Kibingu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2022
- 1,078
- 1,445
Pamoja na stori hii ndefu, bado naingiwa na shaka kama kweli uchawi ni kitu halisi. Labda tukubali kuwa uchawi kwa asilimia 99.99% ni propaganda zinazotumika na wajanja wachache kuwalaghai wajinga walio wengi.
Ulaghai huu unatokana na masalia wa wafuasi wa ibilis, pamoja na historia zilizoachwa na mababa wa uchawi, zinazoenezwa kwa njia ya mila, tamaduni, au desturi za kimakabila, kiukoo na hata kifamilia. Tujikumbushe kuwa Ibilis, baada ya kufukuzwa kwenye ufalme wa Mungu, aliamua kuwatumia binadamu kuanzisha himaya yake hapa duniani alipodondokea.
Uchawi wa asili ulitoweshwa duniani baada ya ujio wa Yesu Kristo. Kristo alipotua ulimwenguni, ilikuwa ni pigo kuu kwa shetani, ndiyo maana maandiko yanatuambia kuwa shetani aliandaa joka kubwa limmeze huyo Kristo.
Yesu, alishinda hiyo vita, na mwishowe aliutangaza utawala mpya kisha kumweka kizuizini Ibilis. Baada ya misingi mipya, ndipo nyakati ambazo tawala za kichawi zilianza kuanguka mmoja baada ya mwingine. Huku tawala za Kikristo zikichukua nafasi, mpaka utawala mkuu wa kichawi wa Roma ulipoamua kukubali Kristo atawale, na kuusambaza ukristo dunia nzima.
Yesu pamoja na mambo mengine, kazi kubwa ya ukombozi ilikuwa kumtia kizuizini shetani na kuwafungua baadhi ya mateka waliokuwa wameshikiliwa na ibilis huko kuzimu (wakaitwa mizimu). Mizimu hii ndiyo inatumika mpaka sasa kuendeleza mawasiliano ya kichawi kwa vizazi, mataifa, makabila na koo nyingi, japokuwa nguvu yake rasmi imefungwa huko kuzimu.
Kifungo hiki kitakapokamilishwa, ataachiwa na tutashuhudia tena uchawi dhahiri kwa macho hapa duniani. Watakuja watu, wataonyesha ishara mbalimbali, na watu watawaamini. Ishara hizi zitakuwa ni za kichawi, na wala siyo ishara za kimungu kama itakavyokuwa inadaiwa.
Asante kwa kazi nzuri...