Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Tena chuki kubwa mnoo hapo wameshatafuta namna ya kumwangusha na hatokaa apate upenyo wa kuyafanya yale aliyoyafanya kijitonyama....labda aanzishe mwendo kivyake na si chini ya taasisi tena
Chuki ipi, aanzishe KKKT yake kama Dr. Mwaikali.....
 
Hii dhana ya ukubwa kuliko taasisi kwani kanisa ni mali ya mtu,au genge la watu?. Kanisa sio jengo, ni mwili wa Kristo ambapo watu wenye imani juu Kristo wanaamua ku team up na kumtafuta Mungu hata kwa kupapasa wakamwone sasa kuwa na kiongozi mwenye kuonyesha njia imekuwa nogwa?. Mwenye kanisa ni Mungu, mwenye roho za watu ni Mungu.
Eti wengine wakajidai kuzimia UJINGA bwana....
 
Nimekufuatilia sana nikagundua wewe mfia kkkt na haukubaliani ma mabadiliko ya kiroho.
Bado unaipenda kkkt iliyodumaa kiroho na hukupendezwa na huduma za uamsho za Kimaro.
Nimekugundua kuwa umhafidhina na sio imani sahihi ya Kikristo.

Kkkt ni dude kubwa ambalo halina msaada katika jamii bado lipo kuwanyonya wa kkkt kimapato ilhali mrejesho katika jamii ni hafifu sio kiriho wala kimwili.

1. Shule za kkkt ziko kipigaji ma ziko taabani
2. Hotel ya corodor spring wakunwa walipiga zaidi ya 3B waumini wamechangishwa karibu wafe na wakakimbia walio wengi.

3. Selian hospital nahitaji kusema zaidi?

Bora Kimaro mara 1000 kuliko hao wachungaji na maaskofu vihiyo.
Sikawasifia? mpeni no. ya sheikh kipozeo tuachie KKKT yetu salama...
 
Tena chuki kubwa mnoo hapo wameshatafuta namna ya kumwangusha na hatokaa apate upenyo wa kuyafanya yale aliyoyafanya kijitonyama....labda aanzishe mwendo kivyake na si chini ya taasisi tena
hapa ndio napata mwanga ni kwanini kitu kinachoitwa protestants kilipotokea.Mtu kama huyu akiamua kujiengua na akaanzisha dhehebu lake wafuasi wengi wanamfuata.Hapa ndio dini za kikristo zinapochemshaga na ndio utitiri wa madhehebu unapotokea waslam wao hawako hivi kivile japo nao wana madhehebu yao lakini sio kwa kasi kama ya wakristo
 
Sahihi Sana Hilo ,alijisahau Sana Hadi kuanza kuwasifu wakatoliki na waisalmu hadharani eti ,roma Catholic wako vzr so wat aende uko sasa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hlafu nina mshaka hawa wote wanaojitokeza kwenye maandamano ya kumuunga mkono ni hao VIJANA waaminifu anadai kawaajiri....
 
Alijisahau Sana Hadi kuanza kuwasifu Wakatoliki na Waisalmu hadharani eti ,roma Catholic wako vizuri aende uko sasa...
Mzazi/mlezi akiwaambia kwenye kikao cha familia/ukoo kwamba nyie sio waaminifu kama watoto wa fulani mtamsusa na kumpasua?
 
hapa ndio napata mwanga ni kwanini kitu kinachoitwa protestants kilipotokea.Mtu kama huyu akiamua kujiengua na akaanzisha dhehebu lake wafuasi wengi wanamfuata.Hapa ndio dini za kikristo zinapochemshaga na ndio utitiri wa madhehebu unapotokea waslam wao hawako hivi kivile japo nao wana madhehebu yao lakini sio kwa kasi kama ya wakristo
Ajiengue tu, hata Mwaikali alijiengua, yuko wapi??? KKKT bado iko imara, hawa wanataka kuanzisha "MAMLAKA" ndani ya mamlaka, hilo haliwezekani...
 
Hao Catholic wana yao wala sio kusema Eti labda ni vipi!

Halafu hoja ni kwamba walishapita wachungaji wengi sana kabla ya yeye kupelekwa hapo Kijitonyama, lakini kwa kuangalia historia na muda ni kuwa yeye amefanya mambo mengi mazuri sana .

Mengi yepi?. Project kubwa pale ni Jengo la kitega uchumi. Nani alilihamasisha?. Acheni siasa kanisani
 
Tumsubiri huyo Mchungaji Msaidizi kama ataweza kuendesha hizo projects (maana nina uhakika pesa ilikua inatoka kwa waumini ambao wamestuka kwa Dkt Kimaro kupewa likizo na kuhamishwa Kijitonyama.
Kumbe shida ni PROJECT!!!
 
Tukubali Kimaro Ni jembe. Kabla yake aliyekuwepo Kijitonyama alifanya mangapi? Baada ya kuondoka Kariakoo Hali ipoje Sasa?

Acheni siasa kanisani. Nyie mmeijua KKKT Kijitonyama leo, mnalazimisha wengine wawa sikilize. KKKT Kijitonyama ilikiwa inajaa mpaka nje, kabla ya huyo Kimaro. Halafu Hilo jengo la kitega uchumi kalijenga Nani?. Usidharau ambachao kwa msala upitao. Kijitonyama ilikuwa maarufu enzi na enzi, huyu katumia umaarufu wa kijitonyama kujijengea jina.
 
Alijisahau Sana Hadi kuanza kuwasifu Wakatoliki na Waisalmu hadharani eti ,roma Catholic wako vizuri aende uko sasa...
Kwahiyo kilichowakasirisheni sana ni yeye kusifia Wakatoliki na Waislamu? Hampendi kuambiwa ukweli waamini wa KKKT?
 
Kanisa sio siasa!ama mtu kutafuta umaarufu

Kwahiyo unataka kusema bila yeye usharika huo,unakufa na hauwezi kuendelea?sio kweli Huwa inafika wakati sharika kukua na hapa nasisitiza bila Baraza la wazee kuamua,kuwa na Nia Moja hakika ni ngumu kuendelea
Achana na wavaa kobazi wamepata kiki, mchukueni kwa mtoro akake na MAZINGE...
 
Alijisahau Sana Hadi kuanza kuwasifu Wakatoliki na Waisalmu hadharani eti ,roma Catholic wako vizuri aende uko sasa...
Sasa kuwasifu Waroma na Waislamu ni kosa? Kwani si ni binaadamu tuu kama sisi. Mbona hizi dini zinavuruga sana wapokeaji kuliko hata waliozileta?
Yaani ww hapo ni Mlutheri kwa kuwa baba na mama yako walikuwa Walutheri na pengine walizaliwa Bara. Ungezaliwa Zanzibar au Pwani ww ungekuwa Muislamu. So dini isikutoe ufahamu jamaa.
 
Usharika hautakufa asilani. Ila hauwezi kuendelea kama sasa. Leo EVENING GLORY haikurushwa Youtube kulikoni?
Loh! kwahiyo unamtafuta Yesu kristo kwa ku-search you tube!!! Rwanda mauaji ya kimbari makanisa yote yalichomwa kwahiyo na Yesu aliungulia humo.... acheni ushamba... injili itabaki kuwa injili si mtu..
 
Back
Top Bottom