Pugu Boys Secondary School a.k.a Pond boys

Mimi nimesoma pale enzi za Mwalimu Mkuu Magambwa, walimu kama Mabagala, Ngola,Mtela nk. Aisee Fungusi walikuwa wananitafuna sana. Siku ya kwanza kufika nikaoga bila kutumia detol. Aisee Fungus walinitafuna ile mbaya hadi kwenye anus.

Tukio la Huzuni ni siku Mwanafunzi mwenzetu alipopigwa risasi. Ilikuwa bado miezi michache amalize form six,alikuwa EGM. RIP

Namkumbuka yule mama aliyekuwa anatuuzia wali pale bondeni, Mama Pendo, Nasikia naye amekufa.

Tukio jingine na Kaka Mkuu aka Mwenyekiti wa Shule ndugu SOSTHENES BAGUME alipovuliwa cheo chake kwa kukitumia kuwanyanyasa wanafunzi hasa wa O'LEVEL.

Napakumbuka Baghdad katikati ya Pugu na Mwisho wa lami, tulikuwa tunaenda angalia Pilau
 
Giro.....umevunja mbavu zangu mpaka noma kweli! Kwenye mboga, maandazi, diet ....namkumbuka mama mmoja alikuwa anaitwa Mama Pendo....du kale Kapendo...machizi walikuwa wanakamendea kweli!
mama pendo keshafariki wakubwa,tulimzika 2009...R.I.P
 
Dah nami 2002-2005. respect kwanza kwa mwl mzava rip. mkuu magambo, mkuu shirimo. nawakumbuka kina jumanne mohamed, peter maha, ernest mtera, shakiri shakifu, deo jonas, ras ben, na 4m 4 leaver 2005. aisee tulinunuaga tshirt za jubilei haikufanyika. afu mnakumbuka shule tulizokuwa tunaletewa wasichana kwa ajili ya disco? respect all.
 
sure! rwezaula alinipa book store ya maths niisimamie. respect sana.
 

MKuu inaonekana ww wa kitambo sana mbona kwenye list yako hakuna jina la Mwl. Mkandawile? alipendelea kuwaita pugu boyz! nakumbuka alikuwa akipenda kusema ukiwasimamisha pugu boyz utawajua tu "haziwezi kupita dak2 bila kujikuna sehemu za siri" teh teh!
 
Mzee wa shamba was a legend, hivi wale akina amanda walipotelea wapi... hiyo ilikua miaka ya 1992
 
eeh ngomani nani amewahi hudhulia zile za usiku-disco vumbi.
 
Hii thread inanikumbusha mbali sana, kuna msela wangu alikuwa anasoma pugu, kila weekend alikuwa anakuja kibaha boyz kuja kuoga. Alikuwa ananichekesha sana alipokuwa ananiambia "nimechoka kupiga pond mzee!" jamaa akiingia chooni kuoga hatoki! alkitoka chooni utamsikia ebwana hapa ni Chuoni au UD?
 

Duh! Buberwa kumbe naye pugu boyz?
 

Daaah life ya pugu wakati mwingine huwa sitaki kulikumbuka...naona ni baya sana,nadhani ni moja ya sehemu nilizoishi vibaya so far.
Nakumbuka tulikuwa tukienda kujisaidia chooni tunaacha mashati nje ili kuepuka harufu isibaki kwenye shati.
Chai ikipoa tu ujue huinywi,ina test kama klorokwini-maji ya POND hayo
Mwalimu mabagala naye-MABAGUS
Kwenda shule tunapanda malori ya mchanga(nilisoma O level na A level)

Wazee mlosoma O level 1995-1999 mnamkumbuka jamaa alikuwa anajiita WASAPE (WATSUP)? jamaa alikuwa natesa form one sana yule
 
hahahaha!! mabagala alikuwa mwalimu pale pugu, alitukosesha raha sana kule kwenye bweni la MAPINDUZI
 
Mzee wa shamba was a legend, hivi wale akina amanda walipotelea wapi... hiyo ilikua miaka ya 1992

Mkuu umenikumbusha mbali, Amanda kila mtu alikuwa anamtaka yule demu!! sijui yupo wapi siku hizi...
 
sure! rwezaula alinipa book store ya maths niisimamie. respect sana.
mkuu umenikumbusha mbali sana, rwezahula, mnongalingi, baba nzoi,mkandawile, hawa walitusaidia mno "DY/DX- BOYS"(PCM)
 
..............daah, nimefurahi sana kusikia PUGU boys mpo jamvini. mimi ni ex-pugu boys...form 6 leaver 2005. ni daktari Masters degree holder kwa sasa. DOCEBIT VOS OMNIA ni TEACH THEM EVERYTHING.
mkuu mbona unataka kutuharibia mudi sasa? unaijua vizuri miaka ya kusomea udaktari? acha kuleta ubabaishaji hapa!
 
mkuu lakini huyu rwezaula si alikuwa anafundisha Advanced Maths A -Level??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…