Protokali ya Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu ipoje?

Maandishi ndiyo hayako sawa, lkn kwa majukumu wote ni wasoma magazeti tu.
 
Amir Habib Jamal hakuwa mzungu. Alikuwa ni mhindi alizaliwa Mwanza 1921 na kufarikia Vancouver Canada 21 March 1995.
 
Shukrani mkuu, kuna document yiyote tunaweza rejea?
Waraka wa Utumishi no.3 wa mwaka 2002 Ukisomwa pamoja na Kanuni Za kudumu za utumushi wa Umma mwaka marekebisho ya mwaka 2009 (Standing order of Public servants 2009) pamoja na Kanuni za Utumishi wa umma zanzibar za mwaka 2014..

Sheria ya Mfuko wa jamii kwa watumishi wa Umma (Wastaafu) sheria namba 2 ya mwaka 2018 na zingine pia
 

Lowasa alistaafu au alijiuzulu?
 
Vuta subira, muda si mrefu utajua kuhusu protokali.
 
Sikuwa na haja ya kumuandika Nyerere kwa sababu kipindi anakuwa Waziri Mkuu Tanganyika haikuwa Jamhuri ilkuwa ni Jimbo la Uingerez
Nadhani hujui nini maana ya Jamhuri, Tanganyika baada ya Dec 1961 haikuwa chini ya Uingereza otherwise utuambie mpaka leo kwa kuwa ni wanachama wa common wealth bado tuko chini ya Uingereza, nenda kasome upya forms of government..
 
Nadhani hujui nini maana ya Jamhuri, Tanganyika baada ya Dec 1961 haikuwa chini ya Uingereza otherwise utuambie mpaka leo kwa kuwa ni wanachama wa common wealth bado tuko chini ya Uingereza, nenda kasome upya forms of government..
With all Due Respects Sir!
Nafurahi kukuelekeza!

Jamhuri (Republic) a country where power is held by the people or the representatives that they elect. Republics have presidents who are elected, rather than kings or queens...

Serikali ya Jamhuri au Republic Haina Utawala wa Ki-Monarch kwahyo Kiongozi wa Nchi hachaguliwa na Wananchi na sio Watawala..

Maybe kilichokuchanganya Ni Neno Jimbo..
Jimbo Inaweza kutafasiriwa pia kama State (Rejea States of American) pale ambapo Utawala wa States unapokuwa haukp chini ya Raia wa eneo husika..

Nyerere alikabidhiwa Madaraka ya kuongoza State Na Sir Richard Turning kwa Maelekezo ya Queen Elizabeth II kwa kipind hicho..

Utawala wa Kwanza wa Tanganyika mwaka 1961 ulitokana na Azimio La bunge La uingereza na kuundwa kwa Katiba ya Tanganyika ya mwaka 1961 iliyotokana na sheria ya uhuru (Order in Council) liliyopitishwa katika bunge la Uingereza na kuletwa Tanganyika kama Katiba ya awali.

Katiba hii ndio iliyoweka Tanganyika Ikiwa Bado Chini ya Utawala wa Mwingereza kama uliwahi kusikia neno linalosemwa sana Kwamba Tanganyika ilipata Uhuru wa Bendera mpaka mwaka 1962 ndo ilipata Uhuru kamili sasa hiyo ndiyo maana yake..

Tuendelee;-

Mambo mengi bado yalitegemea kufanyiwa maamuzi toka Uingereza chini ya Malkia ambaye aliendelea kuwa mkuu wa nchi ya Tanganyika mpaka mwaka 1962, Na waziri wake Mkuu akiwa JK.Nyerere
Baraza la mawaziri lote Pamoja na Waziri Mkuu akiwemo Nyerere na waziri mmojammoja waliwajibika kwa bunge (Kipindi Hicho Lilikuwa Bunge la Tanganyika lililokuwa na wawakilishi 70 pamoja na Bunge la Uingereza)..

Sasa mwaka 1962, Wabunge 71 wa TANU, Walijigeuza na Kuwa Bunge maalumu La Katiba na wakatunga katiba Mpya ya mwaka 1962..
Na kwa mujibu wa Katiba hiyo wakajipa Rasmi madaraka ya Ujamhuri kwahiyo Uteuzi wa kiongozi ukawa Rasmi Mikononi mwa wananchi tena..

Na Nchi ikaondoka kuwa nchi ya Kimonarch...

Katiba ya 1962 ndiyo ilianzisha mfumo wa Urais ambaye pia alikuwa Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa serikali.
Baraza la Mawaziri na waziri mmojammoja sasa waliwajibika kwa Rais badala ya bunge (Bunge la Tanganyika na Bunge la Uingereza)..

Sijui kama Umenielewa mpaka hapo?

Commonwealth Haina madaraka Ya kiutawala dhidi ya nchi wanachama sijui kama unalifahamu hilo?
 
5.Edward Moringe Sokoine (1983–1984)
6. Salim Ahmed Salim (1984–1985)
 
Mbona hujamuweka Nyerere?
 
What an Embicile!..
 
Tulia na acha kukurupuka!
Unapotaka kujua kitu kwanza wewe mwenyewe shughulisha bichwa lako Hilo na uache kuchosha watu!
Mawaziri Wakuuu tuliowahi kuwa nao ambao sasa wametangulia mbele za haki ni Hayati Julius K.Nyerere, Hayati Edward Moringe Sokoine na Hayati Rashid Mfaume Kawawa.
Itifaki ya mazishi ya mtu inahusisha mambo mengi ya ikiwemo wosia wa Marehemu, Dini, Cheo, jinsia n.k.
 
Sema nimesahau kuandika mwaka vizuri lakini nahisi kati ya mwaka 83 mpaka 85 alikuwa waziri asiye na wizara maalumu maana yake alikuwa waziri mkuu Na aliweza kufanya kazi wizara yoyote
Mkuu, kuwa waziri asiye na Wizara maalumu haimufanyi awe Waziri Mkuu.

Ukweli ni kuwa Jamal hakuwahi kuwa Waziri Mkuu. Hicho kipindi unachokitaja ya kati ya 83 na 85 Mawaziri Wakuu walikuwa ni Sokoine na Salim.
 
Sokoine hakuwa Waziri mkuu kuanzia mwaka 1972.

Nafikiri alikuwa Waziri Mkuu mwaka 1978 - 1980 then 1983 - 1984. Check your facts.

Pia Jamal hakuwahi kuwa Waziri Mkuu kwa kipindi chochote ....!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…