TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

Dah!

My guy Superman is gone for good.

I’m at a loss for words.

Tumetoka naye mbali sana kwa kweli. JF mwaka huu inatimiza miaka 18!

Ni muda mrefu kiasi chake mpaka ‘wakongwe’ wake wanaanza kupungua.

Kuna mwaka nilishinda ‘JF Man of the year’ na yeye alihusika sana kwenye ushindi wangu huo [it was all in the name of levity, of course].

I’m so sad.

Pole za dhati ziwafikie ndugu, jamaa, na marafiki zake wote popote pale walipo.

Nitamkumbuka kwa mengi sana.

Pumzika rafiki yangu.
 
Pole sana Max na wana JF.

Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather".

Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.

Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo aliyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.

Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.Iwe kwenye biashara za mitandao au hata majibizano ya hapa JF tu.

Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.

Uko sahihi, Kila nikimkumbuka huyu jamaa, taswira yake inakuja akiwa kwenye viazi la suti nadhifu na tai.
 
Sifa zote hizi Kem Kem nina uhakika zingetolewa wakati bado akiwa Hai si tu zingependeza bali hata Yeye angezifurahia mno ila ni bahati mbaya sana anapewa akiwa Ameshafariki labda Ndugu zake walio Hai ndiyo sasa wataziona na pengine hata Kushukuru.
 
Back
Top Bottom