PSSSF Dodoma mama yangu akifa kwa uzembe wa staff wenu hakika jiandaeni kupokea maiti ofisini

PSSSF Dodoma mama yangu akifa kwa uzembe wa staff wenu hakika jiandaeni kupokea maiti ofisini

babajeska

Senior Member
Joined
Aug 22, 2016
Posts
148
Reaction score
182
Mimi ni mwanachacha wa mfuko wa psssf namba ya uanachama 110---652 ambaye nilipoteza ajira tangu may 2023, mwaka huu mwezi wa kwanza mama yangu alipata changamoto ya maradhi ya moyo baada ya nyumba yetu kudondoka kutokana na mvua kubwa zilizonyesha ilipelekea akapooza, kwakuwa mimi ni kijana mkubwa nyumbani na hadi sasa sijapata kazi gharama za kumtibu mama zikanielemea hivyo nikaamua nifatilie utaratibu wa fao la kukosa ajira ili nitakachopata kinisaidie kumhudumia mzazi wangu pamoja na marekebisho ya nyumba japo chumba kimoja.

Nilienda ofisi za PSSSF kinondoni walinipa utaratibu wote nikaufata na mwisho mwajili wangu wa mwisho alisubmit fomu zangu ili zifanyiwe kazi kama utaratibu unavyotaka. Mchakato ulienda vizuri hadi kwenye hatua ya malipo ndo tatizo lilipoanzia.fao la kukosa ajira hulipwa kwa mwanachama kuwekwa kwenye payroll ambapo jina langu liliwekwa lakini jina la bank halikuwa sahihi nililoandika(natumia DCB BANK ila psssf walipeleka DTB BANK) nikafatilia psssf kinondoni wakawasiliana na dodoma ambao ndo huandaa hiyo payroll majibu ya staff wa dodoma anayeitwa Haika yalipoteza tumaini la kupata haki yangu,Haika alisema namnukuu"nikweli nimekosea kwenye kuselect bank name badala ya DCB niliweka DTB kwahiyo atalipwa mwezi ujao JUNE"

Naomba nikuulize Haika na psssf dodoma kwa ujumla 1. huo mwezi ujao ukikosea tena badala ya DCB ukaweka TCB (Tanzania commercial bank) inamaana nitasubili hadi july? Na ikifika July ukakosea ukaweka MCB (mwalimu commercial bank)nitalajie august?hizo danadana si mwaka utaisha?

2. Mshatesa wangapi kwa uzembe wa kutokuwa makini wakati wa kufanya kazi maana document zote zinaambatanishwa ni wajibu wenu tu kuhakiki unachofanya na document zilizowekwa?

3. Je, Mkuu wako wa idara baada ya wewe kuandaa hizo boko zako naye huziapprove nzima nzima bila kufanya countercheck?

4. Kuna wakosa ajira wangapi wanaopigwa danadana kulipwa miezi na miezi wakiambiwa mchakato haujakamilika kumbe uzembe wenu unawaghalimu?

NB: Kwa majibu ya niliyojibiwa najua sina tumaini jingine la kupigania afya ya mama yangu zaidi ya kusubili muujiza maana dawa anazotumia sitaweza kumudu najua huo mwezi hatafika hivyo nitawaleteeni maiti yake mkae nayo ili mioyo yenu ifurahi matokeo ya mateso mnayotupa wanyonge tusio nawatu wakutusimamia.

MREJESHO:
Nimetafutwa na meneja wa pensheni PSSSF namshukuru kaniahidi kulitatua tatizo langu haraka.

Huduma mbovu ya watumishi wa ngazi za chini sio huduma ya wakubwa wao.Tatizo langu nnahakika lilikuwa linaweza kutatuliwa bila ata kulileta huku na kusumbua watu.

NAKUSHUKURU SANA MENEJA

NB: JAMII FORUMS NI SAUTI YA WASIO NA SAUTI

1716843374486.png
 
Nimeambiwa nisubili mwezi mzima
Nchi yetu ina janga la watu kutokuwa makini kwa mambo yote halafu ukiwaambia wanakuwa wabishi kweli kweli. Hili la kukosea jina, jinsia au mambo kama ya huyo aliyekosea benki ni jambo la kawaida sana na itashangaza kama fomu yoyote itapita bila kuwa na kosa. Siyo hivyo tu hata kuandika nako ni shida! Na wewe uko kwenye hilo hilo fungu. Sasa ''kusubili'' ndiyo nini? Anyways, pole ila huyo mwanamke aliyekufanyia hivyo ni kuwapeleka mahakamani kwa sababu hajali.
 
Hii Nchi Mtu Akiwa Ofisini Anasahau Yote Mtu Anasaga Soli Ya Kiatu Kama Mkimbizi
Mlioko Ofisini Tendeni Haki Pia Lazima Mjue Mtapisha Siku Moja Nanyi Mtasumbuliwa
 
Pole Sana Mwalimu kwa kweli kuna watu, hawajali wenzao kabisa, kuna wengi ambao wameajirwa kwa vimemo ni SHIDA kwenye maeneo ya HUDUMA.
 
Hii ndio Tanganyika ya KIZIMKAZI. Hakuna anae jali kabisaa. Hapo niko na 100% wanataka rushwa tu.


KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom