TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

Niliwasiliana na bro kuhusu kunisaidia kuweka radio yetu Tzgospel Radio Tzgospel Radio satellite alinipa ushirikiano wa kutosha na mwongozo ilikua ni vibali pekee tu nimekaribia kukamilisha kaka umeenda kaka umeendaa!

Ungesubiri basi radio iingie kwenye satellite
 
Apumzike kwa amani mkongwe Mtsimbe...

Inasikitisha sana, nimekutana na hii habari katika instagram page ya Azamtv , nikaja upande huu kuona kama kuna tanzia ya huyu mkongwe...
 
Looh, pole sana kwa familia! Naikumbuka sana michango yake hapa jukwaani!
Yeah mwenyewe ni mgeni machoni na masikioni ila inatukumbusha kutojisahau sana...tunakufa bro..daah
Mliojiunga JF miaka ya 2020 hamwezi kumfahamu huyu bwana. Naona alipunguza sana uchangiaji hapa jukwaani. Aliwahi kuleta simulizi moja nzuri sana ya vituko vya JKT ya miaka ile (siyo hii ya miezi 3).
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu

R.I.P
 
Pole sana Max na wana JF.

Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather".

Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.

Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo aliyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.

Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.Iwe kwenye biashara za mitandao au hata majibizano ya hapa JF tu.

Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.
Ni kweli, apumzike kwa amani mkwe wetu. Tuko hapa nyumbani kwenye kikao cha familia.
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
R.I.P Mwamba mwenzetu JFs.

Tangulia tunakuja
 
Shocking news ! RIP Mtsimbe.
 
Tujitahidi tunapokuwa na nafasi mbalimbali maisha yetu yaguse Watu as possible as it can take ili tusiwape watu kazi ya kutuelezea kinagaubaga ili kufahamisha waliobaki hai jinsi tulivyokuwa muhimu.

Mtu anaweza kuwa na kanafasi kadogo akagusa watu na maisha yake kuliko mwenye Macheo makubwa yaliyojaa ubinafsi.

Mnisamehe kama nimekuwa so Hatsh labda ni vile leo nimetoka msibani nikaona jinsi watu na magari yalivyojaa kumsindikiza mama huyo mzee utadhani alikuwa waziri.

Na upendo wa watoto wake ndio ulimaliza kabisa mpaka mvua iliyokuwa ikikaribia kabisa kunyesha na kulowesha kila kitu haikunyesha tena
 
Back
Top Bottom