Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?


Mkuu Pasco hebu niambie uelewa wako juu ya hili. Kwakuwa zipo nguvu za Mungu na za shetani, kwa watu walizonazo ipi ni Nguvu kuu? Je, kwakuwa ni imani zetu tu ndio umesema zina invoke nguvu za kutenda miujiza kwa watu wawili kwa mfano, mmoja anaamini shetani na mwingine anaamini Mungu wakipambanisha imani zao ktk kutenda muujiza fulani ni yupi atashinda? Na kama atashinda/atashindwa kwanini ashinde/ashindwe wakati kila mmojawapo kati yao anatenda ivyo kwa imani iliyo ndani yake?


 

Katika episode 2 ya mafundisho haya ya Pasco aliahidi kujibu maswali yote mwisho hili hasije akapoteza mtiririko mzuri wa somo...kwahiyo mkuu tunza swali lako litajibiwa mwishoni.
Afu hili kama wazo naona kama hakukuwa na ulazima wa wewe ku quote posts zote hizo wakati swali lako ni general in fact hii ni thread ya Pasco kwahiyo chochote kinachofanyika hapa anapata notifications tu...point yangu unatupa kazi sana kufollow siye wengine tunatumia simu afu vile vile unakua umeshiriki kuijaza saver unnecessary...
 
Hapana ndugu mbeki hili ni jukwaa la wazi hivyo huna ulazima wa kunifunga mawazo ya kuhitaji kujua nisichokijua. Badala ya wewe kupoteza muda kwa kuniambia najaza server ni vema ungenijibia maswali yangu kama una ufahamu nayo kuliko kujaza server kwa swali lisilokuhusu.
 

Mbona mkuu hata sina uwezo wa kukufungia kujadili hata ningekua na uwezo huu uzi huu sio wangu...niwie radhi kama nimeleweka vibaya kwako ila nia yangu ni kuboresha tu uzi huu maana kila mtu yupo hapa kujifunza.
Kama ukirudia soma upya nilichosema sina tatizo na wewe kuuliza swali ila nilitoa kama wazo unapo quote post nzima kwa sie wengine tunapata shida kufollow uzi vzr maana tunatumia simu kama unatumia JF app utakua unanielewa.
Na kuhusu kujaza sever nililisema sio kwa sababu ya we kuuliza swali bali nimesema hilo sababu nimeona hakukua na ulazima wa wewe kuquote post nzima maana hata ungeuliza swali lako tu pasipo kuquote posts zote maana ungeleweka tu.
All in all sikuwa na nia mbaya nawe samahani kama nimekukera kwa namna moja au nyingine
 
Inaonekana ni Topic moja nzuri sana. Nmekuwa Interest nayo kwa kias kikubwa, tangia nianze kufuatilia Habari kama hiz kwenye source mbalmbal (nilianza na Illuminant nikaja Freemasonry lakin bado nilikuwa cjapata point nilizokuwa nikizihitaji. Sasa nmeona hii maada inabeba kila kitu chenye uhalisia wa Maisha Ya WanaDamu.

Ushauri wangu ni kwamba kwann tuiishie kusoma,kuelewa na kuchangia point kwenye Mada hii tusifanye taratibu tukafungua kituo cha Mafunzo/Masomo il hata wengine tuzidi kukomaa kufuatilia kila Hatua.

NaSupport Sana Kichwa cha Mada hii kuwa Kila Mwanadam ana psychic powers na kuna wakati anaweza kuzitambua ama haczitambue ila akawa anapatwa na baadh ya strange things akabaki anashangaa 'What is this!?'

Binafsi huwa kuna hali fulan hiv Ambayo kuna wakati ninapofanya tukio hisia za haraka unitokea na kuonesha kama nimeshalifanya mda si mrefu lakin papo hapo nafikiria kuwa nilikuwa bado sijalifanya, mf: Nikiwa Nataka kuruka either Mtaro/shimo nk.. Katika ile hali ya maandalizi Akili yangu inaflash kama hilo tendo nimeshalifanya pia nikiwa kwenye motion na inachukuwa mda mfup sana kupatwa na kubaini nini kinaendelea. Ni mara nying nmekuwa nikipatwa na hali hii japo sku hz inaelekea kupungua. Na huwa najaribu kujichunguza lkn conclusion nilikuwa nikijisemea kuwa na Mambo ya kawaida ya Mwilin mwangu. Ckujua kama nia Psychic Powers.

Sasa pengne ninazo nyingne ila zjajtambua maadam nimepata sources nyingne sasa nina mpango wa kufuatilia mwanzo Mwisho Kuhusu suala la "UTAMBUZI"

Tupeane shavu. Nafikiri Illuminant,Freemason na Taasisi nyingne za siri (Secret Societies) walipitia na wanatumia njia hizi katika Kufanya UTAMBUZI,nahisi kama Wamefanikiwa japo inasemeka wao wanatumia ule upande wa Giza haswa na wanatumia fursa hiyo kuconnect pple kwani walishagundua mapema, Kuna Ushindani Mkubwa Hapa Ulimwenguni.

"Just Enough Education To Perform"

TUJITAMBUE!.


Sent from my BlackBerry 8520 using Jamii Forums
 
Yani mambo mnayo sema its like mpo kwa akili yangu. Yani Pasco kuna kipindi nilikuw naota ndoto zingine zinakuwa kama fumbo vile bt nikiamka nkilifikiria na kupata jibi hutokea kama ilivyo pia kuna sometimes zinakuja direct kabisa..sas kuna mtu alikuw ameokoka sas hizo za mafumbo bfore nilikuw sizielewi so nkawa namhadithia akawa anantel maan zake after that nkajifunza kuzitambua ilifika stage akawa anantel Mungu husema nami kupitia ndoto kuna siku nikiwa chuo juzi kati tu hapo nilishtuka kweny ndoto usiku kama saa tisa hivi ilikuw ikimuhusu marehem K(movie star) kuwa amekufa tena ile ya gafla nilivo stuka sikupata usingizi tena yani ukawa hauji nkamshtua mate wangu nkamtel abt ndoto akasema kaka unazngua hizo ishu hazipo bt nilikuw na hisia kwamba hilo tukio limetokea and kufika asubuh inatangazwa kweli jamaa alinishangaa sana.
Pia kuna hichi kitu cha kuona matukio kama yana jirudia naweza kaa na washkaji we talk then mind ikasem imewah hapen.sas nikiwambia tu kam imejirudia hushangaa n wakiniask wat will be next hapo niksema mambo yanakuw sio same ila nikikaa bila kuwambia kila kinaenda the same kama vinajirudia yani
Pia hata hii ishu ya wiling huwa inatokea nikisema ktu nikiw na strong will huenda the way i want
nikaja gundua.kuwa nikiwa mtu muongeaji sana hile strong willing inapotea.
Ila kwa sas huu huwezo umepungua sijui kwa nin yani.hebu mwongozo tafadhari
 



Hiyo inaitwa Clairvoyance, but inawezekana una Precognition, mkuu ... Hata mimi nipo nayo, na tangu nimeanza kusoma uzi huu umenisaidia kujitambua zaidi ...!! Tuendelee kupata darasa toka kwa Pasco ..!!!
 
Kuna ile hali ya mtu kila anapotulia anakuwa anafikiria mambo mazuri yajayo mbele yake(yaani anakuwa anawaza mafanikio makubwa tu katika maisha yake hapo badae), Je aki Concentrate kwa kile anachokiwaza anaweza kufanikiwa? Pia, Je Hayo mawazo ni ya Kuigiza tu au yanahusiana vp na Psychic powers.

Pia eti niliwahi kuambiwa kuwa 'Siku zote mtu anayewaza kupata Bahati/Mafanikio katika maisha yake kwa Fikra inakuwa ni Ngumu kwa yeye kuja kufanikisha kile anachokiwaza! Je hii ni kweli?
Msaada wakuu,maana hii dhana huwa inanigusa sana kwani mda mwing ninakuwa na hizi ndoto zczo na ucngz. Baadh walinifafanulia wakisema ninafaa kuwa muigizaji wa sanaa!

Sent from my BlackBerry 8520 using Jamii Forums
 

Huyu ni mwingine mwenye nguvu hizi

Nimeishamshauri cha kufanya!,

Pasco.
 
Watanzania ni waajabu sana. Mnapend spoon feeding. Hakuna jipya hapa kwa mwenye ufahamu.

Ndio maana nimesema kuna watakaosoma lakini hawataelewa,wengine kama nyie mnaotaka jambo jipya,hakuna jipya duniani,vitu vinajirudia tu sema katika njia tofauti,changamoto tofauti,watu tofauti,mazingira tofauti.pasco hajasema ni maarifa mapya,bali yalikuepo hata kabla ya hizi dini za ukristo au uislamu zilizoanza juzi tu.hizi taarifa ni kama dhahabu lazima uchimbe chini uipate na unaweza kuuza vitu vyako vyote ili uipate kwani ukishaipata ina thaman kuliko ulivyoviuza
 
Nimesoma page zote 45, baadhi ya hizo:- zinafurahisha, zinahuzunisha, zinakera, zinaburudisha, zinaboa pia ZINA ELIMISHA

Nadhani nimepata mwangaza kidogo wa safari ya basi hili ni la wapi?, ngoja nione!

Aaah! kama sio au nilisikia vibaya, si mbaya ntashuka tu kimya kimya japo ntakua nimepoteza muda na nauli.

Endeleeni wakuu mi natazama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…