maadili na misingi ya kulinda taasisi Yao ya kidini. Ngoja niishie hapo,anayetaka kubishana NAMI aje saiz
 

Unaijua vita anayopigwa Mastai?

Ndiyo vita aliyopigwa Kimaro shida tu huyu kaingia kwenye 18
 
Amen
 
Natabiri 22/1/2023 patachimbika
 
Usharika wa K-nyama ni mkubwa sanaa chief usiuchukulie poa poa unafahamika tangu enzi kwa makubwa yake
 
Kuna tuhuma haheshimu wakubwa anafanya anavyotaka ...hafuati misingi ya kanisa ...
Makanisa yote yenye mfumo wa taasisi usipokubaliana na wakubwa hata kama wako wrong kisa ukajidai kusema biblia inasema hvi lazima wakule kichwa 😁, Yesu mwenyewe mafarisayo walimla kichwa Kwa sababu hzi hzi , wao waliona ndo wakubwa Ila yeye mara nyingi akawa anatofautiana nao hadharani ....
 
Kwenye kila baraka kuna laana
Kila penye mafanikio pana mapungufu
Kufanya mambo fulani hakukufanyi kuwa mkubwa kuliko taasisi
Kkkt kinyama imekuwa kubwa kabla ya kimaro
Pengine kwaya ya uinjilist knyama miaka ile ikiongozwa na joshua ndio walifanya kanisa kuwa kubwa sana miama 2000

Ujenzi wa jengo la kitega uchumi ghorofa ile ni ya mwaka 2006 hivi kama sikosei

Kituo cha watoto yatima kimekuwepo tangu

Nakumbuka nikiwa kijana wa mafunzo ya kipaimara tulikuwepo na kituo kijichi na tulienda mara kadhaa kutembelea
( kijichi kumbukumbu inaweza kiwa sio sawa jina )

Kujaza waumini

Ile kanisa inajaza mpaka nje ndo chanzo tv zikawa zinafungwa nje kabla ya kimaro

Kuna muda huwa namuona kimaro kama pandikizi kutoka sehemu flani ( hapa mungu anisamehe kama ntakosea)


Kkkt ni taasisi
Ina misingi kama taasisi nyingine
Mf roma wana mpaka amri za kanisa
Kiuka hizo uone cha moto
 
Ngoja aende namtumbo akapige injili
 
Pilipili ya shamba inakuwashia nini?
 
Hekima haikutumika kwenye hili
 
Kanisani unafuata nyota ya mchungajii au kumuomba Mungu wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…