Sijaona tofauti ya ulichokiandika na nilichokiandika, siku zote mawazo yenye hekima kuu hupingwa, ni ubinadamu wetu huu. Nilichokupinga ni suluhisho tu ulilolitoa. Kwamba tuishi kwa kujihami ktk mataifa yetu, kwanza hofu tu ni chanzo kikuu cha maafa.
Nimekwambia hadi sasa hakuna taifa kamili, liitwalo Kenya wala Tanzania nje ya sheria na mipaka na majeshi, dola. Yote ndo kwanza yanajenga misingi yake, nyumba bado kabisa.
Kuna mengi yanayoendelea ktk mataifa haya yanayohatarisha huu utaifa. Tanzania, kuna udini, ukanda, bara na visiwa vyake nk.
Wenye hekima walishayaona haya tangu miaka ya 60, wakahitaji utaifa wa kiafrika. Taifa moja la Afrika. Tutawafukuza wakenya, tukimaliza, wamalawi, wakongo nk. Tukishawamaliza, tutajiuliza kwani sisi ni wamoja? Jibu ni hapana, tutafukuzana wenyewe, JK Nyerere.