Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?


Pasco ww ni maarufu humu jamvini kuliko mii ambaye huja nadra lakini nimekusoma sana. sasa kwa upande wangu nijiona kuwa naaminika sana watu waliojenga ukaribu na mimi wote hutokea kuniamini na kushangaa uwezo wangu katika masuala kdhaa. ikitokea mfano nikazoeana na mdada katika mahusiano ya kawaida itakuwa vigumu kuacha mawasiliano. tatizo mi si msemaji sana na mwoga kutongoza. ajabu wanawake niliowapata huko nyuma ni wale tu tuliozoeana au waliojikaribisha hata nikagundua la sivyo mahusiano ni ya kawaida kabisa hadi wakati mwingi nililaumiwa sana.
Sasa Pasko kwa kuanzia ninaweza kuwa na power gani. zaidi niseme kuwa nina uwezo wa kusoma kwa mda mrefu bila kuchoka kwa hivo karibu nusu ya siku hutumia kusoma vitu mbalimbali. je hii itanipoteza au inasaidia nini ukihusisha na haya?
 
Mkuu Mzamifu, huo uwezo tuu wa kusoma, peke yake ni powers tosha, kila mtu anazo nguvu hizi tatizo ni kutojitambua!. Kwa vile uwezo wake ni kwenye kusoma, then, take your time, pitia hizo links, hivyo vyote ni vitabu jisomee tuu for leisure, until when you are ready, utafunuliwa!.
Pasco.
 

Fake fake fake....upotoshaji mkubwa.
 

Samahani Mkuu, sasa kwa Upande wa Yesu yeye alitenda haya mambo kwa kutumia nguvu zake ambazo alizaliwa nazo ama?
 

Unasali wapi Mkuu?
 

Mwanzo wa Mungu ni sawasawa na wa Shetani!!?? Unasomaga maandiko? Maandiko gani yanayosema hivi?
 

Japo wengi wanakupinga ila unaongea kwa hoja nzuri sana. MUNGU akutie Nguvu kwa kweli.
 

Sina muda nawe, najikita kwenye mada ya Pasco.
Bye.
 
Last edited by a moderator:

shetani ni nani?
 
shetani ni nani?

Ni kiumbe kama wewe mwenye nguvu tofauti na wewe!
Wewe unanguvu ambazo yeye hana!
Na yeye ananguvu ambazo wewe huna!
Ukiniuliza nimejuaje!
Jibu langu ni kuwa nimesoma elimu ambayo wewe pia unaweza kuipata na ukatumia ubongo ulionao (kama upo)
Ku analyse kama ni kweli au si kweli!!
 

Swadakta kaka Hayo ndo majibu Kwa maswali yasio maana
 
Hii mada mbona inavurugwa mwenye mawazo ya kidini aende kwenye jamvi la dini hapa tunataka elimu jitu hata bibilia halifungui lakini linaleta ubishi wewe vipi. Sasa wacha tupate Mada hii tufumgue akili wengine humu ni wavivu wa kusoma vitabu hapa tunapata vitabu vingi Vikiwa analysed.
 

Maneno meeeengi! Utumbo mtupu!

Yaani hizi stori za watoto ndio unaziita "kujitoa muhanga"!!
Kama unauwezo wa kujua mtu muongo si ukaombe kazi mahakamani! Tuone utakamatisha vibaka wangapi! Na wabakaji wangapi!

Unasema unauwezo wa kupata utakayo!
Hebu amua kuwa rais au waziri na hizo nguvu zako! Saana lbd balozi wa nyumba kumi!
Digrii mke na gari ndani ya mwaka mmoja! Hio degree ya kufuga bata!!

Au huyo mkuu wa chuo alikuwa mtoto wa mjomba wako!!

Unasema pia "wenye nguvu ndio watakao uona ufalme wa mungu! Halafu unasema kila mtu ana nguvu! Kwa maana hio kila mtu ataingia ktk ufalme wa mungu!!?

Wale mapadri wanaobaka watoto!.wale makatikista wanao oana, na waliberali woote waingie peponi??

Halafu uwezo wako wa kuchukua machangudoa mitaani unauita NEEMA YA MUNGU!?
Yaani uzinifu wako Mungu ndio amekupa huo uwezo!? We huna adabu kwa Mungu sio! Au mpaka uondoke na ukimwi ndio utamthamini Mungu!! Na kumuheshimu!?

Au mkuu wakati unaandika haya ulishavuta ile maneno!!

Kwa sababu hizi stori saana utazikuta.kwa wavuta bangi! Tena ile bangi mbichi!!

Mtu anajiona yeye superman! Lkn ukimpa moja ya uso. Anakimbia kama kaumwa nyuki!!

Hebu rudi hapa na akili timamu uandike tena!

Hizo ganja ukichanganya na kubeli! Unaweza kuja kumtongoza mkeo bure! Wakati unae kila siku.
Cc faby Tayeb
 
Last edited by a moderator:

Una tatizo la kusoma na ukaelewa

Mkuu Nyenyere anakuambia kuwa kitendo chako cha kumtaja Kisto na kulinganisha nguvu zake na za wachawi pia kuitaja biblia moja kwa moja

Hapo ndipo tatizo lilipoanzia na ni hapo sisi tukaja kukukosoa na kuonesha nma ulivyokosea

Unadai kuwa unafundisha kuhusiana na power ambazo hata husemi zinatoka wapi,lakini ulishindwa nini kufundisha hizo power zako bila kuwataja Roho mtakatifu,Yesu na biblia?
Ulishindwa nini kujenga hoja kivyako?
Au ulikuwa unatafuta tention kutoka kwa wasomaji?

Hizo meditationa unazodai zipo miaka mingi na sijui kitu gani,sisi hatuna tatizo na hilo, tatizo linakuja pale ulipotamka Roho mtakatifu na Yesu pamoja na biblia.Ungekuwa umesema tu Mungu kusingekuwa na tatizo maana kuna wengi wanaabudu mawe na wanayaita Mungu,hata Hsetani nae anaitwa hivyo na wafuasi wake na tusingekuwa na tatizo

Tatizo linakuja kwenye mambo mawili,Biblia na Roho mtakatifu
Hao huwezi kuwapata kwenye imani yoyote ile tofauti na biblia,kwenye Yesu wapo watu wengine wana yesu wao lakini ulipoitaja biblia hiyo inamaana kuwa unamtaja Yesu wa kwenye biblia na ndipo tulipata jukumu la kukukosoa na mafundisho yako ya kishetani[samahani kwa kutumia lugha kali] na tumekuonesha ni namna gani ni ya kishetani

Mtu unasema shetani hakuumbwa na Mungu na hana mwanzo wala mwisho.unadhani hayo sio mafundisho ya kishetani na ni kwanini usiitwe mpinga Kristo?

Halafu hao wengine unaodai tunawaingilia sijui ni wakina nani,ni nani anamwabudu Roho mtakatifu tofauti na wakristo?Ni nani anamwabudu Yesu Kristo wa Biblia tofauti na wakristo?
Hao wengine unaodai ni wakina nani?

Suala hili la hizi power tunakushauri u edit mada yako iwe huru ili wote wanaochangia wasichangie wa mitazamo ya kidini
Kama ni kosa limefanywa kwa watu kuchangia kwa mtazamo wa kidini kosa hilo umelianzisha wewe mwenyewe kwenye post yako

Tafadhali sana Invisible hebu fanyeni haki kwetu yunaemwabudu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu!
 
Last edited by a moderator:

Halafu mi nauliza! Vipi huyu Pasco ajiite mkristo hali ya kuwa anamlinganisha yesu na mchawi??

Hii si laana hii?? Anasema yeye ni mkatoliki!
Hivi ndivyo wanavyofunzwa na papa!?

Kumfanya nabii wa Mungu kama shemeji yako??

Ama.mtoto wewe huna adabu!

Laiti ningemjua baba Pasco ! Ningeenda mchapa kofi kwa kutokufundisha nidhamu!
Yaani mi nilidhani Nicholas na Matola ndio hawana adabu lkn wewe mwisho!

Mfnssssssssssss!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…