TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
R.I.P my Brother
 
Sanctus Mtsimbe nimemfahamu hapa JF enzi zile akiwa active sana humu. Nilibahatika kukutana nae around 2 yrs ago aki launch Zuku products. Anaonekana ni mtu mtulivu, mcha Mungu na mbunifu sana.

Rest in peace brother Sanctus Mtsimbe
 
Pole sana Max na wana JF.

Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather".

Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.

Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo aliyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.

Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.Iwe kwenye biashara za mitandao au hata majibizano ya hapa JF tu.

Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.
Munajua kumpamba mno marehemu
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Apumzike Kwa Amani
 
Pole sana Max na wana JF.

Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather".

Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.

Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo aliyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.

Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.Iwe kwenye biashara za mitandao au hata majibizano ya hapa JF tu.

Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.
💯

May he rest well!😔
 
" Maisha ya binadamu ni hadithi, basi jitahidini kuacha hadithi nzuri", Hayati Ally Hassan Mwinyi, Poleni sana na huu msiba mzito,RIP mpambanaji.

Kwanini bongo kuweka sababu ya kifo cha marehemu uwa ni big deal??
 
Back
Top Bottom