Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Kuna tuhuma haheshimu wakubwa anafanya anavyotaka ...hafuati misingi ya kanisa ...
Taja hiyo misingi ya kanisa? Kimaro kama ni unyenyekevu kazidisha. Angekua mwingine angeshatoka kuanzia akiwa KARIAKOO maan nako haikua rahisi.
 


Ni kweli.

Na ikiwa hivyo basi na ijulikane kuwa vita hii si zidi ya Kimaro bali ni ya Bwana,

Sisi tusimame tuweze kuona wokovu wa Bwana.
 



Hao Catholic wana yao wala sio kusema Eti labda ni vipi!

Halafu hoja ni kwamba walishapita wachungaji wengi sana kabla ya yeye kupelekwa hapo Kijitonyama, lakini kwa kuangalia historia na muda ni kuwa yeye amefanya mambo mengi mazuri sana .
 
Hiyo barua imekaa kama kumdhalilisha Dr Kimaro. Kwa kosa lipi umpe likizo siku 60? Kama ni uhamisho kwann isiwe sasa? Haya mambo ndo yaliwakimbiza kina Mwingira KKKT
 
Hao Catholic wana yao wala sio kusema Eti labda ni vipi!

Halafu hoja ni kwamba walishapita wachungaji wengi sana kabla ya yeye kupelekwa hapo Kijitonyama, lakini kwa kuangalia historia na muda ni kuwa yeye amefanya mambo mengi mazuri sana .
Tukubali Kimaro Ni jembe. Kabla yake aliyekuwepo Kijitonyama alifanya mangapi? Baada ya kuondoka Kariakoo Hali ipoje Sasa?
 
Ningekuwa jamaa ningeanzisha kanisa ndo nipige mkwanja mrefu. Akizubaa hapa atakuwa mchaga wa ajabu san
 
Zile TV kila kona ya kanisa si kitu kidogo. Nenda KKKT Mwenge au Sinza ndo utajua nguvu ya Dkt Kimaro
 
ni masikitiko haswaa. Ila utashangaa KKKT wapo kimya maovu yakifanyika kwenye jamii. UK hutoa ruzuku kwa wachungaji design ya Dr. Kimaro hapa wanamchukulia poa.
 
Hawa jamaa wangetafuta consultant awashauri kwenye hiyo miradi yao SHULE (waumini wanachangia halafu ukipeleka mtoto hapo unachanjwa upya kama mgeni). Selian ipo sehemu very STRATEGIC ila uongozi sasa!
 
Niseme tu, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Kilichokuwa kinatakiwa kufanyika ni kum demolish Kimaro tangu akiwa Usharika wa Kariakoo.

Kwa miaka mingi tumefanya mbinu na njama mbalimbali kumuondoa lakini hazikuwq na matokeo tuliyo yatarajia. Hivyo tukajaribu mbinu nyingine na nyingine tena, hatimaye leo mbuyu haujaanguka ila umemwagika.

Mara ya kwanza tulipofanya yetu akiwa pale Kariakoo alikimbia usharika na kwenda kujificha kwa Mapadre, na mapadre ndio waliofanya jitihada hadi akarudi tena usharikani, ila hii ya sasa harudi, na akirudi basi itakuwa zamu yetu kusalimu amri.

Kimaro alipokuwa Kariakoo, sio kwamba aliharibu taratibu za ibada hapana, hii ni cover tu, tunayoitumia.

Kimaro alipokuwa Kariakoo aliharibu biashara za wengi kwenye ulimwengu wa roho.

Watu walikuwa na madhabahu zao kubwa ambazo ziliprovide ulinzi wa pesa na mali, pia zikikuwa zikivuta mali kutoka kwa maboya wengine.

Alipofika Kimaro, wale ambao tulikuwa tukizivuta mali zao, wakaanza kumiminika kule kila alfajiri, ulinzi wa mali zao ukaanza kuongezeka, na zile biashara zao ambazo tulizifanya zisionekane na wateja zikaanza kuonekana, na taratibu taratibu wakaanza kukua na kutupora wateja wetu.

Kwa msio na ufahamu wa biashara, hamna biashara isiyo na madhabahu (iwe ya asili au hizo kama za Kimaro), hamna biashara isiye na kuhani, na wala hamna biashara isiyotolewa sadaka/kafara.

Watu wakaanza kufundishwa kutoa sadaka za maneneo na manuizi kwa ajili ya biashara zao, tukapata upinzani sana.

Kwa kushirikiana na wenzetu ndani ya kanisa, tukaanza figisu. Ibada hizo mpya zifutwe na ikiwezekana Kimaro ahamishwe Kariakoo.

Tukafanya Kimaro apitie magumu, tukakausha kabisa hali ya utoaji wa sadaka hadi kanisa likashindwa kulipia umeme na maji, tukahakikisha wanapitia kwenye hali ya ugumu kweli kweli.

Baadae Kimaro anajua alichokifanya, akapindua meza, hali ya uchumi wa kanisa ikaimarika sana, likawa pigo lingine kwetu.

Kipindi kile mkuu wa kanisa alikuwa yule jamaa wa Mbeya, tukafanya kila liwezekanalo ahamishwe. Ndipo akapelekwa Kijitonyama.

Zama zile Kijitonyama alikuwepo dogo mmoja anaitwa Kinyaha, hayo mambo ya ibada za asubuhi yalikuwa hayapo au yamekufa kabisa.

Ibada ilikuwa ikihudhuriwa na vizee vienne, wakizidi sana sita. Sasa alipokuja Kimaro sijajua alikuja na mguu upi, akaleta ibada za asubuhi na usiku.

Watu wakaanza kufurika, akaanza kununua nyumba za watu wetu na kuzifanya kuwa za kanisa. Kijitonyama yote ilikuwa ni ngome yetu.

Kata ya Kijitonyama ndio kata ina vijiji viwili mjini kati Dar es Salaam. Kijiji cha Mwenge na Kijiji cha Makumbusho. Jina na asili Kijitonyama sitaki kulielezea leo, lakini kaa ukijua kuwa ile ni ngome yetu na sehemu yetu ya kulia nyama na vitu vyetu vya kutuongezea nguvu. Kijitonyama ndiko kwenye madhabahu ya kuteketeza, ndio maana hata Wahindi miili yao huchomewa Kijitonyama.

Pale tulijaribu mbinu za kishushu, kuna kipindi tulitaka kumfitinisha na serikali kwa kupitia kijana aliyejinyonga kwa madeni aliyokuwa nayo, lakini alikwepa vihunzi kwa namna ya ajabu kabisa.

Kwetu sisi ni furaha, watu waharibifu aina ya KIMARO hawafai, wakakae huko vyuoni wafundishe. Na tutammaliza kwa njia hiyo.
 
Amepiga simu polisi kuomba usaidizi ili aweze kuanzisha ibada ya masifu ya asubuhi kesho asubuhi, anapiga piga simu ovyo kusumbua wazee wa watu kuulizia hali ilivyo baada ya kufanikiwa kutoroka kanisani
Duuh. Mara hii kaanza kupiga simu mbona mapema? Aendelee alipoishia dkt. Kimaro jamani hizi taasisi zinataka kujitoa na unyenyekevu sasa wewe ukija macho juu lazima macho yakutoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…