Nikiwa primary, nilisumbuliwa sana na malaria, dawa zilikuwa choloquine, baadaya kupona nilikuwa nawashwa sana!, nikawa napewa na phenogan, lakini wapi, ukijumlisha nilikuwa kibonge na vipele vya jasho, ilikuwa baada ta kupona napata mateso makubwa zaidi kuliko hata nilivyokuwa naumwa!. Nikaanza kudevelop ioga wa dawa za malaria, hivyo nikiumwa, bora nisiseme, nijikaze hadi nikizidiwa saana ndipo niseme!.
Thrugh nilipoingia sekondari uoga huu wa dawa,ukazidi, nikawa nikisikia dalili kwa mbali, napiga moyo konde, kisha dalili zinapotea. Tangu baada ya mulaliza sekondari, nilikaa 10 years bila kuugua malaria!. Mwaka 2000, nikapata trip ya Canada nikatakiwa kuomba migrant visa, inatolewa Nairobi, ila pia shurti upime ngoma kwenye accredited hosputal ilioorodheshwa, hivyo nikaenda Agha Khan hatua ya kwanza ni kupima full blood picture!, jamaa alinipima tuu, akaja ana shangaa, how could this man survive vidudu ving ajabu vya malaria sijui ni plus plis ngapi!.
Jamaa wa maabara akaniita ni kuniambia nina malaria nyingi ya ajabu kiasi kwamba anashanga niko hai?. Kwa kiwango hicho, i was supposed to have been dead long ago!. Sikumuhadithia, nikamweleza hapa nimekuja kupima ngoma ndio mpango mzima!, jamaa akasema kwa kiwango cha malaria kilichopo, natakiwa kwanza kirudi kwa daktari, ndipo nikaridi kwa dakrati na vipimo, Dr pia akashangaa!. Akasema first thing natakiwa kuwa addmited haraka sana!, nikamgomea kuwa siumwi, sikubali kuwa addmited nahitaji tuu kipimo cha HIV!.
Ndipo yule dr akanieleza kuwa huwezi kupimwa HIV kwa sababu damu yangi ina kiwango kikubwa mno cha vimelea wa malaria beyond human survival, hivyo white blood cells hazionekani kabisa!, kipimo cha ngoma enzi hizo kimbe kilikuwa kinapima tuu kiasi cha kinga iliyopio, wakikuta imeshuka, ndipo wanajua ni HIV+ve, akanieleza nina very chronic malaria, hivyo kipimo kitaonyesha ni positive hivyo ili nipime, ngoma lazima kwanza niitibu malaria!. Akanieleza hata wagonjwa wa TB wakiscreen inaonekana ni ngoma, ukiitibu ukapona ndipo inapimwa ngoma!.
Hiyo daktari nikamweleza ukweli kuwa huwa naugua malaria lakini kutokana na kuogopa dawa, sithubutu kuitibu, its 10 years now!. Akashangaa na kusema hakuna hii kitu ya mtu kutougua malaria tropical Africa. Akanihimiza kukubali admission, pesa ikawa ni issue!, ndipo akaniambia kama tatizo langu lilikuwa chloroquine sasa kuna metakelfin na fansidar hivyo element ya kuwashwa hakuna!, lakini kutokana na kiwango kikubwa cha malaria kwenye damu yangu, ana recomend drip ya quinine ili kuipinguza kidogo kodogo!. Sina pesa za kulazwa Agha Khan, kwanza nimekwenda tuu hospitali hiyo kwa sababu ni mark hospital kwa migrant visa ya Canada.
Hivyo nikasisitiza nipewe tuu vidonge. nikapewa metal kelfin kunywa winne siku ya kwanza, kisha vinne tena siku ya pili na viwili siku ya tatu, siku ya nne nirudi kucheki!. Siku hiyo nikanywa usiku, na maji mengi kwa maelekezo ya daktari!, mwili ulikuwa unawaka moto, sikulala usiku kucha ni kukoroma tuu kwa kugumia maumivu, kesho yake sikuweza kuamka, mwili wote umevimba, chakula hakipiti, maji hayapiti, siwezi kuamka, kiukweli nikajua sasa ndio safari!.
By that time wife keshahamia US, na mimi naenda kuhamia Canada kwenye issue nyingine kama prospective husband wa a Tanzanian lady mwenye Canadian citizenship!. Hivyo nikaomba msaada home kwa wazee, nikafuatwa nikapelekwa Tumaini Hospital nikalazwa, wakachukua vipimo upya wakakuta kuvimba ni reaction ya sulfa, hivyo wakabadili dawa nitundikiwe drip ya quinine kuishusha hiyo malaria wakati huo mwili unajoto kali ajabu!.
Drip ya kwanza imekwisha uvimbe umepungua lakini malaria bado ipo na homa bado juu, drpi ya pili ikaisha hsli ile ile, drop ya tatu naingia siku ya pili, hali ile ile, nikaona madaktari wanapisha, kama panic fulani, homa gani hii haishuki, Dr, Mkuu wa Pale Dr. Yongolo akasema ikifika siku ya tatu haijashuka, nitahamishiwa muhimbili!. Pia akamleta Dr Mmoja bnti mrembo toka Mhimbili akiita Dr. Masha Makata, Msukuma ni Msukuma tuu, hata mgonjwa vipi, binti mrembo mweupe!, mbona nilipata nafuu ghafla, nikakaa kitandani!.
Kiukweli Masha alikuwa very friendly, akajaribisha dawa nyingine nyingine, homa ikashuka, vidudu vya malaria sasa havipo, lakini bado naumwa!. Nikaomba Masha aje baada ya ndugu kuondoka, ndipo nikaconfess kwake kuwa hii inawezekana kuwa ni ngoma!, nakamuomba akanipime kisiri siri ili nijue cha kufanya na sio kuunguza tuu fedha hospitalini. Akasema mgonjwa mwenye hali kama yangu, haruhusiwi kupima ngoma, ila kila mgonjwa anaelazwa kwa lolote, pia anapimwa ngoma, hivyo na wao walikuwa wanasubiri 7 days ndipo nipimwe!, nikaziona ni mbali, nikamsihi amisaidie, akanigomea kuwa yeye kama daktari hawezi, ila kunisaidia ataniitia mtu wa maabara niongee nae!.
Jamaa wa maabara akaja siku ya nne, akatoa damu, na kwenda kuipimia Mhumbili majibu atampa Masha. Siku hizo ukipima leo majibu kesho. Adubuhi ya suku ya 5, Dr. Masha kaja asubuhi, smiling na mimi nazidi kupata nafuu, huku riho inadunda. Niliisha panga nini cha kufanya iwapo nitakuwa positive maana nimeisha shuhudia shughuli ya kuwahudumia terminal ill HIV victims ndani ya familia, by the vidonge vya kupunguza makali vinatoka Nairobi au South na ku drain the family at the end of the day bado mtu ni safari!. Miliisha jiandaa kisaikolojia kuzuia kutesa watu!. Ndipo Masha akaniambia niko negative!. Amini usiamini nilipona pale pale nikataka kusimama drip ikanizuia!.
Mwaka huo wa 2000, ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kutibiwa malaria ndani ya miaka 10!, na ndio mara yangu ya mwisho kutibiwa malaria mpaka hii leo 14 years on, no more malaria!. Hata nikijisikia kuumwa, nikipimwa na kukutwa nayo, never again nitathubutu kuitibu!.
Huu ndio ushuhuda wangu!.
Next ni how is it possible, jee ni malaria tuu au na magonjwa mengine?.
Pasco.