Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Mkuu umeuliza maswali mazuri,
Niwaombe mods waruhusu chalenge kwa pasco na wafuasi wake tusijenge Taifa la ndio mzee

Tatizo Pasco anajificha kwenye kivuli cha dini. Kwamba kila anayehoji asili ya nguvu hizi anaendekeza udini, bali yeye haoni kuwa anafundisha ushirikina kwa kutumia Biblia Takatifu. Yaani apotoshe maandiko halafu tumtazame tu. Shetani huwa haanzishi jambo jipya bali ana-twist maandiko.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Eiyer, nakuomba sana usilazimishe mambo!, hapa sio nyumba ya ibada!, naomba tufanye appontment kule jukwaa la dini, nikupige somo!, usijekujikuta na wewe ndio hao wamuabidia shetani aliyejidisguised kama Mungu, ndio maana unababaika sana!. Issue ya shetani aliumbwa na nani usiifanye a very big deal!, nilikuuliza huko nyuma, jee unaujua mwanzo wa Mungu?!, jee unaijua source of powers za Mungu?!, Jee unaujua mwanzo wa shetani?!, kama ulifundishwa kuwa shetani aliumbwa na Mungu, na ndiye aliyempa hizo nguvu za kushetani tufuindishi na sisi tujue!. Nilikuuliza baada ya shetani kuasi kule kwa Mbinguni, jee unajua ni kwa nini Mungu hakumuangamiza?!. Jee unajua Mungu alituumba sisi binadamu kwa mfano wake?!, jee huyo shetani baada ya kumdanganya mama Yetu Eva na kumshawishi kumuasi Mungu!, unajua alifanywa nini?!. Baada ya Kaini mtoto wa kwanza wa Eva, kumuua ndugu yake Abeli, unajua alifanywa nini?!.

Kwa maana hiyo jinsi Mungu aliupenda ulimwengu, hadi akamtoa mwanaye mpendwa wake anayependezwa naye kuja kuuokoa ulimwengu from what!, yaani huyu shetani ni nani haswa hadi Mungu kumtoa kafara mwanaye?!, kwa nini asingemuangamiza shetani na yote yakaisha!.

Nakushauri kwa mambo usiyoyajua ukidhani unajua, bora jikalie kimya, acha watu tufungulie watu milango ya kumtambua shetani na kumuepuka!, huku tukiwaacha watu mliojifungia katika box la shetani, akiwaaminisha yeye ndio Mungu, huku mkiamini!, bila kuwa elightened!, utajikuta unamtumikia shetani bila kujijua!.
Sio lazima kuchangia, fuatilia tuu uzi huu ukifunguka, utakuja kunishukuru nimekuokoa!.
Kipimo cha kwanza kwa wanaomwabudu shetani bila kujijua, Yesu wa ukweli akitajwa, watataka kukuzuia usimtaje!. Huyo Roho Mtakatifu mnaotaka kuzuia tusimtaje ndio hizo powers zenyewe na kufanya kila kitu!, neno Roho Mtakatifu likiwa ni jina tuu, the essence is powers!.
Nitamtaja Mungu!, Nitamtaja Yesu, Nitamtaja Roho Mtakatifu kwa ajili ya wale waaminio, na kwa kwa wasio waaminia, nitawaruhusu kuitumia imani yoyote wanayoiamini kuifungua milango ya "powers from within!".
Pasco!.

Kutokana na Usomaji wangu wa Biblia, Mungu anamjibu Mussa 'Mimi niko ambayo niko'. Pia Yesu ktk Ufunuo anasema 'Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho'. Hivyo basi mwanzo wa Mungu haujulikani na hakuna Mwanadamu ajuaye ila kama wanafunzi wa Yesu wangemwuliza Yesu mwanzo wa Shetani kipindi akiwa Malaika angewapa jibu sahihi kwa sababu kila tunachokiona na tunachokisikia hiko kimeumbwa na Mungu, sasa wewe sijui una maana gani unaposema mwanzo wa Mungu ndio mwanzo wa Shetani, uko wrong kabisa.

Mkuu Pasco Mungu maandiko yanasema alituumba kwa mfano wake akimaanisha kuwa yeye ni Roho, na mwanadamu ana Roho pia. Lakini sio uweza sawa Mungu, kama kweli hizo Power zipo embu nihakikishie kwa kuniumbia kitu kilichohai kwa mfano mmea, mnyama au mwanadamu. Kama hakuna usiseme tuna Uungu ndani yetu, Mwanadamu kapewa mamlaka tu hapa duniani, na mamlaka haya shetani aliyakosa yaani hakupewa na Mungu hivyo akaona wivu kwa wanadamu.
Mungu hakumchagua Yesu aje duniani ila Yesu ndie aliejipendekeza aje duniani.
Hakuna Mkristo ambae anaweza kukubali kuwa chini ya hizi nguvu, kama unaamini mwanadamu anazaliwa na dhambi ya asili, je hiyo dhambi ni Mungu ndie anaeiweka kama hizo Power???
 
Tatizo Pasco anajificha kwenye kivuli cha dini. Kwamba kila anayehoji asili ya nguvu hizi anaendekeza udini, bali yeye haoni kuwa anafundisha ushirikina kwa kutumia Biblia Takatifu. Yaani apotoshe maandiko halafu tumtazame tu. Shetani huwa haanzishi jambo jipya bali ana-twist maandiko.
Pasco anatumia biblia hiohio unayotumia wewe na kwa madai yake ni mkristo safi kama wewe.
Sasa badala ya kumu attack yeye unachotakiwa ni kuleta point za ku challenge anayoyasema!

Kumshambulia yeye binafsi kunaonyesha udhaifu wako ktk kulijua andiko.lako mwenyewe!
Sisi hapa tusiokuwa wakristo tunaangalia movie! Tuone starring atakufa saa ngapi!?
Teh teh teh teh teh.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo Pasco anajificha kwenye kivuli cha dini. Kwamba kila anayehoji asili ya nguvu hizi anaendekeza udini, bali yeye haoni kuwa anafundisha ushirikina kwa kutumia Biblia Takatifu. Yaani apotoshe maandiko halafu tumtazame tu. Shetani huwa haanzishi jambo jipya bali ana-twist maandiko.

Ndio maana hata Pasco anadai kuelewa Biblia ni powers.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Eiyer, nakuomba sana usilazimishe mambo!
Nimelazimisha mambo gani?
, hapa sio nyumba ya ibada!,
Who said so?
naomba tufanye appontment kule jukwaa la dini, nikupige somo!,
Kwanini?
Naanza kuapta wasiwasi na uwezo wako wa kuelewa
Napata wasiwasi kwasababu nashindwa kuelewa ni kwanini unashindwa kuliona tatizo lililoko kwenye mada yako
Alietakiwa kwenda huko kwenye hilo jukwaa ni wewe pamoja na hii mada yako na sababu nimezieleza hapo kwenye post yangu uliyoi quote,au hujaisoma?

Unaponiambia nalazimisha mambo bila kusema ni mambo gani na bila kueleza vile ninavyolazimisha mambo utaonekana ni kituko tu
Pia sio mimi peke yangu niliekuambia hayo,lakini ajabu huelewi
usijekujikuta na wewe ndio hao wamuabidia shetani aliyejidisguised kama Mungu,
Hili ni sehemu ya mada yako?
ndio maana unababaika sana!.
Kubabaika maana yake nini?
Nimebabaika wapi?
Issue ya shetani aliumbwa na nani usiifanye a very big deal!,
Wewe huoni kama ni big deal?
Hujui umuhimu wa kumjua shetani kwenye imani ya Kikristo?
Au wewe ulikua unaandika ukidhani ni kitu kidogo sana?
Unazidi kuonesha namna usivyojua mambo
nilikuuliza huko nyuma, jee unaujua mwanzo wa Mungu?!, jee unaijua source of powers za Mungu?!,
Utaendelea kushangaza kama utakuwa huelewi uzito wa haya unayoongea hapa
Na nakuambia huenda kukawa kuna watu walikuwa wamevutiwa na hii mada yako na watakapoona unazungumza mambo kama haya watagundua tu kuwa hayo uliyoandika hapo hukutoa kichwani mwako kwa kutafakari bali umekopi mahali tu

Unaulizaje kuhusu kuhua mwanzo wa Mungu na nguvu zake?
Hivi unamjua Mungu wewe?
Unaweza kumtafakari akaweza kuenea kwenye mawazo yko yenye ukomo?

Hebu niambie huo mwanzo wa Mungu ni upi ili uwe umethibitisha kuwa alisema uongo aliposema hana mwanzo wala mwisho.tuambie hicho chanzo cha nguvu za Mungu ili wewe uwe ndie Mungu

Usichokijua ni kwamba unayosema na kujidai kufundisha hapa ni pure satanic na wewe hujui tu au unaamua kudanganya kwa makusudi

Dhana ya kutaka kufanana na Mungu aliianzisha shetani mwenyewe huko mbinguni na wewe unaiendeleza hapa kwakudai kujua mwamnzo wa Mungu na nguvu zake

Trust me hutakaa ujue na haitatikea binadamu yoyote akajua mwanzo wa Mungu wala nguvu zake kwakuwa hazina mwanzo na yeye ni zaidi ya huo mwanzo

Ni sawa na kijiko kitake kijue mwanzo wa aliyekitengeneza,inawezekana hilo?
Japokuwa aliyekitengeneza kijiko ana mwanzo lakini kijiko hakiwezi kuujua,sijui wewe kutaka kujua mwanzo wa asiyekuwa na mwanzo utaujuaje
Jee unaujua mwanzo wa shetani?!,
Simple,
Aliumbwa na Mungu
kama ulifundishwa kuwa shetani aliumbwa na Mungu, na ndiye aliyempa hizo nguvu za kushetani tufuindishi na sisi tujue!.
Nishakujibu tayari
Nilikuuliza baada ya shetani kuasi kule kwa Mbinguni, jee unajua ni kwa nini Mungu hakumuangamiza?!.
Kwani hujui ni adhabu gani Mungu aliyomuandalia?
Kwanini wewe unadhani alitakiwa amuangamize?

Hujui kuwa Mungu hakuona busara kuwa dikteta?
Ile haki yake ya kuishi aliendelea kumpatia na huo ndio upendo

Lakini pia hujui kuwa unajikinza?
Wewe ulisema hapa kuwa shetani hakuumbwa na Mungu,sasa Mungu atakuwaje na mamlaka ya kuangamiza ambacho hata hakuhusika na mwanzo wake?
Hayo mamlaka aliyatoa wapi?

Nilikuuliza maswali kuhusiana na hili lakini hukujibu
Jee unajua Mungu alituumba sisi binadamu kwa mfano wake?!,
Najua hilo

Halafu wakati mwingine naona unauliza maswali ambayo hata sijui na sioni mantiki yake iko wapi
Au unauliza tu bila kujua lengo la swali lako?
jee huyo shetani baada ya kumdanganya mama Yetu Eva na kumshawishi kumuasi Mungu!, unajua alifanywa nini?!.
Hakuna alichofanywa
Tayari adhabu yake ilishaandaliwa tangu mwanzo na ni hiyo hiyo wafuasi wake watakayoipata pamija nae
Kilichoadhibiwa ni kile kiumbe ambacho shetani alitumia umbo lake kumuendea Hawa na kumdanganya pamoja na binadamu aliekubali kudanganywa
Baada ya Kaini mtoto wa kwanza wa Eva, kumuua ndugu yake Abeli, unajua alifanywa nini?!.
Narudia tena haya maswali yako hayaeleweki lengo lake
Huenda ukiniambia leng lake kwenye mjadala huu na maswali niliyokuuliza naweza kupata hamu ya kukujibu
Kwa maana hiyo jinsi Mungu aliupenda ulimwengu, hadi akamtoa mwanaye mpendwa wake anayependezwa naye kuja kuuokoa ulimwengu from what!,
Sababu si umeiandika mwenyewe hapo juu?
Au umesahau?
yaani huyu shetani ni nani haswa hadi Mungu kumtoa kafara mwanaye?!,
Your mixing things here
Sababu ya Mungu kumtoa mwanae wa pekee sio shetani bali ni upendo wa Mungu kwa binadamu
Wewe ni mkristo kweli?
kwa nini asingemuangamiza shetani na yote yakaisha!.
Hili swali linaonesha wewe hujui ukristo kabisa
Halafu aina la hili swali lineulizwa na atheist ningeelewa,lakini linapoulizwa na mtu anaesema kuwa yeye ni mkristo napata wasiwasi na maelezo yake na nina kila sababu ya kumuita mpinga kristo

Kuhusu sababu ya Mungu kutokumuangamiza shetani nimekujibu hapo juu
Soma
Nakushauri kwa mambo usiyoyajua ukidhani unajua, bora jikalie kimya, acha watu tufungulie watu milango ya kumtambua shetani na kumuepuka!, huku tukiwaacha watu mliojifungia katika box la shetani, akiwaaminisha yeye ndio Mungu,
Sitaki ushauri wako
Anza wewe kujishauri kwanza

Hakuna unachokijua kinachoweza kumpeleka mtu mbali na shetani badala yake wewe unawasogeza watu karibu na shetani

Hivi mtu unasema kuwa nguvu inayotumika kufanya mabaya na mema ni ileile ila inapotumika kutenda maovu huhesabika kama shetani na inapotumika kutenda mema inahesabika kuwa ni Mungu unakuwa unawasogezaje watu mbali na shetani?

Ndi maana nakuambia ushauri wako kaa nao mwenyewe
huku mkiamini!, bila kuwa elightened!, utajikuta unamtumikia shetani bila kujijua!.
Hizi trick zako tunazijua
Huko kuwa enlighted sikutaki na sitakutaka hata Illuminati nao hudai hivyo
Huo mwangaza wako kaa nao mwenyewe
Wewe unachokifanya wewe ni kuwafanya watu wamtumikie shetani kwa uhakika kabisa
Sio lazima kuchangia, fuatilia tuu uzi huu ukifunguka, utakuja kunishukuru nimekuokoa!.
Nilichokifanya na ninachokifanya mimi na wengine kuwafunulia watu udanganyifu wako na wapo waliokuja kushukuru hapa
Acha danadana
Kipimo cha kwanza kwa wanaomwabudu shetani bila kujijua, Yesu wa ukweli akitajwa, watataka kukuzuia usimtaje!.
Yesu wa kweli ni Yupi?
Ana sifa gani?
Huyo Roho Mtakatifu mnaotaka kuzuia tusimtaje ndio hizo powers zenyewe na kufanya kila kitu!,
You may be right here,lakini usichokijua wewe ni kuwa unadhani kuna nguvu zinazotumika tu hovyo hovyo biula kutumia kanuni

Huyo anaitwa Roho mtakatifu,maana yake ni takatifu,smoja kati ya sifa kubwa ya kitu kitakatifu ni kuwepo palipo patakatifu

Sasa wewe unadai kuwa mtu yoyote anaweza kuitumia hiyo nguvu,yaani haijalishi kama ni mtakatifu ama laa yaani mtu wa imani yoyte ile anaweza kuitumia hiyo nguvu
Hapo umedanganya sana
Njia pekee ya binadamu kuwa mtakatifu ni kusafishwa kwa damu ya Yesu kwa kumkiri Kristo kuwa mwokozi wake na kuacha dhambi,sasa hao walioko kwenye imani zisizokubaliana na hayo na wala huyo roho mtakatifu watawezaje kuitumia?

Ni sawa utake kuupitisha umeme kwenye kamba ya katani,itawezekana kweli?
neno Roho Mtakatifu likiwa ni jina tuu, the essence is powers!.
Nguvu gani zinazotumika bila utaratibu?
Humu duniani kuna nguvu zinaoendana na kutokuwa mtakatifu na kuna nguvu zinazoendana na kuwa mtakatifu,na nguvu hizi zina vyanzo tofauti kulingana na hizo sifa[utakatifu na kinyume chake]
Hivyo napenda kuwaambia wana JF kuwa wasijidanganye kuwa hata ukitoka kuzini huko unaweza tu kuzitumia nguvu za Mungu kwa kupitia roho mtakatifu

Kama kutakuwa na nguvu unayoitumia hiyo itakuwa ni ile inayoendana na huo uchafu wako[shetani]
Nitamtaja Mungu!, Nitamtaja Yesu, Nitamtaja Roho Mtakatifu kwa ajili ya wale waaminio, na kwa kwa wasio waaminia, nitawaruhusu kuitumia imani yoyote wanayoiamini kuifungua milango ya "powers from within!".
Go on brother,i can not stop you because i don't have that authority
Lakini huyo mwenye hizo nguvu na mamlaka unazozipotosha hapa iko siku na saa atakuzuia na utazimika kama umeme wa tanesco
Kuwa makini sana
Mungu wetu wa mbinguni akuhurumie!
 
Pasco anatumia biblia hiohio unayotumia wewe na kwa madai yake ni mkristo safi kama wewe.
Sasa badala ya kumu attack yeye unachotakiwa ni kuleta point za ku challenge anayoyasema!

Kumshambulia yeye binafsi kunaonyesha udhaifu wako ktk kulijua andiko.lako mwenyewe!
Sisi hapa tusiokuwa wakristo tunaangalia movie! Tuone starring atakufa saa ngapi!?
Teh teh teh teh teh.

Tayari tumeshafanya hivyo
Mathay 7:1 inasema "Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi."
Kwa nini inasema hivyo. Mstari unaofuata (ambao kwa kutojua au makusudi umeuacha) unasema "Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa."

Kwa hiyo mstari huu unaonge hukumu ya kinafiki a sio hukumu ya kweli kwa kuwa Yesu mwenyewe alihukumu, Yohana Mbatizaji akahukumu na mitume wote walihukumu so..!?

Biblia haiko vague juu ya nani ataenda mbinguni. Kila aliitae jina la Bwana ataokoka. Kwa hiyo hata kama Hitler aliliita jina la Bwana haitakuwa ajabu kumkuta mbinguni! Mungu si Pasco wala Mtangoo
Nahisi una matatizo fulani wewe! Yaani huoni ni kwa jinsi gani andiko hili limeuhusisha Ukristo moja kwa moja na ushirikina? Hebu ona hiyo nukuu ya Pasco hapo juu halafu ulete ubishi wako tena. Jifunze kusoma between lines.



Narudia tena, kufuatia ushuhuda alioutoa Pasco katika maandiko yake humu jamvini, hastahili kujiita mkristu. Kabla sijaja kwenye swala lako la kuhukumu (kichaka cha waovu), nitakueleza mkristu ni nani;

Wakati unadhani kwamba kuwa mshirika wa kanisa fulani (mf. Katoliki) ni kuwa mkristo, ukweli ni tofauti kabisa. Wakristo wote wamo katika kanisa ya Yesu Kristo, lakini si kila mshirika wa kanisa ni mkristo. Hawa ndio wakristo wanaokusudiwa na biblia takatifu:

Mathayo 28:19 ..... Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.......

Yeyote anayefanyika mwanafunzi wa Yesu Kristu kwa kushika yale yote aliyoagiza huyo ndiye mkristo. Hebu soma tena:

Matendo 11 : 26 .....Hapo Antiokia ndipo waamini waliitwa 'wakristo' kwa mara ya kwanza.

Kumbe kuhudhuria kanisani, au kujitangaza wewe ni mkristo haitoshi hata kidogo, bali msingi wa ukristo ni kuyaishi mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Kuhusu kuhukumu:
Andiko hili linatoka katika injili ya Mtakatifu Mathayo 7 : 1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
Andiko hili limekuwa likitumika kama kichaka cha watenda maovu kukwepa kurudiwa. Na hii inafuatia tafsiri potofu kabisa, nje ya kile Kristo alichokikusudia. Kwa nini?

Kusudio la Kristo hapa ni kwamba usihukumu kama wewe mwenyewe hauko safi. Kwa lugha nyingine ni sawa na kusema, usihukumu wengine, vininevyo na wewe uwe tayari kuhukumiwa nao. Ndio maana mstari unaofuatia unasema:

2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa

kwamba ukimwambia mwenzio aache wizi hali wewe pia ni mwizi, atakuhukkumu kwa hukumu hiyo hiyo, au ukimshambulia mwenzio kwa kosa la uzinzi wakati wewe pia ni mzinzi, atakugeukia wewe pia. Hivyo unapomhukumu mwenzako wewe pia uwe tayari kuhukumiwa.

3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?


Hapo maana yake safisha kwanza mwenendo wako ndipo uwe na moral authority ya kunyooshea kidole wengine. Ni sawa na Papaa Msofe aanzishe kampeni ya kupinga utapeli, wakati watu wengi wanamchukulia yeye ni tapeli aliyekubuhu.

5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Na hiyo red ndio msingi mkuu wa fundisho hili, kuacha unafiki. Ndio maana anamalizia kwa kusema itoe kwanza boriti... ndipo umtoe na mwenzako kibanzi. Hivyo haijakatazwa kwa namna yoyote ile. Tunapaswa kuikemea dhambi ili shetani akimbie. Kufundisha vinginevyo ni kuwapoteza wana wa Mungu.

Kwenye hoja:

Alichokifanya Pasco ni kumkana Kristo wazi wazi. Kusema Jina la Yesu halina nguvu yoyote kuponya bali ni nguvu iliyo ndani yako ni kumtupa nje Kristo. Sasa kama bado unabisha itakuwa ni tatizo lako binafsi.




Nadhani kilichoandikwa kimejibu swali hili



Hapa nakuchalenji soma biblia, ni swali basic sana hili.
 
Duh somo zuri sana hili Pasco, nilikuwa sijaliona na ndio nimeifuma hii thread leo....
Tupo pamoja mkuu, nimeongeza maarifa leo hususan maoni ya wachangiaji wenye uelewa wa taaluma hii.....
 
Last edited by a moderator:
Pasco worships a strange god. The god that have beginning is no god at all.
Its just a human being, may be a demigod or something mythical of that kind.
The god Pasco worships is not worthy of single of my worship.
The god Pasco worship is close to Mormon god than a Christian God
So Pasco is worshipping something than God of Christianity. So the argument goes:

"Christians worship God of the Bible.The God of the Bible permits worship of no other god. Pasco worships another god. So Pasco is not a Christian"
 
Last edited by a moderator:
Hivi Eiyer ni kwa nini mara nyingi ukiulizwa swali ambalo wengi tunasubiria jibu ni lazima useme "Narudia tena haya maswali yako hayaeleweki lengo lake
Huenda ukiniambia leng lake kwenye mjadala huu na maswali niliyokuuliza naweza kupata hamu ya kukujibu"??

Tahadhari: maswali kama "mara nyingi ni nini?", wengi ni akina nani?" sitayajibu.
 
Mkuu Pasco huwezi kumlinganisha Mungu na shetani kwa namna yoyote ile huo ni ukengeufu eti unatofautisha kwa Kusema shetani hawezi kuumba!
Ukisoma kitabu cha Isaya 14:12-14 Hasa kale kamstari Ka Mwisho! Shetani anasema " I will be like most High"
Hapa shetani anajilinganisha na Mungu na Wewe Unatofauti gani na shetani kwa kumlinganisha na Mungu?
Acha bhana mambo yako

Na pia Ukisoma kitabu cha ufunuo 12:7-9 Utaona Michael na malaika wake Ndio aliopambana na joka na si Gabriel Kama ulivyoandika!

Utumiapo mafungu ndani ya bible yatumie vizuri kwani ata shetani ana nguvu na ni Mjuzi Wa maandiko!
Kumbuka alivyo mjaribu Eva pale bustanini na kumdanganya kwa kutumia maneno ya Mungu na kugeuza kidogo tu!

Na pia Yesu nae alijaribiwa Na na shetani kwa kutumia maandiko hayo hayo!

Na Wewe Leo unatumia maandiko haya haya kupotosha na kuleta mafundisho ya kumlinganisha Mungu na shetani!
 
Mkuu Bona, hili ni swali la msingi sana, kuna wanaojua sana dini humu, lakini hawajibu!. Ukijibu wanakuja juu!.
Sambamba na swali hili, dini zote hawaruhusiwi kuuliza Mungu ni Nani?, wala kuuliza mwanzo wake!, wala hawaulizi Roho Mtakatifu ni nani, wala hawaulizi mwanzo wake!.
Hili linaweza kuwa sawa
Inawezekana kukawa na dini kama hizo,lakini usichanganye dini na vitabu vya dini
Kitabu kinaweza kusema tofauti na waumini na viongozi wakawa wanafanya tofauti
Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, kulikuwepo na Powers, hizo powers ndizo Mungu. Hana mwanzo, hana mwisho, yeye ni Alfa na Omega!.
He!!!!!
Wewe si ndio ulikuwa unataka kujua mwanzo wa Mungu?
Iweje tena useme hana mwanzo wala mwisho?
Huyu Mungu alikuwa na wasaidizi, waitwao Malaika, kati ya malaika hawa, malaika Mkuu kabisa kuliko wote, mwenye madaraka makubwa karibu kabisa na Mungu, aliitwa Luciferi. Huyu alikuwa na karibu nguvu zote sawa na Mungu, ila alikosa nguvu mbili tuu, Uumbaji, na Utoaji Roho!.
Hii umeitoa wapi?
Yaani Lucifer kama malaika Mkuu,
Ndio maana nakuambia wewe ni mpotoshaji kabisa
Ni wapi pameandikwa kwenye biblia kuwa Lucifer alikuwa malaika mkuu?
Au haya maelezo hujayatoa kwenye biblia?
alikuwa na uwezo wa kufanya kila Mungu anachofanya, isipokuwa hakuwa na uwezo wa kuumba, wala kutoa roho!. Malaika wa tatu kwa ukuu aliitwa Gabriel!, wa nne Mikaeli, malaika wote waliobakia hawakutajwa kwa majina!.
Hivyo viwango vya fulani alikuwa wa tatu na sijui nani wa ngapi umevitoa wapi?
Hivyo ambavyo shetani alivyoweza kuvifanya ambavyo Mungu alivifanya ni vipi?
Hivi wewe unaona unavyompa shetani ukuu fake hapa?
Hakuna mahali popote palipoelezwa Mungu aliwaumba hawa malaika akiwemo Luciferi!.
Kama huji jambo ni bora ukauliza uambiwe
Yoh 1:3
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

Kol 1:16-18
16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.

Hivyo huu uongo wako kaa nao mwenyewe
Hivyo mwanza wa Mungu ndio mwanzo wa Malaika!
.
Huu uongo wako kaa nao mwenyewe nimeshakuambia hivyo!
Malaika huyu Mkuu, Lusiferi, akaendesha uasi mbinguni kwa kuandaa jeshi la malaika kutaka kuyatwaa madaraka ya Mungu, baadhi ya malaika ambao ni watiifu kwa Mungu wakiongozwa na Gabrieli, hawakukubali kuasi!. Vikapiganwa vita kati ya jeshi la Mungu na jeshi la Luciferi, jeshi la Lusiferi likashindwa, hivyo ndivyo Lusiferi akapewa jina la shetani!, akatupwa duniani kuja kutafuta wafuasi!. Haikuelezwa popote kama alinyanganywa hizo nguvu!.
Kwanza ni nguvu gani anazo?
Alizitoa wapi?

Halafu umetoa wapi kuwa shetani alikuwa malaika mkuu?
Huo ukuu aliutoa wapi?
Shetani aliumbwa kama malaika mtakatifu (haikusema aliumbwa na nani), Isaya 14:12 inampa Shetani jina kabla aanguke kuwa nyota ya alfajiri. Ezekieli 28:12-14 inamwelezea Shetani kuwa, aliumbwa awe kerubi, kawaida malaika mkuu. Aligeuka na kuwa mkali kwa ajili ya urembo wake na cheo chake na akaamua kuwa aketi kwenye kiti kilicho juu ya Mungu (Isaya 14:13-14; Ezekieli 28:15; 1 Timotheo 3:6). Kiburi cha Shetani kilimfanya aanguke. Kumbuka usemi wa wengi "nita" katika Isaya 14:12-15. Kwa sababu ya dhambi zake, Mungu alimfukuza Shetani kutoka mbinguni na kumtupa duniani!.
Nimeshakuonesha hapo juu kuwa shetani aliumbwa na nani
Acha uongo kuwa haikusemwa aliumbwa na nani
Shetani akawa kiongozi wa ulimwengu na mfalme wa anga (Yohana 12:31; 1 Wathesalonike 3:5), na mwongo (Mwanzo 3; 2 Wakorintho 4:4; Ufunuo Wa Yohana 20:3). Jina lake linamaanisha Mwenye "majanga" au "mpingamizi." Majina yake mengine ni, Ibilisi kumaanisha "mdanganyaji."
Kwanini husemi kuwa utawala wake ni wa muda?
Hata kama alifukuzwa kutoka mbinguni, bado anazidi kujinua kiti chake juu ya Mungu.
Kuzidi Mungu?
Una hatari wewe sio kidogo

Unamjua Mungu wewe?
Anayageuza yale Mungu anayafanya,
Unayajua ya Mungu wewe?
Umeyapimaje ukajua ameyafanya?

Again,unamjua Mungu wewe?
Yaani elimu yako ndogo kumhusu Mungu unakufanya umfanye Mungu kama vile kikaragosi cha kuja hapa JF na kumlinganisha na shetani ambae hata kule kumlinganisha na Mungu tu ni matatizo
akitumaini kuabudiwa na ulimwengu na anatia tumaini kwa pingamizi zote za ufalme wa Mungu.
Hiki tumekisoma kwenye makala za devil worshipers mara mia kidogo
Unadhani unaleta kitu kipya hapa?
Shetani ndiye ako nyuma ya dini zote za uongo na dini za dunia akijipretend ni Mungu!.
Dini ni nini?
Shetani atafanya na kila kitu katika uwezo wake ili ampinge Mungu na wale wote wanaomfuata. Ingawa hatima ya Shetani imewekwa muhuri kuwa tanuru la moto milele (Ufunuo Wa Yohana 20:10).
Hivi wewe unadhani unazungumza na watoto hapa?
Atachomwa na nani wakati hana mwanzo?

Huyo atakaemchoma atafanya hivyo kwa mamlaka ya nani?
Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kimeweka sheria zote na jinsi ya kuabudu!.
Sheria ni nini?
Kuna dini nyingi duniani zinamwabidu shetani bila masikini waumini kujua!.
Na wewe ni mmoja wao
Ukijisomea Bibilia Takatifu, huku umetulia, utafunuliwa tuu na kuijua kweli,
Ambayo wewe unaipinga
hivyo kama uu miongoni mwa waabudu shetani bila kujijua, utafunguka na unaweza kuamua kubadilika, au kuendelea kuabudia nyumba za Ibada zile zile, huku moyoni mwako unamwabudu Mungu wa Kweli!.
Hakuna ushirika kati ya nuru na giza wewe
Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano wake, akatupulizia pumzi ya uzima ambayo ndio source ya hizi nguvu tulizo nazo za kutenda mema, na miujiza na kutenda kila kitu!. Kwa vile shetani naye yuko duniani, naye ananguvu na kufanya kila kitu,
Wewe si umesema hawezi kufanya kila kitu?
[QU OTE=]ila kwa lengo la kupoteza wana wa Mungu!.[/QUOTE]
Hawezi
Kuna wakati huwa anazungumza hata na Mungu kabla ua kuleta majanga na huwa anapata kibali cha kufanya hayo majanga mfano ni kwa Ayubu!.
Anaendaje kuomba kibali kwa ambae hakuhusika na mwanzo wake?
Hoja zako ni za kitoto na hazina mashiko
Hata Yesu alipokuja duniani, kuna wakati Shetani alimjaribu.
So what?
Katika nguvu tulizopewa na Mungu, pia tumepewa uwezo wa kujitambua na kuzitambua hilo zote za shetani. Bila kuwa na uwezo huu, unaweza kabisa kujidhania unamwabudu Mungu wa kweli, kumbe sivyo, bali unamwabudu shetani, ibilisi na mwisho wa siku, utateketezwa nae kwenye jehanum ya milele!.
Kwaniniusitafute kitu kingine cha kufanya ukaachana na hii mada yako ya kitoto?

Umeshindwa kutueleza mwanzo wa shetani kwa ufahamu wako halafu unatuambia kuwa sisi tumepewa uwezo wa kutambua hila za shetani na ambae hata hakuhusika na uwepo wa shetani

Kwako hii ni sawa?

Hujui kuwa anaetengeneza pikipikindio anaeamua pikipiki hiyo iwe na uwezo gani na pia anaweza kuamua pikipiki moja ikawana uwezo kuliko nyingine?

Hujui kuwa kama wewe huhusiki na hayo huwezi kuyaamua hayo?
Kwa vile Mungu ni onmipresence, vivyo hivyo shetani naye ni omni present!,
Tabia yako ya kuzungumza mambo bila ushahidi watu watakuona kama vile unapiga story za kwenye kahawa na kashata tu,huna ushahidi wowote
binadamu wote ambao hutenda mema, hutumia nguvu za Mungu, na wote watendao maovu hutumia nguvu za shetani!.
Hadi unatia uvivu
Hujui umeanzisha mada inayohusu nini na hujui hata kwenye mada hiyo umeandika nini

Kwa kifupi mada uliyoanzisha inaonekana hukuiandika wewe na hujui chochote kuihusu
Huwezi kuandika mambo yanayojikinza
The dividing line between nguvu za Mungu na nguvu za shetani is very thin!, the only diference ni Nguvu za Mungu ni freely na unconditional, hazina masheri yoyote zaidi ya kuamini tuu!. Nguvu za shetani ni conditional, kwamba uli zipate lazima ufanye hiki, na kile!.
Umejuaje haya?
Umeyatoa wapi?
Mafunzo ninayoyatoa humu ni free, freely na unconditional, na nguvu hizo wote tunazo ila tuu hatujaziamsha!.
Hakuna aliekuambia uwatoze
Usikute hata hizi juhudi zinazoendelea humu watu kuogopa zisifunuliwe, inaweza kabisa kuwa ni kazi ya shetani, nawahakikishia zitashindwa!, watu watafunuliwa na watatenda miujiza!.
Unadhani shetani anadhihirika kwa vitisho kama vyako hivi?

Tunajua namna ya kuzijua hila zake kwa kupitia neno la Mungu!
 
Hivi Eiyer ni kwa nini mara nyingi ukiulizwa swali ambalo wengi tunasubiria jibu ni lazima useme "Narudia tena haya maswali yako hayaeleweki lengo lake
Huenda ukiniambia leng lake kwenye mjadala huu na maswali niliyokuuliza naweza kupata hamu ya kukujibu"??

Tahadhari: maswali kama "mara nyingi ni nini?", wengi ni akina nani?" sitayajibu.

Inawezekana hujui nii faida ya kuuliza
Kuuliza ni matokeo ya kutokuelewa au ni kutaka kujua aliyesema kitu fulani anakijua

Mfano ninapokuuliza "Mara nyingi maana yake nini" lengo langu ni kutaka kujua kama unajua maana ya mara nyingi au ulikurupuka tu kuandika hivyo maana huenda hata nikikudai ushahidi wa hiyo mara nyingi unayodai nimejibu hivyo huenda ukawa huna sasa kama hukukurupuka ni nini?

Tena ni muhimu nikuulize "Lazima ni nini" kwakuwa umesema ni lazima nijibu hivyo
Maelezo yako yataniridhisha sababu ya wewe kusema hivyo na sio mimi ku assume tu kuwa unajua maana yake

Sasa nakuuliza ili nijiridhishe kama ulikuwa unajua hata ulichokuwa unaniuliza
Ni wapi nimejibu mara zote kwa jibu ulilolisema hapo kwenye maelezo yako?
Kwanini umesema mara nyingi?
Mara nyingi ni nini?
Na kwanini umesema ni lazima?

Kama hutajibu maswali haya utakosa umuhimu wa kujibiwa maswali yako kwa sababu inaonekana hujui ulichouliza,kama hujui ulichouliza utajuaje jibu sahihi kwa maswali yako?

Kama hutajua majibu sahihi basi kuna uwezekano wa maswali yako kutokuwa sahihi!
 
Back
Top Bottom