TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Poleni sana ndugu, jamaa na marafiki zake , namkumbuka kwa ile series ya Siri za Familia alifanya vizuri sana, baadae ikapotea, I didn't know if he was such a big man and extensively used across various spheres of interests and disciplines. Na hakuwa mtu wa kuonekana sana kwenye vyombo vya habari hasa visibility kwenye camera.
 
Mungu ampumzishe mahala pema mja wake... Halafu huyu si ndio alikua muundaaji wa drama ya Siri za familia???

NB.
Kama hutajali mkuu, kuna member tulikua nae kwenye jukwaa la Great Thinkers ghafla tu niliona status yake imebadilika ikawa RIP na haikutolewa ufafanuz juu ya kifo cha member huyu. Hivyo basi ikikupendeza utujuze chanzo cha kifo cha member huyu Mlenge
Mlenge tuliletewa taarifa na familia juu ya kifo chake.

Naye alikuwa verified member. Ni bahati mbaya tulijua ikiwa late.

Sababu/Chanzo cha kifo hatuwezi kuweka (kumradhi).
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Nilimfahamia Simbanet 20 years ago, alikuwa mkarimu na msikivu sana ukifika ofisini kwake

Pumzika kwa amani Ndg yetu
 
Back
Top Bottom