Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Kama mkristu akiamua kusoma uislamu ni sawa,mwislamu kusoma hinduism ni uamuzi wake binafsi,kwa nini kulazimishana kufungiana kwenye box?

Hakuna aliyezuia mtu yeyote kusoma mafundisho yoyote, hata kama ni uchawi. Tatizo litaanza pale tu utakapojaribu kutumia maandiko yake kutoa tafsiri potofu. Kama unaona sisi ni wakorofi, jaribu kuhubiri uislamu tofauti na wao wanavyofundisha, halafu njoo na hiyo logic yako uone moto wake.
 



Kweli Mkuu ajaribu kufundisha huo upande Wa wenzetu kwa mafundisho Yake tofauti na wao aone moto.
 

Mbona maswali haupendi kujibu?
 
Tatizo huyu jamaa anajibu maswali kutokana na kichwa chake kinavyomtuma, kama yeye anakiri kuwa ni Mkristo kwanini apingane na Biblia?

Kuna maswali nimemuuliza kuhusu tunda walilokua wazazi wetu Wa kwanza Adam na Hawa.

Na pia kuzaliwa kwa Yesu bila mama Yake kuingiliwa.

Biblia Yake na kwa fasiri Yake tunda walilokula si tunda toka kwenye mti Kama bibilia inavyosema.

Na kutokana na Hilo tunda walilokula Adam na Hawa Ndio maana Yesu akazaliwa na mama yake bila kuingiliwa Na mwanamke. Eti kwa kukwepa dhambi ya asili!

Mimi na swali jepesi haya Ndio mafundisho ya Ukristo Au hivi ndivyo Biblia inatuambia?
Nasubiri majibu!
 
Tukutane Jukwaa la Dini, tuelimishane kuhusu dhambi ya asili.
Pasco
 
Mkuu Mimi nasubiri ushahidi Wa mafungu Wa kufanya kila kitu kasoro kuumba na kutoa Roho!
Hapa ndipo naposubiri!
Huku ndiko tulikotakiwa kwenda tangu mwanzo na sio huu ubishani!, wewe una uwezo wa kufanya kila kitu!, na kwa vile u miongoni mwa mlionibeza sana humu, hebu pokea mstari huu, kutoka [h=3]Mathayo 17:20[/h][h=3]"Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu" [/h]Maana ya mstari huu ni binadamu amepewa uwezo wa kufanya kila kitu only if, ataamini kuwa uwezo huu anao!, chembe ya haradali ni mbegu ya tunda la komamanga!, hii inamaana imani ya wengi ni kama mbegu ya mchicha!,
Kitu cha kwanza to open powers doors ni kuamini, " you have the powers!, and you can be anything, anybody, and you can do everything!.
Pasco.
 
Tatizo huyu jamaa anajibu maswali kutokana na kichwa chake kinavyomtuma, kama yeye anakiri kuwa ni Mkristo kwanini apingane na Biblia?
niwekee kifungu chochote cha Biblia unachodhani nimepingana nacho, nami nitakuwekea kipande hicho kutoka ndani ya Biblia, na kipande kama hicho kutoka vitabu vingine vilivyoandikwa miaka 300,000 kabla ya Biblia, ili kuwatendea haki wasio Wakristu!.
Pasco.
 

Narudia tena, Imani anayozungumzia Yesu ni Imani ya mwanadamu kumwamini Mungu na si vinginevyo kama unavodai. Ndio maana walioponywa walimwamini Mungu na si kujiamini wao kama wao. Mbona hiyo Imani iliyomo ndani mwao haikuwaponya mpaka walimwomamini Yesu? Wengine walipogusa upinde wa nguo ya Yesu waliponya. Mbona hakutumia Imani yake kujiponya?
 

Umesema kuwa kinachoponyesha ni power na Si Jina la Yesu. Mbona Yesu alisema Waaminio Jina lake watatenda Ishara hizo??? Wewe unasema sio Jina la Yesu, huoni kama unapingana na Biblia???
 

Kwa nini usiachane na hawa walokole waliokunywa maji ya msalaba, kisha tukaendelea na mada yetu ? Wameshaambiwa waende kwenye thread nyingine inayohusiana na dini, but wao wamekazana kubishana tu hapa ...!!! Achana nao, tuendelee na masomo yetu, maalim Pasco
 
mbona najibu kila kitu?!, sijajibu nini?!.
Pasco

Ulisema kuwa kila mwanadamu ambaye yupo hai yaani amepuliziwa pumzi basi huyo ni nafsi hai na huo uhai umesema ndio Roho na roho hiyo ndio R/Mtakatifu. Sasa nataka nikuulize maswali kutokana na maneno haya :-
1. Unajua maana ya Ubatizo?
2. Nini tofauti kati ya Ubatizo wa Yohana na aliokuja nao Yesu?
3. Yesu alikuwa mwanadamu kamili, sasa Je, kama R/Mtakatifu alikuwa ndani ya Yesu kama unavodai, unadhani kwanini hakutenda Miujiza yoyote ile??? Na kama Yesu tunatambua amekuja kama Mwanadamu yaani akiwa na Powers kwanini hakutenda lolote kupitia hizo Powers?
Biblia inaniambia Kristo alipobatizwa Mbingu zilifunguka na ROHO MTAKATIFU alishuka kama ua na kuketi Begani kwa YESU. Wewe unadai Yesu alikuwa na R/Mtakatifu tangu alipopata pumzi kuwa nafsi hai, BIBLIA inasema ni punde pale alipobatizwa. Na Yesu hakuanza kazi rasmi aliyotumwa na MUNGU mpaka pale ROHO MTAKATIFU alipomshukia.
 

Ndugu fungua ufahamu wako, kama haya mafundisho msingi wake ni Biblia, basi hii thread ina-qualify kuwa ya kidini na si vinginevyo. Na kama haya yanayofundishwa yapo zaidi ya miaka 300,000 iliyopita, basi hayataitwa ukristo wala hayatatumia Biblia kama msingi wake mkuu. Na kila kilicho nje ya Biblia si ukristo, mbona logic ni simple sana? Mweleze guru Pasco aeleze ukweli wa asili ya haya mafundisho na aachane na Biblia ambayo imekuja jana tu kwa mujibu wake.
 
Last edited by a moderator:


:closed_2:
 
Hii hapa ndiyo asili ya hii imani inayodhaniwa mpya. Tazama hii video ujifunze siri zooote za maguru:

[video=youtube_share;mLHx-r6-a3o]http://youtu.be/mLHx-r6-a3o[/video]
 
Kwanini usiupeleke huko na huu uzi wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…