IGWE
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 9,578
- 7,774
...ukiulizwa ni vipi Mungu mwenye uwezo wote ,na upendo wote ni kwanini aliumba Ulimwengu kwenye mapungufu hivi...na akamuumba Shetani mpinzani wake utajibu mini.Sawa nimekuelewa.
Katika uzi wako nimeona kuwa sababu kuu ya wao kuumba binadamu ni kutaka binadamu kuwasaidi kukusanya madini ambayo hao wamekuwa wakitumia akili zaidi kutafuta namna ya kuyarejesha madini hayo.
Sasa nauliza.
1.Licha ya akili nyingi walizonazo na tekinolojia yote walishindwa wao kurejesha madini hayo pasina kumuhusisha binadamu ambaye anayatumia madini yao kwa matumizi yake binafsi?
2.Kwanini tekinolojia hiyo haikuanza kwa binadamu wa kwanza ambaye walimuumba na hatimaye kuanza miaka mingi baadaye?
3.Sasa kama binadamu walimuumba awasaidie kukusanya madini yao na wao ndiyo wanamuongoza binadamu iweje wampe akili za kuyatumia madini hayo ambayo hata wao inaonekana wanayaitaji zaidi?
4.Kwanini hawakuumba binadamu kwa wakati mmoja tena kwa idadi waitakayo ili wafanikishe adhima yao ya kukusanya madini kwa muda mfupi yaani wafanye kazi kwa pamoja?
Naomba tusaidiane kueleweshana.
Sent using Jamii Forums mobile app
.....ukinisoma kwenye mistari utaona hoja yako ni sawa na hii ya story za bible na quran
Sent using Jamii Forums mobile app