Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Hatimae Pasco amesanda game...vita kuhusu uhalali wa uzi huu na maudhui yake ilikua kubwa sana...kwa sisi wapenda kujifunza mambo mapya na makuu tusiyoyajua tulikua nae bega kwa bega katika kumsupport na kuupa nguvu uzi huu uendelee kuwepo.
Binafsi nakushuru bwn Pasco hata kwa hichi kidogo ulichotupa nimeongeza ufahamu na maarifa mapya ingawa sita kuwa mkweli nisipo kuambia "I am very disappointed " uelewi ni jinsi gani nilivyokua keen kuufatilia uzi huu toka day one.
Wadau mliokua mnampinga Pasco moja kwa moja naona lengo lenu limefanikiwa
 
Last edited by a moderator:
Pole!. The game is still on again, ila na break vipande vidogo vidogo!.
Pasco.
 
Wanabodi,
(Hii ni topic mpya nimeipandisha humu, nasubiri approval ya modes ndipo ianze kuonekana rasmi, hivyo kwa vile sijui mode ataaprove saa ngapi, na sisi wengine tunaweza kuandika only wakati tukiwa kwenye mood ya kuandika, hivyo naiendeleza hapa wakati mood bado iko juu, mode wakisha approve, nitaihamishia kwenye thread yake)

Baada ya mapimziko ya muda mrefu, nimerejea katika makala zangu kuhusu "works of powers", nguvu za kutenda miujiza, "psychic powers!", leo nitajikita zaidi katika nguvu za uponaji "faith healing!". Nitakuwa na maeneo yafuatayo.
  • Faith Healing ni nini?.
  • Faith Healing Inafanyikaje?.
  • Nguvu za Uponyaji zinatoka wapi?.
  • Je Wahubiri wa Uponyaji ni Lazima wawe Wakristu?.
  • Kwa Wanaoamini Mungu, Roho Mtakatifu na Yesu, Jee ndie yeye anayeponya?!.
  • Kwa Wasioamini Mungu huyu tunayemuamini, Jee na hao wanatumia nguvu za nani kuponyeshea?!.
  • Jee mtu asiyeamini kabisa Mungu, anaweza kufanya miujiza?!, kwa nguvu za nani?!.
  • Mungu ananguvu, ila shetani pia ananguvu!, jee kuna miujiza inafanywa na shetani?!.
  • Nitajitambuaje kama nina uwezo wa kufanya miujiza?!.
  • Nakuhakikishia, ni Hakika Asilimia 100% kwa 100% Uwezo huo unao, ila kwa vile hujitambui, hautumii!. Jitambue, utumie!.

NB. Ili kutopoteza focus, naomba mniruhusu nisijibu hoja zozote mpaka mada ikamilike points zote kumi, huku nikisisitiza hizi mada ni kwa watu ambao ni open minded!, Nawaomba sana wale wahafidhina na ma conservatives wa imani za dini zao, shikilieni mafundisho ya dini zenu, na wenye nia ya kuanzisha malumbano ya dini, tukutanie Jukwaa la Dini, tuwekane sawa!.

Natanguliza Shukrani.

Pasco.
 
1. Somo la Kwanza, Faith Healing ni Nini?!.

Kwa wale ambao ni wageni, nawashauri kabla hujaanza na uzi huu, wapitie kwanza hapa, Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila ...

Na tuanze kwa kukumbushana tuu kidogo the basics!.
  • Sisi binadamu tumeumbwa na Mungu kwa mfano wake. Ule uhai aliotupulizia, una nguvu za KiMungu ndani yetu!. Haijalishi wewe ni wa dini gani, ni wa imani gani, au hata wasio amini, wote tumeumbwa na Mungu, hivyo uwezo wa KiMungu uko ndani yetu, ni kwa kuutumia uwezo huu, ndipo muujiza hufanyika!.
  • Faith Healing, ni uponyaji kwa kutumia imani!. Ambapo ule uponyaji huitwa muujiza. Hitoria ya kupona kwa miujiza ilianza zamani na sehemu kubwa ilijikita katika dini!, huko mimi siendi. Lengo la uzi huu ni kukujulisha wewe kuwa miujiza yoyote inayotokea, inawezekana kwa uwezo ilio ndani ya mtendewa muujiza na sio mtenda!.
  • Hii Faith Healing ni kitendo cha mtu mwenye ugojwa fulani, kupona kwa njia ya imani tuu bila kutumia dawa yoyote, hivyo kipona kimiujiza, na uponyaji huu sometimes unahusisha hadi kukua wafu, au kuzui kifo, vipofu wanaona, visiwi wanasikia, bubu wanaongea, vilema wanaponyeka, viwete wanatembea, wagomba wanapata watoto, maradhi yoyote yanaponyeka.
  • Miujiza hii imegawanyika katika makundi makuu matatu, ya kwanza ni ile miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe, muujiza mkuu ukiwa ni uumbaji! wa ulimwengu na kumuumba Adam. Miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe mingine ina sababu na mingine haina sababu, mfano muujiza wa kuiamuru bahari ya Sham kufunguka, ilikuwa na sababu ili Wana wa Israel wapite, lakini muujiza wa Bikiri Maria kupokea mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, haukuwa na sababu kwanini Maria, kulikuwa na mabikira wengi tuu!. Hii miujiza ya Mungu mwenyewe huitwa miujiza mikuu!. Miujiza iliofanywa na Yesu, nayo inaingia kwenye kundi hili la miujiza mikuu kufuatia imani kwa wanaomuamini Yesu ni Mwana wa Mungu, hivyo ni Mungu!
  • Kisha kuna miujiza inayofanywa na sisi binadamu kupitia uwezo wa KiMungu ulio ndani yetu. Hii inajumuisha miujiza iliyofanywa na manabii, miujiza iliyofanywa na binadamu kwa uwezo wa Mungu ilio ndani yetu na mambo mazuri, na mema yote yanayofanyika duniani, ni kazi nzuri ya roho wa Mungu aliye ndani yetu.
  • Pamoja na uwepo wa Mungu ndani yetu, mwovu shetani pia naye yupo duniani, na anazo nguvu kama za Mungu kutenda karibu kila kitu ambacho Mungu anatenda isipokuwa Mungu ana nguvu zaidi ya shetani!. jambo moja tuu!, upande wa uumbaji!. Yaani God is the creator and giver of life na ni ndani ya hii life ndimo zilimo nguvu za Mungu ndani yetu. Tofauti pekee kati ya Mungu na shetani, ni "life" shetani hawezi kuumba ila ndie muagamizi wa life. Maovu yote yanafanyika humu duniani ikiwemo miujiza ya uovu, ni kazi ya shetani. Zile sifa kuu tatu za Mungu, Omnipotence, hana mwisho, na shetani pia hana mwisho, tofauti ni Mungu ni wa milele na makao yake ya milele ni peponi, mbinguni au ahera kwenye furaha ya milele, na shetani makao yake ya milele ni motoni, kwenye ziwa la moto, akiungua na kuteseka milele!. Mungu ni Omnipresence, yaani yuko kila mahali, kitendo tuu cha mwanaadamu kupuliziwa pumzi ya uhai yenye Uuungu ndani yake, kunapelekea ndani ya kila binadamu kuna Mungu ndani yetu!, shetani naye alitupwa duniani, yeye na jeshi lake, nao pia wako kila mahali!. Mungu niOmniscience, ana uwezo wa kujua kila kitu kabla hakijatokea, there is nothing new under the sun, hivyo lolote litakalotokea, lilikuwa litokee, ila shetani naye ana uwezo wa kuijua mipango yote ya Mungu na kujitahidi kuiangamiza!.
  • Hivyo faith healing ni uwezo wa kufanya miujiza ya uponyaji kwa kutibu kwa kutumia nguvu za Uungu zilizo ndani yetu, au kwa waliomkaribisha shetani ndani yao, basi ni uwezo wa iponyaji au kutibu kwa kutumia nguvu za shetani zilizo ndani yao!.
Somo la pili la Faith Healing hufanyika vipi, linafuata.
Pasco.
 
Tiririka baba, wale wahafidhina walozaliwa wakakaririshwa vitu angali wadogo hadi sasa wapo jf chondechonde musiharibu hii mada sasa,
Mtulie tuli kama maji ya mtungi, soma pita kule if no constructive idea.
 
Afadhali mkuu Pasco umerudi kwenye psychic powers,angalizo,wa imani kali msituharibie uzi kama mlivyofanya mwanzo,hili sio jukwaa la dini,ningeomba pia mods wawe wanazihamisha posts zozote zitakazokuwa zinaletwa kuhusiana na dini wazipeleke jukwaa la dini.
 
Last edited by a moderator:
Sikubaliani na hilo hata kidogo, nitachojua no salvation , no life,,, nitarudi kwa ufafanuzi zaidi,
 

Hakuna cha imani kali, vikitumika vifungu vya biblia lazima tuje kunyoosha panapopindishwa makusudi.
 
Last edited by a moderator:

Watanzania ni waajabu sana. Mnapend spoon feeding. Hakuna jipya hapa kwa mwenye ufahamu.
 
Tiririka baba, wale wahafidhina walozaliwa wakakaririshwa vitu angali wadogo hadi sasa wapo jf chondechonde musiharibu hii mada sasa,
Mtulie tuli kama maji ya mtungi, soma pita kule if no constructive idea.

Unadhihirisha ushamba wako. Kipi kipya hapo? Watu wamefanya hayo, walipoijua kweli wenyewe wakatoka.
 
Somo la Pili. Faith Healing unafanyikaje na inatibu vipi?.
  • The most powerful thing kwenye mwili wa binaadami ni "will powers", "where there is a will, there is a way!. Hii "Will power" ni nguvu ya Mungu iliyo ndani yetu yenye uwezo wa kufanya kila kitu, ikiwemo miujiza!. Ili hii "will powers iweze kutenda miujiza, it has to be invoked!.
  • Prescription ya faith healing, ni imani kuamini, na inafanyika kwa aina nyingi na kwa namna nyingi. Aina maarufu ni ile ya kuombewa na wahubiri/wachungaji/mitume/manabii/masheikh/viongozi wa dini/walokole/wanajimu/waganga wa kienyeji/watoa tiba mbadala etc, etc, dawa pekee kwenye tiba hii ni imani!. Kitendo cha kuamini ndicho kina invoke zile doors za forces of will to act upon a specific desease and cure it!.
  • Kinachofanyika ni kwanza kutengeneza imani ya kuamini unachotakiwa kuamini. Kwa wale wa imani ya Kikiristu kwanza ni kuamini kwa dhati kuwa Yesu anakoa, Yesu anaponya, hivyo anayekuhubiria kwa kulitaja jina la Yesu, "Katika Jina la Yesu Zishindwe!", "Katika Jina la Bwana", etc, etc. Kitendo cha kuamini kuwa Yesu anaponya, kunafungua milango ya "powers of will" zilizo ndani yako ndizo zinazokuponya!. Kinachoponya ni nguvu ya Uungu iliyoko ndani yako, lile jina la Yesu, limetumika kama ufunguo tuu wa kufungulia hizo potentials zilizoko ndani yako!.
  • Wale wahubiri wa miujiza, wanachofanya ni kuutumia uwezo wao wa kuconvince ili kuifungua imani yako, ili ifungue hazina ya nguvu za uponyaji zilizoko ndani yako ndizo zinazotenda miujiza na sio yule mhubiri wala hilo jina!. Mhubiri ni make believe tuu na Jina la Yesu ndio ufunguo wa imani yako ili kufungua nguvu zilizo ndani yako kukuponya baada ya kuamini kwa dhati umepinywa!.
  • Wako watu kibao wanatibu kwa faidh healing bila kulitaja jina lolote na watu wanapona!, kinachotakiwa ni kuamini tuu!, ndiko kunakofingua milango ya "powers" na haijalishi unaamini nini, iwe Mungu, Allah, Budha, Mti, jiwe, milima, kichuguu, hirizi, mganga or whoever, whataver as longo as unaamini utapona, unapona!.
  • Namna ambayo hizo powers of will zinavyofanya kazi, ni un explainable scientifically, biologically, or medically, ila kinachoonekana ni matokeo tuu, viziwi wanasikia, vipofu wanaona, na viwete wanatembea na vilema wanaponyeka! ndio maana inaitwa miracles, miujiza na jina rasmi la kibinaadamu inaitwa ni kazi ya Mungu, au miujiza ya Mungu, na kwa vile nguvu zinazotumika ni nguvu za Mungu zilizo ndani yetu, hivyo ni haki kuita hii ni kazi ya Mungu.
  • Wengi hukumbilia kwa wahubiri kuomba kuponywa wakati tayari wameathirika!. Kwa kujua kuwa hizo nguvu za uponyaji ziko ndani yetu, unaweza usisubiri hadi kuugua ndipo uinvoke will power ikutibu, ikiisha jitambua its you, and no one else, then unaweza kuivoke hiyo will powers ikazuia usipate ugojwa, yaani prevention is cure!.
  • Hivyo kwa kuanzia anza kwa kujiandaa kuamini ili hiyo imani yako ifungue milango ya nguvu za Mungu za kufanya uponyaji zilizo ndani yako, suo tuu zikuponye, bali pia kuzitumia as shield kuzuia magonjwa yoyote yasikufikie wewe na famulia yako!.
Muendelezo unaofuatia ni ushuhuda wangu mimi Pasco wa JF jinsi powers of will inavyotenda maajabu!.

Asate,

Pasco
 
Unaeleweka Pasco,mpaka hapo hakuna point yoyote inayopingana na imani ya mtu lete maarifa mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Nikiwa primary, nilisumbuliwa sana na malaria, dawa zilikuwa choloquine, baadaya kupona nilikuwa nawashwa sana!, nikawa napewa na phenogan, lakini wapi, ukijumlisha nilikuwa kibonge na vipele vya jasho, ilikuwa baada ta kupona napata mateso makubwa zaidi kuliko hata nilivyokuwa naumwa!. Nikaanza kudevelop ioga wa dawa za malaria, hivyo nikiumwa, bora nisiseme, nijikaze hadi nikizidiwa saana ndipo niseme!.

Thrugh nilipoingia sekondari uoga huu wa dawa,ukazidi, nikawa nikisikia dalili kwa mbali, napiga moyo konde, kisha dalili zinapotea. Tangu baada ya mulaliza sekondari, nilikaa 10 years bila kuugua malaria!. Mwaka 2000, nikapata trip ya Canada nikatakiwa kuomba migrant visa, inatolewa Nairobi, ila pia shurti upime ngoma kwenye accredited hosputal ilioorodheshwa, hivyo nikaenda Agha Khan hatua ya kwanza ni kupima full blood picture!, jamaa alinipima tuu, akaja ana shangaa, how could this man survive vidudu ving ajabu vya malaria sijui ni plus plis ngapi!.

Jamaa wa maabara akaniita ni kuniambia nina malaria nyingi ya ajabu kiasi kwamba anashanga niko hai?. Kwa kiwango hicho, i was supposed to have been dead long ago!. Sikumuhadithia, nikamweleza hapa nimekuja kupima ngoma ndio mpango mzima!, jamaa akasema kwa kiwango cha malaria kilichopo, natakiwa kwanza kirudi kwa daktari, ndipo nikaridi kwa dakrati na vipimo, Dr pia akashangaa!. Akasema first thing natakiwa kuwa addmited haraka sana!, nikamgomea kuwa siumwi, sikubali kuwa addmited nahitaji tuu kipimo cha HIV!.

Ndipo yule dr akanieleza kuwa huwezi kupimwa HIV kwa sababu damu yangi ina kiwango kikubwa mno cha vimelea wa malaria beyond human survival, hivyo white blood cells hazionekani kabisa!, kipimo cha ngoma enzi hizo kimbe kilikuwa kinapima tuu kiasi cha kinga iliyopio, wakikuta imeshuka, ndipo wanajua ni HIV+ve, akanieleza nina very chronic malaria, hivyo kipimo kitaonyesha ni positive hivyo ili nipime, ngoma lazima kwanza niitibu malaria!. Akanieleza hata wagonjwa wa TB wakiscreen inaonekana ni ngoma, ukiitibu ukapona ndipo inapimwa ngoma!.

Hiyo daktari nikamweleza ukweli kuwa huwa naugua malaria lakini kutokana na kuogopa dawa, sithubutu kuitibu, its 10 years now!. Akashangaa na kusema hakuna hii kitu ya mtu kutougua malaria tropical Africa. Akanihimiza kukubali admission, pesa ikawa ni issue!, ndipo akaniambia kama tatizo langu lilikuwa chloroquine sasa kuna metakelfin na fansidar hivyo element ya kuwashwa hakuna!, lakini kutokana na kiwango kikubwa cha malaria kwenye damu yangu, ana recomend drip ya quinine ili kuipinguza kidogo kodogo!. Sina pesa za kulazwa Agha Khan, kwanza nimekwenda tuu hospitali hiyo kwa sababu ni mark hospital kwa migrant visa ya Canada.

Hivyo nikasisitiza nipewe tuu vidonge. nikapewa metal kelfin kunywa winne siku ya kwanza, kisha vinne tena siku ya pili na viwili siku ya tatu, siku ya nne nirudi kucheki!. Siku hiyo nikanywa usiku, na maji mengi kwa maelekezo ya daktari!, mwili ulikuwa unawaka moto, sikulala usiku kucha ni kukoroma tuu kwa kugumia maumivu, kesho yake sikuweza kuamka, mwili wote umevimba, chakula hakipiti, maji hayapiti, siwezi kuamka, kiukweli nikajua sasa ndio safari!.

By that time wife keshahamia US, na mimi naenda kuhamia Canada kwenye issue nyingine kama prospective husband wa a Tanzanian lady mwenye Canadian citizenship!. Hivyo nikaomba msaada home kwa wazee, nikafuatwa nikapelekwa Tumaini Hospital nikalazwa, wakachukua vipimo upya wakakuta kuvimba ni reaction ya sulfa, hivyo wakabadili dawa nitundikiwe drip ya quinine kuishusha hiyo malaria wakati huo mwili unajoto kali ajabu!.

Drip ya kwanza imekwisha uvimbe umepungua lakini malaria bado ipo na homa bado juu, drpi ya pili ikaisha hsli ile ile, drop ya tatu naingia siku ya pili, hali ile ile, nikaona madaktari wanapisha, kama panic fulani, homa gani hii haishuki, Dr, Mkuu wa Pale Dr. Yongolo akasema ikifika siku ya tatu haijashuka, nitahamishiwa muhimbili!. Pia akamleta Dr Mmoja bnti mrembo toka Mhimbili akiita Dr. Masha Makata, Msukuma ni Msukuma tuu, hata mgonjwa vipi, binti mrembo mweupe!, mbona nilipata nafuu ghafla, nikakaa kitandani!.

Kiukweli Masha alikuwa very friendly, akajaribisha dawa nyingine nyingine, homa ikashuka, vidudu vya malaria sasa havipo, lakini bado naumwa!. Nikaomba Masha aje baada ya ndugu kuondoka, ndipo nikaconfess kwake kuwa hii inawezekana kuwa ni ngoma!, nakamuomba akanipime kisiri siri ili nijue cha kufanya na sio kuunguza tuu fedha hospitalini. Akasema mgonjwa mwenye hali kama yangu, haruhusiwi kupima ngoma, ila kila mgonjwa anaelazwa kwa lolote, pia anapimwa ngoma, hivyo na wao walikuwa wanasubiri 7 days ndipo nipimwe!, nikaziona ni mbali, nikamsihi amisaidie, akanigomea kuwa yeye kama daktari hawezi, ila kunisaidia ataniitia mtu wa maabara niongee nae!.

Jamaa wa maabara akaja siku ya nne, akatoa damu, na kwenda kuipimia Mhumbili majibu atampa Masha. Siku hizo ukipima leo majibu kesho. Adubuhi ya suku ya 5, Dr. Masha kaja asubuhi, smiling na mimi nazidi kupata nafuu, huku riho inadunda. Niliisha panga nini cha kufanya iwapo nitakuwa positive maana nimeisha shuhudia shughuli ya kuwahudumia terminal ill HIV victims ndani ya familia, by the vidonge vya kupunguza makali vinatoka Nairobi au South na ku drain the family at the end of the day bado mtu ni safari!. Miliisha jiandaa kisaikolojia kuzuia kutesa watu!. Ndipo Masha akaniambia niko negative!. Amini usiamini nilipona pale pale nikataka kusimama drip ikanizuia!.

Mwaka huo wa 2000, ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kutibiwa malaria ndani ya miaka 10!, na ndio mara yangu ya mwisho kutibiwa malaria mpaka hii leo 14 years on, no more malaria!. Hata nikijisikia kuumwa, nikipimwa na kukutwa nayo, never again nitathubutu kuitibu!.

Huu ndio ushuhuda wangu!.
Next ni how is it possible, jee ni malaria tuu au na magonjwa mengine?.

Pasco.
 
Mbona wapo watu wengine hawaijui iyo kweli yenu na wanafanya hiyo hiyo miujiza mnofanya nyie mlio kwenye ukweli,
Nipe mfano wa muujiza ulofanywa na wanoijua kweli yako haujafanywa na wasio ijua iyo kweli,
Kufufua kuna dini/ watu wamefufua,
Kutembea juu ya maji kuna raia zinatembea nenda ka google uone,
Kugawa mikate na samaki wapo walogawa, kila kitu mkuu watu wa mataifa wanaweza, nambie kwann? na hizo nguvu unazitofautishaje na za wanaoijua kweli. Which is false wich is tru
 
Somo la Tatu: Nguvu za Uponyaji zinatoka wapi?.

  • Msingi wa Nguvu za uponyaji ni Mungu, kwa jina lolote lile. Siku Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano ambapo mwili wetu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Mwili ni hii body inashikika, inaonekana, ina uzito, ina tabia zote za maada/matter. Sehemu ya pili roho, ni pale alipotuumba kwa ,fano wake na kutupulizia pumzi ya uzima, life, life force, spirit, spiritual body, astara body, roho, uhai. Kinachofanyika ndani yangu kuzuia malaria ni kufuatia ule uoga wangu kuogopa kuteseka na dawa za malaria, ninapo jisikia dalili tuu za awali kabisa, kwa mwili kuwa hypasensitive to touch, nikijigusa tuu vinyelea vya mkono, you feel something, then nasema kwa imani, it can't be malaria!. Hii inaitwa "denial the negativivity", kwa kujitamkia tuu maneno hayo kimoyo moyo, hiyo malaria stops there and then!.
  • Hizo powers zipo ndani yetu zimehifadhiwa, namna ya kuzifungua ni kwa imani tuu!. Ukiamini, Milango ya powers inafunguka, "powers from within" zinaufanya mwili kuwa stronger na vile vidudu vya malaria harmless ila vipo!. Kadri siku zinavyokwenda vijidudu vinazidi ku pile, ila ni harmless. In ten years time vikawa vingi sana but harmless, nilipopimwa mpimaji anashtuka, daktari anashtuka, mimi niko ok.
  • Kitendo cha kukubali kunywa ile dose, ni "accepting defeat" hivyo nika break ile barrier ya strenght ya powers from within, hivyo ile kinga ya mguva zangu ikatoweka, wale wadudu waliokuwa dormat wakarudi kuwa active, nisingewahiwa hospitali, pale ndio ingekuwa safari!. Once ukishajiaminisha kitu fulani kibaya kwako ni never, then don't and never accept defeat!. Ukiisha weka nia, never go back, ng'ang'ana hapo hapo hata kama hujaona matokeo spontaneously, never give up, Mungu ana namna zake za kujibu, halazimishwi!.
  • Tangu ile 2000 mpaka leo, 2014, sijawahi kuugua tena malaria, lakini sasa sio mimi tuu bali na nyumba yangu yote, nimeishield, hatuugui malaria sisi wote tunaishi humo!. Nina watoto 7!, watano wakubwa na wawili wadogo. Wale wakubwa wote watano hawaishi home, wawili wakubwa wako chuo, mmoja yuko A level boarding na wawili wako O-level boarding, home niko na wale wadogo wawili tulio nao home malaria ni no tangu wamezaliwa ma hakuna trips za hospital zaidi ya cliniki. Wale wa boarding, sometimes wanapata malaria wakiwa shule/vyuo ila wakirudi home, no more malaria!.
  • Baada ya kufanikiwa kwenye malaria, nikaamua kusema no kwa baadhi ya magojwa mengine!. Hata katika pita pita zangu, ukikutana na "njia" ambayo sio, machale yanakucheza hivyo sipiti "njia" hiyo!. Na baada ya kutopita, hautapita muda mrefu sana utasikia ya kusikia kuhusu ile "njia" uliotaka kupita!.
  • Kwa vile hizi works of powers hazina uthibitisho wowote, scientifically, biologically, anatomically or medically to prove how they work, then siwezi kusema conclusiwe kwamba hizi kwangu ni powers za kuzuia malaria, inawezekana its just a game of chance kwamba mbumbu wote wanaingia nyumbani kwangu au kokote ni nilipo ni wale mbu wasio na malaria!.
  • Pia licha ya kuwa na hiyo kinga dhidi ya malaria, au machale ya kuziepuka "njia" fulani fulani katika "pita pita" yangu, sasa badi ndio tusilale na neti, si tuna kinga?, au kule katika ile "pita pita" ndio nijipitie tuu peku peku ati kwa sababu nina kinga!. No way!.
  • Hata wale wanaotibiwa maradhi kwa imani, haina maana akiumwa ndio asiende hospitali ati kwa sababu tuu anamtegemea Mungu!, au alikuwa na ukimwi, kifua kikuu, canser, akatibiwa kwa imani, akapona, basi hospitali ndio basi!, no!. Faith healing is not a substitute to medical treatment, but rather a complementary!.
  • Namalizia kwa msisitizo, kuponywa kwa miujiza, nguvu za uponyaji zinatoka kwako wewe mgojwa mwenyewe na sio hiyo anayekuombea!. Wachungaji wengi au waganga, hujifanya wao ndio wenye hizo nguvu za kuponya!, No way, wao wanakupatia tuu ufunguo wa kuzifungulia hizo nguvu zilizo ndani yako ndizo zinazoponya. Hata kile kikombe cha Babu, what you drink is nothing!, imani kuwa kikombe kinaponya ndio imewafungulia njia wenye imani, nguvu zao zilifunguka zikawaponya, na wale wenye imani haba, it was a waste, wastage of time and resources!.
  • Ukiwa na very strong faith kuwa sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo tunazo nguvu za Mungu ndani yetu, chochote utakachopanga kwa imani, kitafanikiwa!, sky is the limit!.
Anza sasa kuzifungua hizo nguvu zako na kuanza kuzitumia kufanya mambo madogo madogo.
Mada inayofuata ni sura ya 4. Jee wahubiri wa Miujiza ni lazima wawe Wakristo?.

Asante.

Pasco.
 
Ngoja na mimi nichangie kidogo kuhusu hizo nguvu za uponyaji,mimi mzee wangu aliokoka yapata miaka 20 iliopita sasa hivi ana miaka 76,tokea alipookoka aliapa kutokunywa dawa yoyote na yoyote atakae mpa dawa hata kama atakuwa amezidiwa itakula kwake,sasa ilikuja kutokea akapata Tonsilitis aliteseka nazo kwa takriban wiki 2,zilivimba mpaka zikaja kupasuka,hakwenda hospitali wala kutumia dawa yoyote,mpaka hivi leo ninavyokwambia hajawahi kuugua malaria wala ugonjwa wowote amabao ungetgemea kwa utu uzima aliokuwa nao angekuwa nao.Kwa hiyo hapa kutokana na topic yako mkuu Pasco ninakubaliana na wewe kuwa faith may open the healing power that is within ourselves.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…