Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?


Hoja ni kwamba akijibiwa analalamika tunaleta udini, wakati yeye hafundishi dini. Ni mwepesi sana kusukumia hoja zipelekwe jukwaa la dini ili yeye aendelee kupotosha maandiko hapa. Hicho ndicho nilicho maanisha. Hataki majibu hapa kwenye hii thread.
 
Mkuu Aleyn, uko very right kuhusu Mungu, limits za vitabu vyote vya Kikristu ni Mungu ni Alfa na Omega!, Mwanzo na Mwisho!, Wakristu haturuhusiwi kuhoji mwanzo wa Mungu.

  1. Naomba jambo moja la msingi tukubaliane kuhusu Mungu, kuwa, Mungu ni Alfa na Omega, alikuwepo, yupo na ataendelea kuwepo!. Jee unaijua foam of God?, yaani Mungu ni wa Namna gani?, nyama, kiumbe, mtu, or what?!. Kwenye maandiko matakatifu ameelezewa sana tuu ila hajawahi kutajwa!. sasa somo la kwanza kwa kukusaidia wewe na wengine, ni kuwa God is Power!, huwezi kumuona, unaweza tuu kuisikia sauti!. Hiyo Sauti ya Mungu, inaitwa "Voices from Within!", ili uisikie, unahitaji utulivu wa hali ya juu, na meditation ni moja ya njia za kutulia na kuzungumza na Mungu Direct!. Usikute wale wazungumzao na wengine kunena kwa lugha huku wakipiga makelele wa`kijiaminisha ndio wamepandwa Roho Mtakatifu!, usikute wala sio Roho Mtakatifu, bali wamepandwa mashetani aliyejidisguise kama Mungu!. Ili kumjua Mungu wa Kweli, ni lazima uisikilize sauti from within, "inner voice!", vinginevyo...
  2. Jambo la pili ambalo tukubaliane, kuwa kwa vile God is Power, miongoni mwa nguvu yake kubwa ni kuwa ni omnipotent, hawezi kufa, na omnipresent, yupo popote!. Hivyo popote ulipo, Mungu yupo!.
  3. La tatu, tukubaliane kuwa Mungu alituumba kwa mfano wake!. Kama Mungu ni Power, mfano wa Mungu kwetu ni powers!, sio haya maumbo ya kibinaadamu. Ikumbukwe, ulipotuumba, alifinyanga tuu udongo, transfer of powers toka kwa Mungu kuja kwa binadamu ni pale alipotupulizia pumzi ya uzima!, zawadi ya life!, hivyo life ndio zawadi ya Mungu kwa binadamu!. Life ni uzima!, ukiwa hai, una Mungu ndani yako, wengi wanaita Roho!, hiyo Roho, ndio Roho Mtakatifu wa Kweli!. Ukikata Roho, kinachofanyika ni ule uwepo wa Mungu ndani ya Binadamu unakuwa umeondoka, kinachobaki ni mwili, zile process za mazishi na kupamba mwili, kuuvisha vizuri, kuuweka kwenye jeneza zuri, kuuzika kwenye kaburi zuri, kulipamba maua na baadae kulijengea, ni kujifurahisha tuu nafsi, mwisho wa siku hio mwili bila Roho ni nothing!, sipendi kuwaambia kinachoutokea miili ya wapendwa wenu baada ya kuizika!.
  4. Sisi binadamu ni mwili na roho, body and soul, phyical bpdy and spiritual body, hiyo roho, soul na spirit, ndizo nguvu za Mungu ndani yetu!. Kwa vile Mungu ametuumba kwa mfano wake, ametupa nguvu hozo ndani yetu!. Kama alivyo Mungu, ni amnipotent na omnipresent, vivyo hivyo roho zetu, souls zetu na spiritual body zetu ni omnipotent na omnipresent!. Kwenye ulimwengu huu wa mwili, ndiko kwenye principles za physics za distance, time na mass, kwenye ulimwengu wa roho, "spiritual world", hakuna mass, distance wala time!, hivyo ukiwa kwenye spiritual, you can be Dar es Salaam, London, New York in a split of a second!, hiyo ni omnipresence ya uwezo wa Mungu ulio ndani yetu!. Tukija kwenye miili yetu, ukifa kinachokufa ni mwili tuu, roho haifi! hivyo roho zetu ni omnipotent hazifi na zinaishi milele!.
  5. Tukiisha kubaliana hayo, sasa tumrudie kodogo shetani!, kwanza tukubaliane kuwa shetani kabla ya kuwa shetani, ndie aliyekuwa malaika mkuu mwenye mamlaka second to God!. Kama alivyo Mungu, shetani nae pia ni omnipresent na haikuandikwa popote kuwa Mungu alimuumba shetani, na alipoasi haikuandikwa kama alinyang'anywa mamlaka!.
  6. Baada ya Mungu kumuumba binadamu kwa mfano wake, shetani ameweka nadhiri ya kumuangamiza binadamu na kwa kutumia nguvu zake za kishetani, alimdanganya Eva akamuasi Mungu kwa kutenda ile dhambi ya asili, hivyo binadamu wote tunazaliwa kwa tendo lile la dhambi ya asili, mtu pekee aliyekingiwa dhambi ya asili ni Bikira Maria kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, bila lile tendo!, akamzaa Yesu!, hivyo Yesu hakuzaliwa kwa asili ya dhambi ndio maana anaitwa Mwana wa Mungu, aliyetoka kwa Mungu mwenyewe, kupitia kwa Bikira Maria, akawa Mwadamu!. Hivyo aliyetuletea dhambi ya asili ni shetani na dhambi zote zinafanywa kwa nguvu za shetani wakati mema yote yanafanya kwa nguvu za Mungu!.
Nawaomba sana nyie wabishani wote kuhusu Mungu na shetani, tuhamishie mjadala kule jukwaa la dini tukamalizane kule, huu uzi ni wa jinsi ya kujitambua kuwa you have the powers na kuzitumia kujiletea maendeleo!, hapa sio nyumba ya ibada na wala mimi Pasco wa jf sio Padri Paskali yule wa kwenye kitabu cha Bulicheka!.
Pasco.
 
Hoja ni kwamba akijibiwa analalamika tunaleta udini, wakati yeye hafundishi dini. Ni mwepesi sana kusukumia hoja zipelekwe jukwaa la dini ili yeye aendelee kupotosha maandiko hapa. Hicho ndicho nilicho maanisha. Hataki majibu hapa kwenye hii thread.
mbona najibu kila kitu hapa hapa, ila nasisitiza tuykutanie kule ili tujimwage kwa nafasi na uhuru na nitakushushia hadi mistari!.

Mimi mwenzako Bibilia Takatifu nimeisoma mstari kwa mstari tangu page 1, hadi last page na sio mara moja!.
Tena sio version moja, nimesoma hadi Apocalpa Deutrocanonical Books ambazo wengine hawavitambui, hadi Vatican nimefika na kwenye underground ya St Peters Basilica, ndiko kwenye maktaba kubwa kabisa ya Katoliki, walipo loot lile hekalu la Constitantino Pole na kujenga Vatican, walihamisha hazina yote, the good, the bad and the evil!, na wamehifadhi humo!. Huu sio uwanja wa hayo, tukutane nikufunulie, usijejikuta uko kwenye zile ibada za the beast na 666 bila kujijua!. Ujue ukweli, ni ukweli tuu ndio utakuweka huru!.

Be open minded kuhusu powers, zimekuwepo since time immemorial, Hindu wako miaka 300,000 kabla ya Kristu na wamezitumia!. Kristu kaja, amezitumia na kutufundisha ni "imani yako ndio inakuponya!", sasa wewe unapinga nini?!. Unadhani hizo nguvu ndio zinaletwa kwa kulitaja Jina la Yesu!, no!, Kulitaja jina la Yesu ni ufunguo wa imani inayofungua hizo nguvu zilizo ndani yako kutenda miujiza!, nguvu tayari zipo, tulipewa siku tunaumbwa, na zinachukuliwa siku tunakufa!.
Pasco.
 
Kutokuijua kwako Bible kusikufanye uongee na uongo!
Mungu Ndio muumbaji Wa vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani na vinavyoonekana na visivyooneka!
Sasa Kusema Mungu hakuwaumba malaika huo ni Ukengeufu mkubwa!
Mkuu Eiyer amekupa mafungu ya Wakolosai 1:16-17.

Futa kauli yako ya Kusema huyo shetani wako hakuumbwa na Mungu na ndo maana unajaribu kumlinganisha na Mungu!
 

1. Mkuu Pasco umeonesha kuwa hauna Ufahamu juu ya Mungu aliehai ila Ufahamu juu ya Shetani unao. Wewe Unasema Mungu ni Power, sasa msikilize Yesu alietoka Mbinguni anasemaje ktk Yohana 4:24 'Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli'. Upo hapo???

2. Umesema ukiwa hai una roho na hiyo roho ndio Roho Mtakatifu. Mkuu Pasco, bado una elimu changa sana. Nakukatalia katakata kwasababu Yesu alisema 'Kilichozaliwa kwa Roho ni Roho na kilichozaliwa kwa mwili ni mwili. Mbona Yesu hakupokea nguvu ya Roho Mtakatifu mpaka alipobatizwa??? Ina maana Yesu hakuwa na Roho tangu alipozaliwa na kuwa nafsi hai??? Yesu akurehe
 

Asante kwa majibu yako kwa swali nililokuuliza.Nimekuelewa
 
Twenda jukwaa la dini tukamalizane kule!, alijarabiwa Mwana mwenyewe wa Adamu, nitakuwa mimi Pasco wa jf!, bahati nzuri niko enlightened kidogo, shetani hata akijifanya ni mtumishi wa Mungu, ati anaijua sana Bibilia, kwangu namshutukia!, na nawawahikikishia wote wausomai uzi huu, mwisho wa siku shetani atashindwa!, tutazifungua powers tulizopewa bure na Mungu na tutazitumia!.
Pasco.
 

Marko 16:17-18 'Na Ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
We mbona unapingana na maandiko?
 

Kweli Wakatoriki wamepata Hasara kupata muumini kama huyu.
 
Haya mambo ya kuikariri Biblia kikasuku tuu, tumeisha bishana na na kina Max Shimba kule jukwaa la dini, hadi mada za "dhambi ya sili ni nini haswa, nimeishaijibu sana kule!, hapa sii mahala pake, tukutanie kule, tuwekane sana, tumamalizane kwa vifungu!,

Kwa kukusaidia tuu, naomba nikutip, kuna watu walikuwa wakitokewa na visions za Yesu, wakiamimi huyo ni Yesu, kumbe ni shetani!, Twende kule nitakusaidia sana kukufunua, kama na wewe ni mmoja wao unaotumiwa bila kujijua, utapata mwanga na utaondoka kwenye bondage ya mfalme wa dunia hii!.
Tenzrtu kule!.
Pasco.
 
Japo siukumbuki mstari, Bwana Yesu ametufundisha, watakuja watu, watafanya ishara, watatoa mapepo kwa jina lake yaani "Kwa jina Yesu Zishindwe!", kumbe sio wake!, na ametueleza pia namna ya kuwatambua!, tukutane kule, tutambulishane, tukusaidie kuwatambua msiendelee kupotea!.
Pasco.
 

Kaka Pasco,

Nadhani na wewe unatoka nje ya huu uzi uliouanzisha,
kuna vitu vingi vinakorogana kwenye huu uzi kiasi kwamba unapoteza matiki yake halisi,
kuna maswali mengi mazuri sana na hoja nzuri sana khasa kwenye mambo yanayohusu dini hasa (Christianity)

Ombi langu ni hili kwa Pasco, naomba ufungue uzi kule Jukwaa la DINI kwa hizi mada na please uwaalike wote wenye uhitaji wa kujuzana. Ni ukweli usiopingika kuwa waamini wengi wanaabudu wasichokijua na kwa kiasi kikubwa kuna uelewa finyu wa maandiko na ndio kisa cha kila siku kuwa na madhehebu yasiyo na Idadi,

Please Pasco Fungua UZi kule

CC: Nyenyere, ALEYN, Ntuzu, @Aiyer
 
Last edited by a moderator:

Hapo sasa tumekuelewa kuwa mnafanya hivi lakini mkijijua kuwa ni Wapinga Kristo na mnatumia nguvu za Giza kutenda miujiza huku mkilitaja Jina la Yesu.
 

Tunachokitaka ktk Thread hii alioanzisha asiuungize Ukristo hususani anapomtaja Yesu mbaya zaidi kumkashifu hata Roho Mtakatifu. Arekebishe Thread yake na sisi tutatoka.
 
Last edited by a moderator:
Kwa Mimi nilivyo muelewa Huyu ndugu ni kwamba anapingana na makanisa ya kiroho na hao wachungaji wanaodai kua wako na nguvu za Miujiza na atimae wanajipigia pesa/sadaka kwa ujanja kwa kuzitambua Hizo nguvu ambazo Yeye anadai kila mtu anazo isipokua ni kujitambua tu Ndio kunakoitajika.

Kosa Analofanya ni kuweka neno la Mungu kwa mafundisho yake machafu na ata uelewa wake Wa maandiko Uko chini.

Makanisa ya kiroho yamekua mwiba sana kwa makanisa makongwe na ya siku nyingi Kama RC. Yanapata waumini kibao na kuyaacha makanisa kongwe na waumini wachache!
Kwa hiyo Huyu ndugu yetu dhumuni lake Ndio Hilo ni kuuaminisha umma kua Hizo nguvu za kufanya makubwa kila mtu anamiliki. Ila kosa lake ni kuchanganya mafungu Au kutumia maandiko kwa maana anazojua Yeye!
 

Hichi ndicho anachopingana nacho. Hii Miujiza.

Na Yeye ni mfuasi Wa Yule mnyama Wa 4 na ile Pembe ndogo katika kitabu cha Daniel 7:

Na ata Ile Danieli 8 na 9. Inamzungumzia vizuri sana Huyu ndugu yetu!
 

Hii nimejifunza kutoka kwako leo. Haya maswali ni ya kawaida kabisa kwa kila mwenye kutaka kufahamu YHWY ni nani. Wala sijapata kusikia katazo lolote juu ya hilo.


Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, kulikuwepo na Powers, hizo powers ndizo Mungu. Hana mwanzo, hana mwisho, yeye ni Alfa na Omega!.

Hapo umechukua sifa za YHWY ukaziita powers. Halafu umekiri ndiye Mungu. Hapo tuko pamoja.


Ndugu yangu Pasco, huyu shetani hana sifa za Mungu kama unavyodhani. Sifa kuu za Mungu ni Omniscience, Omnipotence na Omnipresence. Au kwa lugha nyepesi All-knowing (Anajua yote-yaliyopita, yaliyopo na yajayo), All-powerful (Ana nguvu juu ya vyote) na All-presnt (Yuko mahali pote, wakati wote). Shetani hana sifa hizi hata kidogo. Ni rahisi kudhani kuwa shetani yuko kila mahali, lakini ukweli ni kuwa hutumia majeshi ya mapepo (malaika walioasi pamoja naye) kufuatilia maisha ya wanadamu. Lucifer alikuwa Kerubi "afunikaye" kwa maana kwamba alikuwa akihudumu kwenye kiti cha enzi. Alikuwa ndiye mkuu wa malaika wote huko mbinguni na sio kwamba alikuwa sawa na Mungu. Aliumbwa katika uzuri kuliko kiumbe chochote kile. Ezekieli 28:13-15


Hakuna mahali popote palipoelezwa Mungu aliwaumba hawa malaika akiwemo Luciferi!. Hivyo mwanza wa Mungu ndio mwanzo wa Malaika!

Katika hili umepotoka ndugu. Mwanzo wa Mungu hauwezi kuwa sawa na mwanzo wa malaika, tena kwa kuzingatia andishi lako mwenyewe! Hindi ndicho ulichoandika hapo mwanzo kabisa:

"
Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, kulikuwepo na Powers, hizo powers ndizo Mungu. Hana mwanzo, hana mwisho, yeye ni Alfa na Omega!"

Sasa huo mwanzo sawa na malaika unatoka wapi? Tayari mkuu Eiyer ameshakupatia vifungu vinavyoonyesha kuwa Mungu aliumba malaika.Tena kwa vile unakiri kuwa shetani ni malaika, basi tutumie nukuu ya kuumbwa kwake kama ushahidi kuwa malaika waliumbwa;

Ezekieli 28
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.

Na kazi za malaika zinaelezwa hapa: Waebrania 1:
13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?
14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?


Shetani hakunnyang'anywa hizo nguvu alizokuwa nazo. Ila nguvu zake zina mpaka, na ndio maana hawezi kuzuia mapenzi ya Mungu (will). Malaika mkuu ni Mikaeli na ndiye aliyeongoza mapambano mbinguni.

Ufunuo 12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.



Shetani aliumbwa kama malaika mtakatifu (haikusema aliumbwa na nani),

Biblia ni kitabu kitakatifu cha Mungu. UUmbaji unaoongelewa humo ni wa YHWY, sasa sijui unakusudia kuna vilivyoumbwa na Mungu mwingine zaidi ya huyo ambaye Biblia inamzungumzia? Au aliumbwa na powers? Sijakuelewa hapo katika flow ya logic. Kwani Biblia inasema vitu vyote vinavyoonekana na vieivyoonekana viliumbwa na nani?



Shetani alikuwa na pride, alikiona yeye na bora na anaweza kuwa Mungu. Hii dhambi imeendelea kututafuna hata sisi. Na hiki ndicho hasa unachokifanya wewe Pasco kuwaambia watu wanazo powers za kuona ulimwengu mwingine. Hiki ndicho alichoifanya shetani kujaribu kuiacha asili yake na kutaka uungu. Nitaeleza zaidi nitakapoanza kuichambua mada yako kama ilivyo na asili yake.



Ndiyo astral plane hiyo kaka, mnakokwenda kiroho kutafuta "powers." Huko ndio mnakutana na ascended masters na spiritual entinties wengine ambao ni mapepo yadanganyayo. Nitafafanua...


Hapo kwenye red unakusudia kuwa shetani kamu-overtake Mungu? Biblia inasema alijaribu kujiinua, akatupwa mpaka chini na nafasi yake haikuonekana tena mbinguni. Sasa huku kudanganya watu ndiyo kujiinua juu ya Mungu? Ina maana ameshafanya mapinduzi tayari?

Ni kweli shetani yuko nyuma ya dini zote za uongo, hata nafsi zinazojiinua juu ya elimu ya Mungu. Na anachofanya shetani daima ni kulishambulia Neno la Mungu ili kuwaondoa watu katika mafundisho sahihi, kwa kuwapa elimu mpya mpya huku akiwaondoa kwa Mungu.



Baada ya kuufahamu ukweli huo, wewe je, unauishi? Je, ndicho unachofundisha hapa? Pia ukiwa mkatoliki die hard, niambie kama unaamini katika agano jipya. Nikijua hapo itakuwa rahisi zaidi kukujibu, kwani tangu mwanzo sioni kama unammchukulia Yesu Kristo seriously.


Mungu alipotuumba alitupulizia pumzi ya uhai. Hiyo ndiyo sura ya Mungu. Maskini, tajiri, kichaa n.k. wote hufa vilevile Mhubiri 3: Asili ya nguvu zetu ni ulimwengu usioonekana, ulimwengu wa roho. Mungu ni Roho, shrtani naye ni roho. Tunapokea mawasiliano ya nguvu za kiroho toka mojawapo ya vyanzo hivyo. Ama shetani, ama Mungu. Naishia hapa kwanza nitandelea jioni.....................
 
Last edited by a moderator:

Mkuu umemueleza ukweli.
Ni kazi kwake kurekebisha hoja zake na ule uongo wake!
Eti anasema haturuhusiwi kuhoji?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kituko, nimekusikia na nimekuelewa,
Wakuu yenyere, ALEYN, Ntuzu, @Aiye na wengine wenye muono wa dini kwenye hili, tuhamishieni majeshi kule jukwaa la dini, tukamalizane kule, hapa tuwaachie wanaotaka kufunguliwa powers from within, zifunguliwe watu walambe bingo, maisha yaendelee!.
Asante kwa ushauri.
Pasco
 

Jibu hoja za wadau sio utuambie tuhame Huku then tukuache Wewe unaendelea na mafundisho yako yasiofaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…